Uongozi na Wafanyakazi Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini KCMC, wanatoa pongezi kwa Dkt. Atukuzwe Kahakwa, kufuatia Ushindi wa Tuzo ya 2025 Coleman/Kaplan Mentorship Fund Award, inayotolewa na International Cancer Expert Corps (ICEC) nchini Marekani.
Shirika la Msamaria Mwema (GSF) kupitia taasisi zake; Hospitali ya KCMC, Chuo Kikuu KCMC, KCRI, International School of Moshi, Saint Luke Foundation na KICHAS, limewapokea rasmi wakurugenzi wapya wawili watakao hudumu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).
Uongozi wa @Kcmc1971 umempongeza CPA. Aisia Makundi kwa kufaulu mitihani ya kitaifa ya uhasibu na kufanikisha kupata Cheti cha CPA. Hii ni ishara ya juhudi, nidhamu na ubora wa kitaaluma unaojengwa KCMC katika kuhakikisha ufanisi na uwajibikaji wa kifedha unaimarika kila siku.
Hospitali ya KCMC imeendelea kuwekeza katika ustawi wa watumishi wake kwa kuwapatia mafunzo ya Afya ya Akili. Mafunzo haya yametolewa na Daktari Bingwa wa Afya ya Akili, Kim Madundo, yakiwa na lengo la kuongeza uelewa, kujenga mbinu bora za kukabiliana na changamoto za kiakili
You are welcome to register for the upcoming Focus on Mental Health conference. Use the following link to enter your information
https://t.co/87rPk31LlA
And refer to the event poster for payment details.
Mikono safi ni silaha rahisi lakini yenye nguvu kubwa katika kulinda afya zetu na za wengine. Kwa kuzingatia usafi wa mikono kila siku, tunaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali kama vile kipindupindu, kichocho na magonjwa mengine ya kuambukiza.