“Shughuli ya kuwashughulikia kina John Heche na washirika wake CHADEMA sisi tunaiweza. Wale nilishawapiga marufuku mkoani Kagera, walikuwa hawaingii. Tuliwaambia hatutaki siasa za udalali, siasa za uongo na siasa za kuwagawa Watanzania,” Faris Buruhani, Katibu Mkuu wa UVCCM
Watoto watatu wa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Cleopa Msuya, wameingia katika mvutano wa kisheria kuhusu usimamizi wa mirathi ya baba yao, huku Mahakama Kuu ikifungua njia ya kusikilizwa kwa maombi ya kulinda mali za marehemu.
Katika uamuzi uliotolewa Oktoba 13, 2026, Jaji Sara Mwaipopo wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Temeke, alitupilia mbali mapingamizi matano kati ya sita yaliyowasilishwa na John Msuya na Naanjela Msuya dhidi ya maombi ya Job Msuya, aliyekuwa akiomba amri za muda za kuhifadhi mali za mirathi.
Job, kupitia Wakili Albert Lema, aliiomba mahakama kuingilia kati akidai wasimamizi wenzake walikuwa wakifanya maamuzi kuhusu mali za marehemu bila ridhaa ya pamoja. Pia alieleza wasiwasi kuhusu nyumba iliyopo Upanga, akidai ilikuwa katika hatari ya kuuzwa kwa bei ya chini au kukodishwa kwa masharti yasiyozingatia masilahi ya mirathi.
Wasimamizi hao waliwasilisha mapingamizi sita wakidai maombi hayo hayakuwa na msingi wa kisheria, yalikuwa yamewasilishwa mapema kabla ya kukamilika kwa orodha ya mali, na kwamba kulikuwa na shauri jingine lenye hoja zinazofanana. Pia walipinga hati ya kiapo ya Job na kudai maombi yalikuwa yamepitwa na muda wa kisheria.
Hata hivyo, Jaji Mwaipopo alieleza kuwa mahakama ina mamlaka ya kutoa amri za kuhifadhi na kulinda mali za mirathi hata kabla ya kuwasilishwa kwa orodha ya mali, hasa pale kunapokuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa mali kuuzwa au kuharibiwa. Pia alibaini shauri jingine lililotajwa na wajibu maombi lilikuwa tayari limefutwa.
Jaji alikubali kwa sehemu pingamizi kuhusu hati ya kiapo, akiamuru aya za 7, 20, 21, 23, 24, 25 na 26 zifutwe kwa kuwa zilikuwa na kauli za imani, maoni na hoja za kisheria ambazo hazikupaswa kuwasilishwa kwa namna hiyo. Hata hivyo, alikataa ombi la kutupilia mbali hati nzima, akisema kasoro katika baadhi ya aya hazibatilishi hati yote.
Cleopa Msuya, aliyewahi pia kuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Viwanda na Biashara, alifariki dunia Mei 7, 2025, katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam. Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa maombi ya Job kuhusu uhifadhi na usimamizi wa mali za marehemu yataendelea kusikilizwa, huku mahakama ikitarajia kuchunguza hoja za msingi kabla ya kutoa uamuzi kuhusu nafuu anazoomba.
#HABARI Damas Mgaya (38), mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake kwa kutumia kamba ya kiatu, kufuatia madai ya mgogoro wa kifamilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa jana, Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi, akieleza kuwa marehemu alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha.
Kwa mujibu wa Kamanda Banga, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na kutokuelewana kati ya marehemu na mkewe kuhusu masuala ya ndoa na tendo la ndoa.
Inadaiwa kuwa mke wa marehemu alikataa kushiriki tendo la ndoa akieleza kuwa mumewe hajaokoka, hali ambayo inadaiwa kuchangia mgogoro huo wa kifamilia na kumsababishia marehemu msongo wa mawazo.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Banga ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhimiza mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano katika familia na jamii, huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua kwa vitendo vinavyokiuka sheria.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
#WNBA SEMIFINALES
DOM 4/10 - J1
15.00 ATLANTA - NEW YORK
17.00 GOLDEN STATE - LAS VEGAS
MIE 7/10 - J2
20.30 ATLANTA - NEW YORK
22.30 GOLDEN STATE - LAS VEGAS
VIE 9/10 - J3
20.30 NEW YORK - ATLANTA
22.30 LAS VEGAS - GOLDEN STATE
De ser Necesario
DOM 11/10 - J4
MIE 14/10 - J5
"Kuna mtu alikuwa unazungumza kwamba ‘waliokufa’ [Oktoba 29]. Wale hawakufa. Waliuwawa. Kwenye ule uchaguzi watu waliuawa. Tumeumizwa watu wote wa nchi hii kwa watu kuuawa alafu kufichwa. Watu wengi wameuawa lakini tunajaribu kuficha ukweli." - Dkt Helen Kijo-Bisimba
Tundu Lissu akiwa bado Ubeljiji mwaka 2022 aliongea na #MariaSpaces kuhusu mgomo wa madereva na akasema wasimsuburi Tundu Lissu aje
Leo Lissu yuko ndani na madereva wenyewe wamejipanga na wamegoma nchi nzima!
Tanzania AMKA!
Tulichokosa na mshikamano sasa tumeshajua TUSHIKAMANE!
Hakuna serikali dhalimu iliyoweza kushinda raia wake ambao wako mamilioni!
@munyamambogo@TBoundBuses msikilizeni Lissu
#TutaelewanaTu
Huyu ndiye Khalifa. Mwenyezi Mungu ambariki huyu kijana amenyooka kama rula. Na hivi ndivyo kazi ya uandishi wa habari unapaswa kuwa kama muhimili wa nne wa dola.
Kuna jinsi ambavyo huyu jamaa amejitoa kwa ajili ya Tanzania na Watanzania….
Na ni kweli matatizo yote ya haki tuliyonayo TZ yanatokana na kundi dogo la watu………. Watu milioni 70 tunabagazwa na kuuawa na kundi halizidi watu 100.