Ni zamu ya wanufaika wa Youth Economic Empowerment Dodoma kupata mafunzo ya mfumo wa kidijitali wa YEE Portal.Watajifunza jinsi mfumo unavyofanya kazi na faida zake, ikiwa ni hatua ya kuelekea dirisha la Mikopo ya 10% kutoka halmashauri
#YouthEmpowermentTz | #Mulika255
Picha ya pamoja ya Maafisa, wasichana wenye watoto katika umri mdogo na Viongozi wa Mulika Tanzania, Baada ya Youth Economic Empowerment Workshop kumalizika kata ya Ndalambo, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe.
#YouthEmpowermentTz | #mulika255
Washiriki wa mradi wa YEE for Young Mothers wilaya ya Momba Mkoani Songwe ambao ni young mothers, wakiwa katika vikundi kujadili jinsi ya kuunda vikundi, kuteua viongozi, na kuandaa katiba kwa ajili ya usajili wa Vikundi vyao.
#YouthEmpowermentTz | #mulika255
"Kabla ya matumizi mengine, ni muhimu kupanga bajeti, kutambua vyanzo vya mapato pamoja na kuweka akiba ili uweze kujenga utulivu wa kifedha na kukuza biashara yako hatua kwa hatua.” — Naamala Samson, Mkufunzi wa Masuala ya Fedha
#YouthEmpowernmentTz | #mulika255
SIDO tunatoa fursa ya kuatamia teknolojia yako ya biashara ndogo ndogo. Hii inawasaidia vijana kupata mazingira ya kujifunza na kuzalisha biashara zao kwa kutumia utaalamu unaowawezesha kufanya kazi.” — Anselm, Afisa Mipango (SIDO), Songwe
#YouthEmpowernmentTz | #mulika255
“Kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri, vijana wanaweza kupata fursa ya kuanzisha miradi yenye kuwaingizia kipato na kujikwamua kiuchumi.” —Aniceth Richard Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Momba
#YouthEmpowernmentTz | #mulika255
"Ili kikundi kiweze kusajiliwa, kunahitajika kuwa na malengo yanayoeleweka, viongozi waaminifu, katiba ya kikundi pamoja na nyaraka muhimu ikiwemo Namba za NIDA kwa wanakikundi.” —- Florentina Welya Mratibu wa Mikopo Wilaya ya Momba
#YouthEmpowernmentTz | #mulika255
“Wengi wanaamini lazima uwe na fedha nyingi ndipo uanze biashara, hata mtaji mdogo unaweza kuanza ikiwa una nidhamu na uvumilivu.
Muhimu ni kuwa na dira ya unachotaka kufikia na kutokukata tamaa.” — Ray Elimuu Afisa Biashara Wilaya ya Momba
#YouthEmpowernmentTz | #mulika255
Kupitia mradi huu, mtajengewa uelewa wa kutambua fursa zilizopo katika kata zenu zilizoko katika wilaya ya Momba na namna ya kuzitumia ili kujijengea kipato na kuleta maendeleo katika jamii zenu.” — Winfrida Mponzi, Mkuu wa Mradi
#YouthEmpowernmentTz | #mulika255
Happy Birthday to Wilbgeorge Bahati, our Communication & Advocacy Lead
Your creativity and dedication continue to inspire change and amplify youth voices. Wishing you happiness, good health, and continued success.
From all of us at Mulika Tanzania 🌸
#Happybirthday | #mulika255
Happy Birthday to our Program Lead, Winfrida Mponzi 🎉
Your dedication and passion for empowering young people continue to inspire positive impact in our communities.
Wishing you happiness, good health, and continued success.
#HappyBirthday | #mulika255
Wiki hii YEE Portal inatua Songwe! 📍
Wanufaika kutoka Wilaya za Momba na Songwe watapata mafunzo ya mfumo wa kidijitali wa YEE Portal na kujifunza faida zake katika kurahisisha upatikanaji wa Mikopo ya 10%. 💻✨
#YouthEmpowermentTz | #Mulika255
This Mother’s Day, we celebrate young mothers in the YEE Program who are turning resilience into opportunity and building brighter futures for themselves and their children.
#happymothersday | #mulika255
Happy Labour Day! Today, we celebrate the dedication, resilience, and hard work of all workers who continue to drive growth and development in our communities. We remain committed to empowering youth and creating opportunities that support decent work.
#labourday | #mulika255
Happy Union Day from Mulika Tanzania 🇹🇿
As we celebrate the unity of our nation, we reaffirm our commitment to empowering young people and communities to build a more inclusive, resilient, and prosperous Tanzania. Together, we move forward stronger as one.
#unionday | #mulika255
Tulibaini changamoto za ukusanyaji na ufuatiliaji wa taarifa kwa njia za kawaida. Mfumo huu unarahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati na uratibu wa shughuli, huku ukifuatilia maendeleo ya Vikundi — Mkuu idara ya Mawasiliano
#YouthEmpowermentTz#mulika255
Mfumo huu wa YEE PORTAL unarahisisha utaratibu wa usajili wa vikundi na wanufaika kwa njia ya kidijitali. Taarifa zinahifadhiwa sehemu moja, hivyo inakuwa rahisi kuzifikia na kuzisimamia kwa ufanisi zaidi.” — Mkuu wa Idara ya Mawasiliano
#YouthEmpowermentTz | #mulika255
Mpango wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Vijana unaendelea nchini, ukiwemo Dodoma, kupitia usajili wa Vikundi vya Mikopo ya 10%. Kupitia YEE PORTAL, changamoto za usimamizi, ufuatiliaji na uhifadhi wa kumbukumbu zinatatuliwa. — Winfrida Mponzi
#YouthEmpowermentTz | #mulika255
VIDEO RECAP 🎥 | Uwasilishaji na mafunzo ya mfumo wa kidijitali wa YEE Portal kwa wanufaika wa mradi Kiwalani, DSM. Washiriki walijifunza namna mfumo unavyorahisisha usajili wa vikundi na usimamizi wake. Mfumo bado uko hatua ya validation.
#YouthEmpowermentTz | #mulika255
Washiriki ambao ni wasichana walioapata watoto wakiwa na umri mdogo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada Mafunzo ya YEE Portal ambapo waliweza jifunza jinsi mfumo unavyofanya kazi.
#YouthEmpowermentTz | #mulika255