Maisha haya yanapita kama upepo. Usipoona thamani ya siku moja, wiki moja, mwezi mmoja, kufumba na kufumbua, kitenzi kikurupushi kinaanza kukuandama. Ukiwa na miaka 20 ni kama huoni kikwazo chochote mbele yako. Muda unao. Ukitazama mbele unajiona ukipata kila unachokihitaji. Huambiki. Hushauriki. Rahisi sana kupotelea kwenye shughuli zinazokuwekea akiba nzuri ya majuto miaka ijayo.
Ukiwa na miaka 30, na bado hujakarabati tabia zako vizuri, unaanza kugundua mambo sio rahisi kama ulivyofikiri. Kazi ulizozibeza ukiwa na miaka 20 na, kumbe nazo ni ngumu kuzipata. Unaanza kugundua kumbe mahusiano si rahisi kama ulivyofikiri. Unaowapenda hawakupendi na wanaokupenda huwaamini. Kumbe si kila mtu kaumbiwa furaha ya mahusiano. Unajielekeza kwenye kazi ambazo nazo haziendani na ndoto zako. Unaanza kuwa na hofu ya mengi lakini bado unaona muda upo.
Ukiwa na miaka 40 unaanza kuukabili ukweli ulioukwepa kwa muda mrefu. Unaanza kuuishi upweke wa kukosa mtu wa kumwamini. Unaanza kupambana na matokeo ya kuishi maisha yenye mafanikio yasiyokuwepo. Matokeo ya maamuzi uliyofanya miaka 20 iliyopita yanaanza kukuwinda. Unaanza kuishi kwenye ninge, ningefanya hivi, ningekuwa vile. Unaanza kuona ulivyo na mengi ya kufanya na muda huna. Jumatatu, mara Jumamosi hii hapa. Tarehe 1, mara tarehe 30 hii hapa. Muda huna. Unawasahau watoto. Unaitelekeza familia.
Mara unaanza kuona mvi moja moja. Mara huzioni tena siku zako. Mara unaanza kupewa shikamoo na watu unaoamini mnalingana. Kufumba na kufumbua miaka 50 hii hapa. Kila mpango wa muda mrefu unaanza kuuogopa. Hata taasisi za fedha zinaanza kuwa na tahadhari na wewe. Kazini, kama umeajiriwa, wanaanza kukuona kama mzigo. Ubabaishaji wa miaka mingi unaanza ‘kukulipa’. Hakuna anayekuamini. Rika lako wanakuwa viongozi. Unaanza kuongozwa na vijana. Unaanza kuutafuta utulivu. Hupendi tena maeneo yenye kelele. Unaanza kuwaelewa wazee uliofikiri enzi hizo kuwa hawakuwa wapambanaji.
Mara umestaafu. Unatamani uendelee kuchapa kazi na mwajiri anakushangaa. Unawalaani watoto wako ambao nao wanashangaa upendo huu wa ghafla umeutoa wapi. Haikuwa kawaida yako. Unailaani serikali wa kusababisha ufarakane na familia yako. Unaulaani mfumo wa hifadhi ya jamii. Unawalaani viongozi wa dini kwa utapeli. Unalalamika muda wote. Unabaki kuwa mzee mpweke. Ukitazama nyuma unatamani ungepewa nafasi ya pili urekebishe makosa.
Tunajifunza nini? Hata sijui. Rudia tena kusoma utafakari kimya kimya. Ukweli mchungu ni kwamba maisha ni ‘mpandiano’ wa maamuzi madogo madogo, ambayo wakati mwingine, hayakupi nafasi ya pili kufanya marekebisho. Unaweza kuchagua aina ya maamuzi unayoweza kufanya leo (na hakuna mtu wa kukuingilia) lakini huwezi kuchagua matokeo ya maamuzi yako.
@pastajoshuatz Movie na simulizi pia ni mzuri hongera kwake ila next hawe makini kidogo na kwenye kuendana na uwalisia mfano kuna mama moja ana onekana amevaa viatu vya kisasa kabisa.
Ingawa haipunguzi kiasi cha sukari kilichopo kwenye chakula chenyewe, Siki (Vinegar) husaidia kudhibiti Sukari mwilini kwa kuchelewesha usagaji wa chakula na kuzuia Sukari isipande kwa kasi kwenye damu baada ya kula
Ulikuwa unajua Mbinu hii kabla haujasikiliza hii video? Share nasi kwenye komenti
Video: Muhimbili TV
Hivi unajua akili huwa haipendi hali ya sin’tofahamu na kitu kisichoeleweka? Unafahamu akili huwa haipendi hali ya taharuki inayetokana na taarifa zisizo na ukamilifu wake na hivyo inaweza kuzirekebisha taarifa ili tu kutengeneza ‘amani’ ya uongo akilini?
Mshunuzi Arie Kruglanski (mzaliwa wa Polandi, anayefundisha Chuo Kikuu cha Maryland, Marekani) aligundua kitu kinachoitwa “tabia ya akili kuhitimisha” inayotokana na akili ya binadamu kuchukia hali ya kutokuwa na uhakika. Woga huu wa kitu kisichokamilika, huifanya akili ya mwanadamu ikose utulivu ambao wakati mwingine huwa ndio msukumo wa kukubali jibu lolote lililopo hata kama ni wazi halina usahihi kabisa lengo likiwa “kulifunga” suala husika na kuacha kufikiria kitu kisicho na majibu.
Hiki anachokisema Kruglanski kinafanana sana na kanuni ya Gestalt ya ‘Closure’ inayosema kwamba akili zetu hujitahidi kukamilisha picha (mchoro) usiokamilika ili kupata “taswira kamili” ya jambo ambalo wakati mwingine halipo. Kwa maana nyingine akili zetu huwa hazipendi mapengo mapengo na hupambana kujaza kinachopungua hata kama ni kwa kutumia dhana ya kuunga unga.
Kumbe saa nyingine una maoni makali, unamchukia mtu, kwa vile umeiruhusu akili yako imalizie kitu usichokielewa vyema. Kinachoshangaza zaidi, hata baadae unapopata taarifa sahihi, bado akili yako huendelea kusimamia hitimisho ambalo tayari ulikuwa nalo hata kabla ya kuwa na taarifa zote.
Una mfano gani wa karibu unaoelezea vizuri hiki anachokisema Kruglanski? Umewahi kuwa na maoni makali sana kwa jambo halafu baadaye ukagundua ulikurupuka? Umewahi kukubali maelezo mepesi mepesi ili tu kufunga mjadala wa jambo lisiloeleweka?