Someone tell @LarryMadowo that retweeting activists and calling it "news gathering" doesn't make him a journalist. It makes him an activist with a blue checkmark. #CNNFalseNarrative
When you report on a country you never visited, you're not a journalist. You're a commentator. When you push one side, you're an activist.
@LarryMadowo, which are you? #CNNFalseNarrative
Dear @LarryMadowo @CNN here is a “dead man” sitting in a morgue when you were filming your propaganda on Tanzania. Your Excellency @SuluhuSamia, October 29 and this CNN propaganda are foreign paid attacks. We are collecting every piece of evidence.
Pongezi za dhati kwako Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge), kwa dhamana uliyopewa na Taifa letu kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Umekabidhiwa jukumu kubwa na muhimu la kuiongoza Serikali, kusimamia utekelezaji wa ahadi zetu kwa wananchi na kuimarisha ustawi wa Taifa letu. Tunakuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa kazi hii.
Mwenyezi Mungu akusimamie, akuongoze na kukufanikisha kwa ajili ya Taifa letu na Watanzania wote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Siku njema sana na wananchi Uwanja wa Kaitaba.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumehitimisha salama kampeni kwa Mkoa wa Kagera, kwa kuzungumza na wananchi wa Bukoba Mjini.
Uhai na uimara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo katika kutekeleza matakwa ya wananchi. Ahsanteni sana kwa kufika kwa wingi na kuonesha ukubwa, kuaminika, kukubalika kwa chama chetu na kuridhishwa na utekelezaji wa kazi mliyotupa. Ahsanteni kwa ahadi yenu ya kuchagua wagombea wa CCM Oktoba 29.
Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Mapema leo Jijini Dar es Salaam, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimepokea Tuzo ya The GoalKeepers Award inayotolewa na Taasisi ya Gates Foundation.
Tuzo hii ni heshima kubwa kwetu Watanzania kwani mbali na sisi kufurahia matunda ya hatua kubwa tunazoendelea kupiga katika sekta ya afya, inadhihirisha dunia inatambua juhudi zetu katika kuboresha afya ya uzazi na afya ya Mama na Mtoto.
Nchi yetu imefanya kazi kubwa na ya kujivunia, ambapo mpaka sasa tumefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 80%, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi 100,000 hadi 104; na vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 67 hadi 43 kwa kila vizazi 1,000.
Kazi hii njema inaendelea ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu wa afya, kutoa huduma za afya bure kwa akina mama na watoto, kuanzisha programu za lishe, kuimarisha mifumo ya rufaa, kuboresha huduma za dharura na kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya afya mijini na vijijini.
Tuzo hii naielekeza kwa watumishi wa afya kote nchini kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana kuwahudumia Watanzania, lakini pia kwa washirika wetu na wadau wa maendeleo katika kazi ya kuboresha afya ya uzazi nchini.