@EsirEid Haya ndiyo yanawatokea walala hoi kila siku wewe tajiri umepoteza mdogo wako pole sana ila kuna wengine wanapoteza wazazi wao na walezi wao hao hawana uwezo wa kwenda kulipia hiyo VIP so pengine wewe na sisi tukaungana basi uhai wa mtanzania utakuwa salama sana
KUNA MUDA KWENYE MAISHA UNATAKIWA KUJUA THAMANI YAKO...
Kuna muda kwenye maisha unalazimika kusimama na kujiuliza, “Mimi ni nani kweli?” na “Ninastahili nini?”
Nimewahi kufika sehemu nikagundua kitu kimoja: si kila sehemu ni ya kubaki, si kila maneno ni ya kuvumilia, na si kila mzigo ni wangu kuubeba. Wakati mwingine tunateseka sana kimya kimya kwa sababu tumekubali kuishi maisha ambayo hayalingani na thamani yetu.
Kujua thamani yako ni kujitambua. Ni kuelewa kuwa una heshima, una uwezo, una ndoto, na una nafasi yako duniani. Na kama unasoma hii, labda na wewe umeshawahi kujikuta sehemu ambayo watu wanakudharau, wanakutumia, au wanataka kukuona chini ili wao wajisikie juu.
Nimejifunza kwamba si kila mtu ana haki ya kuamua kitu kwenye maisha yangu. Si kila sauti inastahili kuongoza moyo wangu. Kuna wakati unatakiwa kusema hapana kwa mambo yanayokushusha. Kuna wakati unatakiwa kuondoka sehemu isiyokupa amani. Na kuna wakati unatakiwa kujitenga na watu wanaoshindwa kuona ubora uliopo ndani yako.
Kwa muda mrefu, watu wengi wamepoteza furaha zao kwa sababu waliishi maisha ya kuwafurahisha wengine. Wakaogopa kusema ukweli wao. Wakaogopa kuonyesha hisia zao. Wakaogopa kusimamia kile wanachoamini. Mwisho wa siku wakaishia kuchoka moyo, kuchoka akili na kupoteza mwelekeo.
Na hapa ndipo nilipojifunza jambo moja muhimu: kujiheshimu si kiburi, na kujua thamani yako si dharau. Ni kujilinda dhidi ya kila kitu kinachotaka kukuangusha.
Mtu anayejitambua hawezi kukubali kutumika vibaya kila siku. Hawezi kubaki sehemu inayomuumiza bila sababu. Hawezi kuendelea kushikilia watu wanaomharibu huku akijua kabisa kinachoendelea.
Kuna watu wana uwezo mkubwa sana, lakini wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu waliamini sauti iliyowaambia hawawezi. Kuna wengine walikuwa na ndoto kubwa, lakini wakaizima kwa kuogopa maoni ya watu. Nimeona hilo likitokea sana, na pengine ndiyo maana ujumbe huu unakuja kwako leo.
Jifunze kujisimamia. Jifunze kusema ukweli wako bila kuogopa. Jifunze kuthamini muda wako, akili yako, na moyo wako.
Ukiona sehemu hupati heshima, ondoka.
Ukiona watu wanakuchukulia kawaida, jitenge nao.
Ukiona jambo linaharibu amani yako, achana nalo.
Kila binadamu ana thamani yake. Tatizo ni kwamba wengi husubiri wengine wawathibitishe kuwa wana maana. Lakini ukweli ni huu: thamani yako haipaswi kutegemea pongezi za watu. Hata dunia ikikupuuza, bado wewe ni wa muhimu. Hata watu wakikudharau, bado una uwezo wa kufanikiwa.
Mimi pia nimeshawahi kufika sehemu nikajishusha ili wengine wajisikie vizuri.
Nimeshawahi kubeba mizigo ya watu mpaka nikasahau uzito wa moyo wangu mwenyewe. Ndipo nikagundua kuwa kuna muda wa kuchagua amani yako kuliko drama za watu. Kuna muda wa kuchagua furaha yako kuliko mateso ya kuwafurahisha wengine.
Jitambue.
Jipende.
Jiheshimu.
Na usikubali maisha yakufanye uwe mtumwa wa kila jambo.
Kwa sababu siku utakapoanza kujua thamani yako, utaanza kuona dunia kwa namna tofauti kabisa.
MWANAHISABATI
#ElimuBure #UsikubaliKuwaWaKawaida
Hapa angalau NIDA mmefanya kitu kizuri.
Sitachoka kuwaambia kuna watanzania mmewapa namba
Mwaka wanaojaza kwenye fomu ni tofauti na namba.
Now wanaomba ajira but ajira zina ukomo wa mwaka.
Wakijaza namba ya nida inaonyesha wana miaka mingi.
Watu wa nida nalisema ile ni no tu
Free Online Cybersecurity Courses and Certifications in 2026.
Here are 15 FREE courses to help you master Cybersecurity 👇👇
1. IBM Cybersecurity Analyst Professional Certificate
🔗https://t.co/2jRxn10kjz
2. Microsoft Cybersecurity Analyst Professional Certificate
🔗 https://t.co/5e5eQxA84P
3. Cloud Application Development Foundations Specialization
🔗 https://t.co/9iWY5A2fup
4. Developing Applications with Google Cloud Specialization
🔗 https://t.co/Mi6gHvfJFN
5. Introduction to Cloud Computing
🔗 https://t.co/0uqyYL9iBK
6. Understanding Google Cloud Security and Operations
🔗 https://t.co/v8Z94BwtN4
7. Innovating with Data and Google Cloud
🔗 https://t.co/dnZ59ZTC9w
8. Microsoft Azure Fundamentals: Describe cloud concepts
🔗 https://t.co/gdHd2SlIra
9. GoogleCloud: Google Cloud Computing Foundations: Cloud Computing Fundamentals
🔗 https://t.co/b3CitYIFtB
10. Cloud Computing Basics (Cloud 101)
🔗https://t.co/vyKDyTcr1o
11. IT Fundamentals for Cybersecurity Specialization
🔗https://t.co/OgWdCensVa
12. Introduction to Cybersecurity Tools & Cyber Attacks
🔗 https://t.co/UbkohxmgJA
13. Cyber Security Course for Beginners
https://t.co/bBDau5ujRI
14. Introduction to Cyber Security
https://t.co/wpNGAmynDK
15. For Beginners
https://t.co/NGiPmE6aCt
Happy Learning 🌟