Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. @SuluhuSamia, amempendekeza Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Chongolo kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamidu Shaka kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho kuchukua nafasi ya Humphrey Polepole ambaye aliteuliwa kuwa mbunge.
"Niwashukuru sana wenzangu UWT na wanawake wote wa Tanzania bila kujali itikadi zao, tangu nimekuwa Rais, wanawake wote wameniunga mkono, nitaendelea kuwa nanyi na sitawaangusha."- Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM.
#BREAKING: Aliyewahi kuwa mwanachama wa
@ccm_tanzania na Waziri wa Maliasili na Utalii na kisha baadaye kujiunga na @ChademaTz na kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais, @LazaroNyalandu leo Aprili 30, 2021 ametangaza kuondoka Chadema na kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Nawashukuru sana wana CCM wenzengu kwa imani kubwa mlionionyesha kwa kunichagua kwa kura zote. Najua jukumu ni kubwa, si rahisi lakini naamini nitaweza." - Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM.
Nawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kunichagua kwa kura zote (100%) kuwa Mwenyekiti wa CCM. Nawaahidi utumishi uliotukuka na CCM imara ambayo inaongoza Serikali yetu ya Awamu ya Sita.
"Niwatake viongozi wa CCM, kuacha kuwa sehemu ya kutengeneza migogoro, baina ya viongozi wa serikali na wananchi." - Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM.
"Nawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kunichagua kwa kura zote (100%) kuwa Mwenyekiti wa CCM. Nawaahidi utumishi uliotukuka na CCM imara ambayo inaongoza Serikali yetu ya Awamu ya Sita." - Samia Suluhu, Mwenyekiti wa CCM Taifa.
"Nawashukuru viongozi wa chama chetu wa zama au awamu zote zilizopita kwa umakini wao katika kukiongoza chama chetu na kukifanya kuwa imara mpaka sasa." - Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM.
Idadi ya wajumbe wa mkutano maalum ni 1909, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, nafasi ziko wazi 33, idadi wanaopaswa kuhudhuria 1876. Waliohudhuria leo ni 1862 sawa na asilimia 99- Rodrick Mpogolo, Kaimu Katibu Mkuu CCM
Ibada ya kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ikiendelea katika Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Parokia ya Mt. Augustino Manundu Korogwe. Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa Serikali wameshiriki katika ibada hiyo.
#HABARI: Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Fredius Philberth (38), mkazi wa Omurushaka wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuuwa mama yake mzazi ili apate utajiri, baada ya kuagizwa na mganga wa kienyeji apeleke damu ya mama yake ili atengenezewe dawa za utajiri.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi,Amina
Mbunge wa viti maalum, Nusrat Hanje amemuomba Rais Dkt. Magufuli kuzifuta kesi zote zinazohusu uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 ili wananchi wafanye shughuli za kuijenga nchi. "Wanasiasa kuendelea kwenda mahakamani wakati uchaguzi umekwisha hakutoi taswira nzuri kwa mataifa mengine."