Kitu kimoja nawakumbusha wanangu, Gawana na wenzio ridhiki Ili ipunguze chuki..
Ama ficha sana neema zako, Ili uikimbie husda..
Watu hawapendi uwe na raha, kama una kazi, mpenzi mzuri, hela na chochote cha kutamaniwa, ficha.
Wengi wameharibikiwa kwasababu ya hasadi
Ukijifunza kukubali matokeo kwamba kuna siku utapata na kuna siku utakosa, kuna siku utafurahi na kuna siku utahuzunika maisha yanakuwa mepesi moyoni. Huwezi kufurahi kila siku, lakini unaweza kuwa na amani kila siku. 🙏💜
MAN TO MAN
Sehemu ya kazi sio mahali pa kupiga story kuhusu maisha yako binafsi wala kuongelea watu.
Nenda kazini kufanya kazi, lipwa ujira wako, kisha rudi nyumbani.
Ukikutana na watu wenye ujuzi zaidi yako, Jifunze maarifa kutoka kwao fanya nao kazi usishindane nao.
Kuwa mwaminifu, Heshimu muda wa kazi, Usiongee sana, acha kazi yako izungumze kwa niaba yako.
Jifunze kila siku, maana maarifa ndiyo mtaji mkubwa
Epuka drama za kazini utulivu hujenga taswira ya mtu makini.
Kuwa mkweli na mwajibikaji, maana uaminifu ndio unaofungua milango ya fursa na mafanikio