Leo hii ni siku ya wanawake duniani kwa niaba ya huyu mama alonileta duniani na alishatangulia mbele ya haki naomba niwape maua yenu leo akina mama wote .
Tunatambua thamani yenu kwetu sisi wanaume mmetuzaa,mnatulea,mnatuzalia watoto mungu awabariki sana kina mama wote
Hizi ndio taarifa za habari za kuangalia.
Sio hizi taarifa za WAANDISHI wanaotegemea tuzo za “KALAMU YA WASENGE”.
Uzuri wa sasa hata mkivibana vyombo vya habari vya ndani page zetu zipo zitapost na dunia inaona.
Hakuna kulia lia tena, UOVU UTAONEKANA, na HAMNA CHA KUTUFANYA.
Chama kimwombe radhi kwa kosa gani alofanyiwa vitus
Hakafu kosa chama kimemfanyia, mbona mnakuwa waongo sana hiyo CPA NA DKT alivipata chuo Gani hapa Tamzania, achen kudanganya watanzanua
Tunajuwa ninyi ni ccm
Nimesikitika Kusikia MUASISI Wa CDM Mhe. CPA Dkt Vitus Nkuna Amejivua Uanachama
Nashauri Chama Kiitishe Kikao Cha Dharura Kumuomba Msamaha Vitus
Watu Kama Vitus Wanazalia Mara Moja Kwa Karne Hivyo Kumpoteza Ni Pigo Kubwa Sana Kwa Chama
Nasisitiza Tumlinde Vitus Kwa Wivu Mkubwa
Tunajuwa mifumo ipo Nyuma yenu tunawatakia kila lenye kheri kwenu
Unakwenda kulea mjukuu then baada muda fulan utasema unakwenda Chama gani je kazi ya kulea mjukuu itakuwa imekwisha?
"Ninaitwa Grace Kiwelu ni Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro, Mwenyekiti kamati ya Fedha wa kanda ya Kaskazini na ni Mjumbe wa kamati tendaji ya Bawacha Taifa. Leo nimesimama mbele yenu kwanza kusema ahsante kwa Chama changu Chadema, kimenipa heshima, nimekuwa Mbunge, nimekuwa Mjumbe wa Kamati kuu na nimejiunga na Chama hiki tangu mwaka 1992 nikiwa Binti na leo nazeeka ndani ya Chama lakini leo nimesimama mbele yenu kwa maumivu makubwa kwasababu nitasema mwishoni ninaenda wapi.
Chama changu nilikipenda sana na nilikitumikia kwa moyo wa dhati, tulizunguka nchi nzima hii kuijenga Chadema, tulikuwa tunazunguka na Mbowe kuhakikisha Chama chetu kinaenea Tanzania nzima, tulifanya ziara wakati huo tukiwa wabunge watano tu, mimi nikiwa Mbunge pekee mwanamke kuzunguka nchi hii tukiwa na fuso, tunaweka viti, meza, spika. Tunazunguka na hatuna mwanachama hata mmoja huko tunapoenda. Tukifika tunashusha viti, tunafunga Spika, tunahutubia miti na watoto. Leo namshukuru Mungu tumefika hapa.
Lakini badala ya kuvuna heshima, tunavuna matusi. Tulishauri chama kwa nia njema kwamba tunahitaji reforms ndio lakini tusizuie uchaguzi. Unawezaje kuzuia uchaguzi wakati wewe sio mshirika wa uchaguzi? Tunafanyaje mikutano wakati tumeshasema tunaenda kuzuia uchaguzi? Tunauzuiaje uchaguzi?, wakasema tutazuia kwa maandamano. Leo wananchi wangu wa Vunjo niwaambie tunaandamana kuzuia uchaguzi, tunaanzia wapi tunaishi wapi? Wazee wangu wa Vunjo na vijana,tunaanzia wapi? Maandamano tunayofanya ama vijana wanaoandika leo kutukana baba na mama zao kwenye mitandao hutowaona kwenye maandamano. Na niwaombe sana wananchi wangu wa Vunjo, nilikuwa mmoja wa G55 kwasababu ninawajali, ninawaheshimu na ninawapenda.
Uamuzi ninaouchukua leo mnisamehe nakipenda, na niliipenda sana Chadema kwasababu ilinipa heshima sana, kufika hapa nilipofika nilijengwa na Chadema lakini sasa itoshe kusema kuanzia leo Tarehe 11 Mei, 2025 ninajiondoa rasmi Chadema, ninakwenda nyumbani- bado nina nguvu, sisemi ninaacha siasa lakini acha kwanza nikapumzike, na ninamshukuru Mungu sana kwamba Aprili 27, mwaka huu Mungu alinipa Mjukuu, nakwenda kulea Mjukuu wangu. Nimechoka na matusi ya mitandaoni kila siku.
Nilimuandikia Katibu Mkuu kwamba ninajitoa kugombea Ujumbe wa kamati kuu kwasababu ya matusi, Katibu Mkuu hajawahi kujibu meseji mpaka leo. Tuna group alianzisha Katibu Mkuu linaitwa MAMAMA, mwenyewe alilifunga kwasababu ya matusi. Leo Viongozi wanaona matusi hawakemei, kosa ni kumuunga mkono Mbowe na nilimuunga Mkono kwasababu ya mageuzi makubwa aliyoyafanya ndani na nje ya Chama chetu. Bila Mbowe tusingekuwa na Chadema hii ya leo. Ana haki ya kupongezwa, kwahiyo mimi nimechukua maamuzi tayari kwamba leo ninafikia mwisho wa kuwa Mwanachama wa Chadema, niwashukuru Viongozi wangu wa Bawacha kwa kuniunga Mkono na tutakwenda pamoja kuendeleza mapambano ya haki za wanawake na wananchi wetu, kuyafikia malengo tuliyokuwa tumetegemea kuyafikia."- Grace Kiwelu
Pole Sana Dr kitima Padre wa kanisa katoliki Tanzania
Hujaumizwa wewe peke yako limeumizwa kanisa nzima
Tumeumizwa wakatoliki wote Tanzania tunakuombea kwa mungu upone
@SShikilie77551 Ni kweli sikuwepo nauguza mgonjwa nipo Ikonda na tunaendelea vizuri kabisa nimepigiwa simu na watu wengi Sana kuuliza Hilo swali
Mm nipo chadema mpaka mwisho wa dahari