@MariaSTsehai@SuluhuSamia Tanzania imepiga marufuku kuanzisha vikundi vya kijeshi visivyo rasmi, kwa kuwa vinahatarisha usalama wa taifa, kuvuruga amani, na kukiuka sheria. Serikali inasisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama ndivyo pekee vinavyoruhusiwa kubeba silaha na kusimamia ulinzi wa raia.
Mwigizaji Gabo ameitambulisha Tamthilia yake mpya ya BARALUKO ambayo amesema itakua hewani kuanzia siku ya Kesho kupitia YouTube channel yake na sio Kwenye tv station ambapo ameeleza kuwa lengo lake ni kuwafikia Watu wake wengi haswa walioko nje ya Nchi ambao wamekuwa hawapati kuona kazi zake.
Salim Ahmed maaarufu kama Gabo Zigamba leo amefanya uzinduzi rasmi wa Tamthilia hiyo mpya fupi inayojulikana kwa jina la BARALUKO mbele ya Vyombo vya Habari na Wadau mbalimbali wa sanaa na Tamthilia hii imekuja baada ya Mashabiki zake walipoburudika na kuelimika katika Tamthilia ya Mawio.
Aidha Gabo amesema Tamthilia hii ya Baraluko imedhamiria kuonesha maisha ya Mtanzania yaliyobeba uzuri na ugumu wa mahusiano ya kifamilia sanjari na hilo pia limelenga kutoa elimu kwa Jamii sambamba kuibua mijadala Chanya kwenye Jamii yenye lengo la kujenga na kutengeneza hoja zenye mashiko katika Jamii yetu na Tamthilia inawahusisha Waigizaji wakubwa akiwemo Gabo Zigamba mwenyewe ambaye ndiye Muhusika mkuu wa Baraluko, Zulfa Msomali, Mary Mawigi na wengine wengi, ikionesha maisha ya ndoa, Familia, usaliti, changamoto za mahusiano, huku ikitunza na kuenzi mila na tamaduni za Kitanzania.
“Wengi watajiuliza wataipata wapi Baraluko na kwa gaharama ya kiasi gani basi tuwatoe shaka kwamba Tamthilia hii itapatikana bure kabisa kupitia YouTube channel ya Gabo Zigamba kwa kila wiki pia vilevile na vipindi vingine vitaendelea kutolewa kila wiki kupitia channel yetu.”- Gabo
#millardayoENT
@TanzaniaLeaks Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeanzisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 2,000 kwa ajili ya polisi ili kuboresha makazi na mazingira yao ya kazi. Nyumba hizi zinajengwa katika mikoa mbalimbali, zikiwemo za kisasa, ili kuongeza motisha na kuimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma.
@TanzaniaLeaks Rais Samia Suluhu Hassan amelipa madeni ya nyuma ya polisi, ikiwa ni pamoja na posho na malimbikizo ya mishahara, huku akiwapandisha vyeo maelfu ya askari. Hatua hii imeimarisha ustawi wa polisi, kuongeza morali kazini, na kuboresha huduma za usalama nchini Tanzania.