Wizara ya mambo ya ndichi ina~deal na petty issues….badala ya ku~deal na vitu serious.
Waziri una deal na mashalove & Pipitilda
badala ya kulinda mipakani huko zinaingia pombe feki daily zinaenda kuua figo za maelfu ya mahomeboys na dada zetu, ajira zenyewe hamuwapi vijana wanashindwa kumudu dialysis gharama wanapoteza maisha!
Halafu hapo utasema wizara inalinda raia na mali zake!!?🤷♂️
Unazungumzia maadili ya kuongea lugha chafu mitandaoni, USA 🇺🇸 Rais Trump anatukanwa na raia ile F****word tena public kabisa kwenye press na raia haguswi na ndio nchi ina mahospital bora,shule na vyuo bora, umeme & maji havikatiki,barabara safi, na ajira za kutosha!!
Wewe maadili yamekusaidia nini mtu nina bachelor ya Architecture GPA 3.5 na naendesha boda tena ya mkataba mwaka wa nne huu kazi hamna, kwa siku naingiza elfu saba, utasema kuna maisha hapo?
Wewe unaekazania maadili una population ya watu milioni 70, unatangaza ajira elfu 45!!
Sasa kuna taifa hapo?
Simaanishi kama taifa tusiwe na maadili au utamaduni, lakini ni petty issues….. kundi la wale mates wangu walipaswa kuitwa hata basata tu wakamalizana nao chaap kwa, kama wazazi/walezi……easy tu, lakini sio waziri wa wizara!!
Kama tunataka kukemea maadili, tukemee maadili ya utekaji na ufisadi na mauaji ya ndugu zetu, hayo ndio maadili ya msingi na uwaite wahusika uwakemee live tuone kama tulivyoona kwa wale wasanii!!
Unaacha kuwaita askari walioua ndugu zetu october 29 uwakemee na kuwawajibisha, unamuita yule sista du anayeuza jeans, unamuita Nicole….kisa anaonyesha kifua!!?
Nini kifua babu, nchi za wenzetu unakuta striper anacheza uchi kabisa usiku club na mchana ni daktari / nurse anatibu watu na ndio ajira yake na analipa kodi na hela anayotengeneza humgusi….na ana degree kasoma na husikii kaitwa na waziri wala Mkuu wa mkoa! Dunia ndio ipo huko!!
CAG kila mwaka anasoma report wizi wa Billions of bags 💰 na huoni mtu akiwajibishwa…..sasa hayo ndio maadili ya kukemea public tena, sio mtuambie tunamalizana kwenye vikao vya kamati sijui za halmashauri…NO!!
Watu wanatekwa kiholela, wanapotea wanakufa….kila kiongozi anayehojiwa anakataa kuwa hakuna utekaji….husikii hata mmoja akikemea…..then leo wizara ya mambo ya ndani head liner unakaa kikao na GiGi money, Anko T unawakemea na mnalazimisha kabisa iwe news kubwa!!
Yani hukemei mtu anaua watu, unakuja unamkemea gigi kavaa mpasuo!?
Hivi tuna taifa kweli hapa jamani!?
Hii nchi ina maigizo sana!!
"Kujibu kunaweza kuamsha hasira zilizolala, kunaweza onyesha ujinga wako, kunaweza toa taarifa za ziada, kunaweza kukunasisha kwenye mtego, na kunaweza kuhitimisha dhana fulani watu walizonazo juu yako. Kutokujibu hakumaanishi huna majibu, bali kwaweza kuwa kipimo cha busara."