Madini haya ndio chanzo cha umasikini
Madini haya ndio chanzo cha ulemavu
Madini haya ndio chanzo cha sisi kufukuzwa kwenye ardhi
Madini haya ndio chanzo cha vifo ya vijana wetu
Boniface Jacob -Mwenyekiti Kanda ya Pwani.
Kwa mujibu wa sheria, anaeisimamia kesi ni mkurugenzi wa makosa ya jinai yaani DPP, na DPP ni mkurugenzi wa mashtaka ya umma.
DPP ni mkurugenzi wetu sisi, kwa lugha nyengine sisi ndo waajiri wa DPP. Na sisi umma wa Watanzania tunamtaka DPP amuachie Lissu huru.
Mh Boniface Jacob
"Ni hawa hawa ambao mwaka 2020-2023 nilifanya kazi kubwa ya kuzungumza nao, nikanyoosha mkono wa rehema, ni kawa ambiance njooni nyie Watanzania tukae, tuzungumze yetu ili twende vile tunavyotaka, ni hawa hawa niliowakuta nje wana-suffer hawana Shilingi mkononi wakaomba sana kuja kuniona nikawapokea tukazungumza, hawana hata Shilingi. Nikatoa posho zangu nilizopewa za safari nikawapa waendelee na maisha wakiwa nje.
Ni hawa hawa waliniambia kuwa tutarudi lakini tuna kesi, nikawaambia kesi tutazifuta njooni tukae tuzungumze na tujenge nchi, walikuja walikuwa hawana kitu tukawapa fedha zetu ili waanzie maisha hapa Tanzania, sasa yule aliyewanyooshea mkono wa rehema ndio wa kwanza kumtukana, kumgeuzia mambo, kumkashifu, kuichafua nchi. Hii si tabia ya Watanzania" Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania