#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 148
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja yangu ya nne Waheshimiwa Majaji ipo kwenye kanuni ya 6(2) ambapo Mahakama inaweza kutoa amri bila kuathiri haki ya kusikilizwa kwa usawa.
Waheshimiwa majaji naomba hiyo kanuni isomwe pamoja na kanuni ya 5(2)(f) ambayo inasisitiza kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kwamba kuna effective cross examination.
Waheshimiwa Majaji naomba mtafakari hayo maneno ya mahitaji ya fair trial, kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kuna effective cross examination.
Waheshimiwa majaji kwenye kesi ambayo adhabu yake ni kifo, shahidi akatoa Ushahidi ambaye Mahakama haimfahamu, mshtakiwa hamfahamu isipokuwa tu mawakili wa serikali.
Shahidi akitoa Ushahidi bila mahakama kumuona, majaji hawamfahamu, mtuhumiwa atafanyaje effective cross examination? Shahidi asiyejulikana na Mahakama, haonekani kwa mtuhumiwa itatoaje uamuzi ambao hauhatarishi maslahi ya haki?
Waheshimiwa majaji kuruhusu Ushahidi wa namna hii itakuwa ni a mockery of justice and just adjudication of cases by the court, hakutakuwa na haki kabisa.
Waheshimiwa Majaji katika mazingira haya shahidi akiruhusiwa kutoa kinachoitwa Ushahidi wake:
Mahakama itajuaje demeanour of the witness?
Hii haitakuwa fair hearing, hakutakuwa na usawa mbele ya sheria, mtahakikishaje waheshimiwa majaji kuwa kutakuwa na usawa mbele ya sheria kama ambavyo Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya JMT inasema.
Tunapozungumzia usawa mbele ya Sheria hatuzungumzii kanuni zilizotungwa na Jaji Mkuu tu peke yake, tunazungumzia kanuni za kikatiba pamoja na Ibara ya 107A ambayo inaweka sharti kwamba Mahakama lazima itende haki sawa kwa wote.
Waheshimiwa majaji hili litawezaje kutekelezwa kama mtaruhusu mashahidi msiowajua na msiowaona kutoa Ushahidi? Waheshimiwa majaji nawaomba msije mkakubali kutumika kuharibu utendaji haki katika mahakama zetu, don’t ever allow.
Labda nichomekee jambo hapa kidogo. Ukiachana na Mh. Lissu anaongea Sheria lakini lolote analosema linamuingia kila mtu akilini na moyoni. Ukiwaangalia hata Majaji ni kama wanasema unachokisema tunakuelewa kabisa na ndio ukweli wa Mungu lakini tutafanyaje sasa? Hiyo ndio impression tunayoiona hapa Mahakamani tukiwa tunawatazama majaji na hata mawakili wa Serikali. Ukiwaangalia hata mapolisi waliopo humu nao sura zao zinasema ni kweli hatujui sheria sisi kama mapolisi ila anayosema Lissu yanaeleweka na ni sahihi.😂
Waheshimiwa majaji haya niliyoyasema ya misingi ya haki yamewekwa pia katika mikataba mbalimbali ambayo nchi yetu imeridhia.
Naomba niwape mifano, Ibara ya 2 , 7, 10 and 11 za Tangazo la Haki za Binadamu of UDHR 1948, Ibara ya 14(1) , 14(3) (e ) na 26 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kirai na Kisiasa wa Mwaka 1966 (ICCPR) zote zinazungumzia usawa mbele ya Sheria, ulinzi sawa mbele ya sheria.
Waheshimiwa majaji naomba kuwasomea Ibara ya 14(3)(e) of ICCPR inasisitiza kuhusu in full equality, mkiruhusu shahidi ambaye hamumjui, hamumfahamu, mimi simuoni na wala simfahamu, hiyo in full equality itatoka wapi?
Vilevile Ibara ya 3 na 7 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu, ibara ya 6(d) na 7(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rules of Procedure International Residual Criminal Procedure Mechanisms hizi zimeweka gold standard na best practices za umoja wa Mataifa hivyo mahakama zetu zinaweza zikazitumia hasa kanuni ya 75A, 75C, 86A na 86B.
Waheshimiwa Majaji hizi kanuni 4 ndio best standards za kulinda mashahidi, hivyo utaratibu huu upo sio kwamba umegunduliwa na mawakili wa serikali na hazina hii darkness tunayotaka kuletewa hapa (Lissu anaonyesha kizimba alipojificha shahidi wa leo),😂😂
Utaratibu huu hauwezi kuleta fair trial, mkiruhusu huu utaratibu unaotaka kuletwa hapa then we must forget about fair trial.
Part 149 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo November 12, 2025.
Last time tuliishia part 145, Leo tunaendelea na-;
Part 146
Mheshimiwa Lissu ameingia Mahakamani kama kawaida akiwa na vibe amekoroga "amezungusha ngumi" akiwa na morali ya kutosha.
Kama kawaida ameambatana na maaskari magereza wakutosha ambao huwa wanamlinda.
Siku za karibuni tulisema sehemu ya askari hawa wamekuwa ni wapya sio tunaowafahamu wa siku zote.
Inapigwa High Courttttttttt kubwa sana na kali.
Watu wote wamesimama hapa na Majaji wanaingia.
Sauti ya Askari imeendelea hadi Majaji wamefika kwenye viti vyao na kukaa ndio ameacha huyu askari.
Mawakili wa Serikali wamejitambulisha na kusema leo wana shahidi na wako tayari kuendelea na kesi.
Shahidi waliyenae leo ni shahidi wa siri ambae ni P11 kwahiyo wako tayari kuendelea Jamhuri.
Anaulizwa Mh. Lissu kama na yeye yuko tayari.
Mhe. Lissu anasema:
Niko tayari waheshimiwa lakini naomba niseme neno dogo tu sio la kuweka kwenye rekodi.
Jaji anashangaa sio la kuweka kwenye rekodi ni jambo gani hilo na lina umuhimu gani sasa?
Mhe. Lissu anajibu ndio waheshimiwa majaji sio la kuweka kwenye rekodi na neno langu sio lingine bali ni kwamba,
Nimefurahi kuwaona maana huko nilikokuwa hizi wiki mbili hakukuwa kwa kawaida.
Watu wote wameangua kicheko mahakamani hadi Majaji wamecheka.😂😂😂
Anaendelea Mh. Lissu
Mh. Jaji hapa Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameiambia Mahakama kuwa kuna mashahidi wengine wa Siri na hivyo leo tutakuwa na Shahidi P11.
Huyo Shahidi wa siri ameingia na Mahakama haijamuona.
Sasa nina pingamizi, waheshimiwa majaji huyo shahidi wa siri anatakiwa asimame kwenye kizimba na sio huko ambako haonekani.
Napenda kuwafahamisha kwamba hili suala la ulinzi wa mashahidi, nimelitafakari kwa zaidi ya miezi 6 sasa na nimeliangalia kwa makini sana.
Naomba kutoa hoja kwamba, hakuna shahidi yoyote kwa amri iliyotolewa na mahakama hakuna shahidi hata mmoja ambaye anatakiwa kutoa Ushahidi akiwa hapo kwenye kificho, anatakiwa akae hapo kizimbani.
Naomba nianze na sheria kwamba inasema nini? hapa Lissu ameandaa nondo za kutosha naona yuko imara kuanza pambano hili la kisheria.
Mahakama imejaa utulivu na kamvua kameanza kunyesha kwa mbali.
Watu wametulia utafikiri wanasubiri kuchomwa sindano au wanasubiri kupewa utaratibu wa kuanza kumuaga marehemu. Utulivu ni mkubwa sana.
Naomba nianze na sheria sasa kwamba inasema nini kuhusu hawa wanaoitwa Mashahidi wa siri?
Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025, zimeeleza hicho kiboksi hapo ni kitu gani kisheria?
Sasa kisheria kinaitwa kizimba maalum cha shahidi na kwa kanuni hizi kizimba kimetafsiriwa kwenye kanuni ya 3 kuwa ni sehemu ya kusimama au kukaa wakati wa kutoa Ushahidi iliyoandaliwa mahususi ili kutoa Ushahidi bila kuonekana isipokuwa na Jaji au Hakimu.
Nasisitiza isipokuwa kwa Jaji au Hakimu. Sasa swali Je hapo alipokaa shahidi waheshimiwa Majaji mnaweza kumuona huyo shahidi?
Majaji wanashangaa na kila mtu anashangaa, Waheshimiwa majaji kwa macho yangu shahidi hapo haonekani kwa majaji, wala mimi simuoni. Watu pekee wanamjua ni hawa mawakili wa serikali waliomleta akina Katuga.
Mhe. Lissu anaendelea kuweka ngumu kuwa huyo shahidi asiyeonekana kwa majaji, kwa mshtakiwa ni shahidi wa namna gani?
Kwa misingi gani ya haki katika dunia hii? Mhe. Lissu anahoji huyu shahidi anapaswa kusikilizwa.
Labda nichomekee kidogo ili mpate picha. Hicho kibox anachosadikika shahidi kipo sehemu ya juu pembeni kidogo na mlango wanaoingilia majaji.
Ni kibox kimetengenezwa kama kasanduku hakuna mtu unaweza kumuona ukiwa upande wowote maana kimezungushiwa pande zote nne so huwezi kumuona kabisa. Pia hakijawekwa hapa kwa sehemu ya mashahidi wanaposimama siku zote. Kiko kule juu kabisa. Hata majaji hawawezi kumuona aliyepo ndani ya hicho kibox chao. Kwa mbele kina kama kioo kidogo lakini pia huwezi kuona ndani kuna nini kupitia hicho kioo.
Part 147 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.