Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), Rufiji, Pwani
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutuwezesha kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa Taifa letu. Hii ni hatua ya kujivunia katika safari yetu ya kuendelea kufanya kazi ya kujikomboa kiuchumi, ili kuiishi maana halisi ya Uhuru wetu, pamoja na malengo na ndoto za waasisi wetu.
Hongera kwa kila Mtanzania.
Ikulu Chamwino, Dodoma
Imekuwa siku njema yenye baraka kukutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Tumezungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa, yakiwemo amani, mshikamano, maendeleo na nafasi ya viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye maadili na uwajibikaji.
Nimewashukuru Maaskofu kwa mazungumzo haya yenye tija, na nimewahakikishia dhamira yangu ya kuendelea kushauriana na kushirikisha viongozi wa dini na makundi mbalimbali, katika masuala muhimu yanayojenga mustakabali wa Taifa letu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah wakati walipokuwa wakizungumza na dereva wa basi liendalo haraka Bi. Happyness Aloyce baada ya kufika katika Kituo cha Mbagala mwisho Jijini Dar es Salaam, tarehe 07 Agosti, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja na Rais wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa Joรฃo Manuel Gonรงalves Lourenรงo kama ishara ya uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026. Kulia ni Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa akishuhudia tukio hilo. Hospitali hiyoimepewa jina la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama heshima na ishara ya kutambua mchango wake katika harakati za ukombozi waBara la Afrika, hususan nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Angola.
Baada ya kuwasili jijini Luanda, Angola kwa ziara ya kikazi, nimekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wangu, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa Joรฃo Manuel Gonรงalves Lourenรงo.
Katika mazungumzo yetu, tumesisitiza umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Angola. Wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika mataifa yetu yalishirikiana kufanikisha uhuru wa kisiasa; sasa ni wajibu wetu kuimarisha ushirikiano huo katika nyanja za uchumi, biashara, uwekezaji na maendeleo ya kijamii kwa manufaa ya wananchi wetu, tukitekeleza maono ya waasisi wa mataifa yetu.