Rais Samia awapa neno watu wa Arusha kuelekea AFCON 2027! 🇹🇿⚽
Amewataka kudumisha amani na usafi ili kuvutia wageni wengi wa AFCON 2027 na utalii, akisisitiza kuwa hiyo ni fursa kubwa ya kiuchumi kwao.
Watu wa Arusha mmejipangaje? 👇🏽 #Arusha#AFCON2027#BongoX
Ninawashukuru wananchi wa Arusha kwa mapokezi mazuri mliyonipa nilipowasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi.
Mwakani, Arusha itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Wito wangu kwenu ni kuendelea kudumisha amani na utulivu, kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi na kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazotokana na mashindano hayo.
Macho ya wawekezaji wa madini yapo Dar es Salaam wiki hii! ⛏���🌍
Mkutano wa TMIC 2026 umeanza leo ukikutanisha washiriki zaidi ya 1,700. Fursa kubwa kwa Bongo, sawa? 👇🏽 #Tanzania #BongoX
Mwamba wa Kaskazini amerudi tena na madini mazito mtaani! 🎤🔥
Joh Makini ameachia ngoma mpya "Njia Inatoa" yenye mistari iliyoshiba haswa. Mashabiki wa Hip Hop ya Bongo, mmeipokeaje hii? 👇🏽 #BongoHipHop#BongoX
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, amesema Meli ya MV Mwanza iliyopata ajali leo kwa kugonga mwamba, ilikuwa kwenye majaribio kabla ya kuanza safari zake rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Hamduni amesema uchunguzi wa kitaalamu umeanza kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kubaini chanzo cha ajali hiyo na madhara yaliyojitokeza.
Amesema Serikali kupitia Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (TASHCO) ilikuwa katika maandalizi ya kuanza safari za meli hiyo.
#KitengeUpsates
Disbelief in Mwanza #Tanzania as recently unveiled MV Mwanza ship appears to loose control and ram the Bismarck rock and heavy smoke billows from the ship!
Haya mambo bwana! Watu hawaamini nchi imeenda mrama hivi!
#TutaelewanaTu
Enzi mpya ya Ureno bila Cristiano Ronaldo imeanza na ushindi mtamu! 🇵🇹🔥
Licha ya kucheza pungufu baada ya Pedro Neto kula umeme, Ureno wameichapa Wales 3-2, huku mrithi wa jezi namba 7, Carlos Forbs, akitupia bao la ushindi! Mnaona Carlos Forbs atamudu viatu vya CR7? 👇🏽⚽ #UEFA
Uzoefu mkubwa unaenda kwenye sekta ya elimu na kilimo! 🎓🌱
Rais Samia amemteua Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango, kuwa Mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha SUA akichukua nafasi ya Jaji Warioba. Watu wa Morogoro na wanafunzi wa SUA mmeupokeaje uteuzi huu? 👇🏽🇹🇿 #SUA#BongoX
Maridhiano ya kweli yanahitaji sauti za wananchi wote, siyo makubaliano ya wachache! 🗣️🇹🇿
Wakosoaji wanahoji iwapo mazungumzo na vyama vilivyoshiriki uchaguzi yataleta mabadiliko bila kwanza kutatua madai ya haki na uwajibikaji. Unadhani hatua hii itamaliza mgawanyiko? #Tanzania
#HABARI Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mazugumzo na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, huku akisema ni wakati mwingine wa kuendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Novemba 16,2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa kikao hicho kimefanyika Ikulu ya Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Rais Samia amelishukuru Baraza hilo pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kwa utayari wao wa siku zote za kufanya mazungumzo ya majadiliano yha kuimarisha misingi ya Taifa letu.
“Sasa ni wakati mwingine wa kuendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi kwa kuunda Tume ya Maridhiano na upatanishi, itakayoratibu maandalizi ya mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania,” imeeleza.
Kikao cha Rais Samia na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kinaendeleza hatua za mashauriano ya Mkuu huyo wa nchi na wadau mbalimbali kuhusu mchakato huo wa maridhiano.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
Naona mmefanya kwa siri 😁
Hiki kikao batili kwishbey! Haina impact! Mlichodhamiria muioneshe kimataifa imefeli! Mnajitekenya na kucheka wenyewe
#SamiaMustGo
Katika azma ya kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa, pamoja na kujenga uelewa na uamuzi wa pamoja kuhusu masuala ya nchi yetu, leo nimekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Tumekuwa na mazungumzo yenye tija kuhusu namna bora ya kusonga mbele katika mchakato wa Maridhiano na hatimaye Marekebisho ya Katiba, kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa letu.
Kusubiri ajira pekee siku hizi ni kujichelewesha mwenyewe! 💼💡
Vijana wengi wameanza kujiajiri kwenye biashara ndogondogo na huduma za mtandaoni na wanapiga hatua nzuri. Kama ungepewa mtaji wa milioni moja leo, ungeanza biashara gani mtaani kwako? 👇🏽🇹🇿 #BiasharaTZ#BongoX
Mvua za burudani kutoka kwa Wakongwe wa Bongo Fleva sasa zinaelekezwa Kahama, burudani zitakazonyesha kwa kishindo Novemba 27, 2026, ndani ya ukumbi wa Malex Hall, Kahama, katika sherehe za miaka 30 ya Bongo Flava.
Mtonyo wa kushuhudia burudani kutoka kwa Wakongwe hawa unaanzia shilingi 50,000 kwa REG, shilingi 100,000 kwa VIP, Tsh milioni 1 kwa VIP Table ya Watu watano na shilingi milioni 3 kwa V-VIP Table ya Watu wanne.
#MillardAyoUPDATES
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua maombi kadhaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kikipinga kitendo cha Jeshi la Polisi kuwashikilia viongozi na wanachama wake kwa muda mrefu bila kuwafikisha mahakamani.
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Gaston Shundo Garubindi, amesema kesho Jumatatu, Novemba 16, 2026, Mahakama Kuu, Masijala ya Dar es Salaam, itasikiliza maombi namba 25432/2026 yaliyofunguliwa na Fadhil Benedict Mbeya dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na wenzake.
Garubindi amesema maombi hayo ya *Habeas Corpus* yamewasilishwa kufuatia madai ya kushikiliwa kwa Mbeya na Polisi tangu Oktoba 10, 2026, bila kupewa dhamana ya polisi wala kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria. Shauri hilo litasikilizwa mbele ya Jaji Awamu Mbangwa.
Amesema pia maombi mengine yamewasilishwa Mahakama Kuu, Masijala ya Mbeya, na Gwamaka Mbughi, Katibu Mstaafu wa Kanda ya Nyasa, Hamad Mbeyale, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Rodrick Alon Mwazembe, Mwenyekiti wa CHADEMA wa ngazi ya kata, pamoja na wanachama wengine.
Katika maombi hayo, viongozi na wanachama hao wanapinga kushikiliwa kwao kwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani. Wengine waliotajwa ni Gidfrey Asubisye, Musa Tomson, Thomas Phillipe, Aman Sango na Yusuph Benito Mwakisunga.
Aidha, Garubindi amesema maombi kama hayo yamewasilishwa Mahakama Kuu, Masijala ya Kigoma, kufuatia madai ya kushikiliwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma, Neema David Mhanuzi, Ismail Amos Nyarubida na Noah Metta Kirabila tangu Novemba 5, 2026.
Katika taarifa yake kupitia mtandao wa X, Garubindi amedai kuwa hakuna sababu zilizoelezwa kuhusu kushikiliwa kwa viongozi na wanachama hao, huku akitaja taarifa zinazodai kuwa baadhi yao walikamatwa kwa maelekezo na wanasubiri maamuzi ya waliotoa amri hizo.
Wakati huohuo, amesema kesi ya Jamhuri dhidi ya Lucy Simon Shayo mkoani Morogoro itaendelea kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha mashahidi. Garubindi amelitaka Jeshi la Polisi kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yake, akisisitiza kuwa kushikilia watu kwa zaidi ya wiki mbili bila kuwafikisha mahakamani ni jambo linalokwenda kinyume na misingi ya utawala wa sheria.
Ujumbe wa Waziri Katambi upo wazi; tutumie mitandao kwa ustaarabu na tuache kusambaza uzushi au matusi! 📱⚖️
Usalama unaanza na sisi wenyewe. Mnakubaliana naye? 👇🏽🇹🇿 #BongoX