Iran imetangaza kusitisha mashambulizi dhidi ya Israel baada ya nchi hizo mbili kushambuliana kwa mara ya kwanza tangu makubaliano ya kusitisha mapigano yaanze kutekelezwa mwezi Aprili.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuzitaka Iran na Israel kusitisha mashambulizi akisema kuwa nchi hizo zinaelekea kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
#KENYA: WANAFUNZI 7 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA YA KUTEKETEZA BWENI YA SHULE, KENYA
Wanafunzi saba wa Utumishi Girls Academy wamefikishwa katika Mahakama ya Naivasha wakikabiliwa na tuhuma za kuhusika na shambulio la moto lililosababisha vifo vya wanafunzi 16.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi ukionyesha kuwa kamera za CCTV zilirekodi ushiriki wa washukiwa hao katika tukio la moto wa bweni uliotokea wiki iliyopita.
Mahakama imeamuru washukiwa wabaki kizuizini huku uchunguzi ukiendelea, na polisi wakipewa muda zaidi kukamilisha upelelezi.
Nje ya mahakama, familia za waathirika walikusanyika wakisisitiza haki kwa wanafunzi waliopoteza maisha katika mkasa huo wa kutisha.
Huwa nawaambia kuwa mngejua wanavyotuona kama sisimizi! Hata mnayemdhania ni mstaarabu ana maoni haya! CCM mkiwaamini shauri zenu! Not this group of CCM!
Utter contempt from Asha Rose Migiro who was Deputy Secretary General of the UN under Ban Ki Moon!
She defended the police of #Tanzania who massacred innocent citizens in the streets, in homes and bars! And she says they did a sacred job!
Heartless but not suprised!
#CCMmustgo #SamiaMustGo
“Udanganyifu mkubwa na hatari zaidi katika siasa ni kuamini kwamba kesho itaendelea kufanana na jana.”
Tawala nyingi huanguka si kwa sababu zilikuwa dhaifu, bali kwa sababu zililewa na mafanikio ya zamani. Zikaamini kwamba hofu ile ile, propaganda zile zile, mfumo ule ule, watu wale wale, na mbinu zile zile zilizowafanya watawale jana, vitaendelea kuwabeba milele.
Lakini historia haijawahi kuwa mwaminifu kwa watawala wanaokataa kusoma nyakati.
Wananchi hubadilika.
Vizazi hubadilika.
Hasira hubadilika.
Na hata ukimya wa wananchi hubadilika.
Kuna ukimya wa heshima.
Lakini pia kuna ukimya wa kuchoka.
Na viongozi wengi hushindwa kutofautisha hayo mawili.
Tatizo la madaraka ya muda mrefu ni kwamba hujenga udanganyifu wa kutokuguswa. Watu wanaanza kuamini kwamba taasisi ni mali yao, sheria ni silaha yao, na taifa litaendelea kuzunguka majina yao milele.
Lakini historia inaonyesha:
Hakuna dola iliyowahi kushinda vita dhidi ya ukweli kwa milele.
Siku zote tawala huanza kuanguka pale zinapoanza kuamini:
• hakuna mbadala,
• hakuna anayethubutu kusema,
• hakuna atakayewawajibisha,
• na hakuna kitakachobadilika.
Lakini dunia hubadilika ghafla.
Kilichokuwa nguvu jana kinaweza kuwa mzigo kesho.
Waliokuwa wanaogopa jana wanaweza kuwa wa kwanza kusema kesho.
Na waliokuwa wakisifiwa jana wanaweza kuachwa peke yao na mfumo walioujenga wenyewe.
Historia imejaa viongozi waliochelewa kuelewa kwamba wananchi wanaweza kunyamaza kwa muda…
lakini hawaachi kuona.”
#TANZANIA:SAMIA:YA OKTOBA 29 NI FUNZO KWA VYOMBO VYA USALAMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, amesema tabia ya kujiamini kupita kiasi na kufanya mazoea ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama inaweza kuhatarisha usalama wa taifa.
Akizungumza leo Mei 28, 2026 katika hafla ya kufunga mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi wa Polisi iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) Kurasini jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema matukio ya ghasia yaliyojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 yamekuwa funzo muhimu kwa taifa baada ya mifumo ya nchi kuingia katika mtihani mkubwa.
Rais Samia amelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha halidharau taarifa yoyote au kiashiria chochote cha kiusalama kinachoweza kujitokeza, akisisitiza umuhimu wa kuwa makini wakati wote katika kulinda usalama wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha, amesema ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 imeonesha kuwa mtazamo wa muda mrefu wa Watanzania kuamini kuwa nchi ni “kisiwa cha amani” umekuwa ukisababisha baadhi ya viashiria vya hatari kuchukuliwa kwa wepesi.
Kwa mujibu wa Rais Samia, hali hiyo huwapa nafasi wahalifu na maadui wa nchi kupanga na kutekeleza vitendo vya uhalifu bila kugundulika mapema.
#HABARI Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imeiharisha Shauri Na. 12194/2026 la Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mpaka tarehe 2 Juni 2026.
Shauri limetajwa leo tarehe 25 Mei 2026, mbele ya Jaji David Ngunyale, limepangwa kuelendelea juni ambapo Mahakama imeutaka upande wa wajibu maombi kuwasilisha viapo vyao kinzani ndani ya siku saba.
Kwenye shauri hilo wajibu maombi ni Said Issa Mohammed, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Maulida Anna Komu (marehemu) na Ahmed Rashid Khamis wajumbe wa bodi ya wadhamini.
Wengine Katibu Mkuu wa Chadema, na wajumbe wa bodi ya wadhamini.
#EastAfricaTV
Klabu ya Manchester imetangaza kumteua mkufunzi Michael Carrick kuwa kocha mkuu mpya wa kudumu klabuni hapo akichukua nafasi ya Ruben Amorim ambaye alitupiwa virago mnamo Januari 5, 2026 kama kocha wa kudumu.
Carrick 44, raia wa England ambaye alikuwa kocha wa muda tangu kuondoshwa kwa Amorim amepewa mkataba wa miaka miwili na chaguo la ongezeko la mwaka mmoja zaidi baada ya kuiongoza timu hiyo kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ikimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu England.
Kiungo huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur ambaye aliichezea Man United kuanzia mwaka 2006 mpaka alipostaafu mwaka 2018 ataendelea kufanya kazi na benchi lake la ufundi klabuni hapo likiongozwa na kocha msaidizi Steve Holland, Jonathan Woodgate, Jonny Evans na Craig Mawson.
#KitengeSports
MAREKANI YAMUWEKEA VIKWAZO FAUSTINE MAFWELE KWA TUHUMA ZA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU
Marekani imemuwekea vikwazo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Tanzania (SACP), Faustine Jackson Mafwele, kwa madai ya kuhusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliodaiwa kufanyika dhidi ya wanaharakati wa Afrika Mashariki waliokuwa Dar es Salaam.
Katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, serikali ya Marekani imesema Mafwele amewekwa chini ya kifungu cha sheria cha Section 7031(c), hatua inayomzuia kuingia nchini Marekani.
Vikwazo hivyo vinahusishwa na tukio la mwaka 2025 ambapo mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire pamoja na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi walikamatwa walipokuwa Tanzania kufuatilia kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Wawili hao baadaye walidai kushikiliwa, kuteswa na kufanyiwa ukatili wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama.
Mashirika ya haki za binadamu pamoja na wanaharakati wamekuwa wakimtaja Mafwele kuhusishwa moja kwa moja na operesheni hiyo, madai ambayo mamlaka za Tanzania hazijayajibu kwa kina hadi sasa.
Watanzania, dunia haijachoka na wala haijalala, haiwezi kuvumilia unyama na ukiukwaji wa haki za binadamu uliotokea Tanzania. Muda sio mrefu mtasikia kishindo kutoka USA. Hizi ni rasharasha tu. Mambo makubwa yapo kwenye pipeline.
Nipo na begi la maamuzi magumu. Yajayo yanafurashisha
#TanzaniaMassacre #FreeTunduLissu
Rio Ferdinand accused of sports washing after going on Tanzania govt visit hosted by minister - his "good friend" - who has been sanctioned by USA for gross violations of human rights. https://t.co/Ag2Y6BvfzC
Marekani wameanza na Mafwele. Watanzania, this is a step in the right direction kwenye kupata accountability. Wauwaji wooote watakuwa held accountable na wananchi tutaipata nchi yetu kutoka kwa wahuni.
Tukimix nguvu zetu za ndani na support ya nje, HAKI itapatikana kwenye nchi yetu…….
Na niwaambie tu, yanakuja mengi na makubwa, wauwaji watatafuta pa kujichimbia……
TUTASHINDA!!!!!!
Thank you so much @SecRubio@StateDept
The @StateDept is designating Tanzanian Police Force Senior Assistant Commissioner Faustine Jackson Mafwele for involvement in gross violations of human rights.
Jeshi la Polisi lilifika Makao Makuu ya Chama na kumtaka David Djumbe kwa mahojiano.
#Picha Jumbe akishuka kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es salaam.
Badala wampeleke hospitali wao wanataka wakamhoji, ikumbukwe Djumbe anapingu mkononi Baada ya kuwakimbuka watekaji usiku wa leo.
Picha zikionyesha Msaidizi wa TUNDU LISSU akiwa ameumizwa vibaya na watekaji usiku wa kuamkia leo.
David Djumbe alitekwa siku ya Jana Maeneo ya Bunju akiwa na rafiki yake wakati wa kutekwa alipiga kelele sana bodaboda wakafukuzia GARI kwa nyuma
Walipofika umbali wa kilometa kama 3 watekaji walipoona bodaboda bado wanafuatilia GARI, watekaji walishuka na kuanza kupiga RISASI wakati huo Djumbe wakiwa wamemuacha ndani ya GARI.
Ndio David Djumbe akapata upenyo na kukimbia akiwa na Pingu mkononi na amelowa damu kama anavyoonekana.
Mungu ametenda watekaji wanazidi kuuumbuka.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Kihulla amewaambia wabunge kuwa WMA hufanya uhakiki wa mitungi ya gesi ya kupikia inayouzwa nchini ili kujiridhisha kuhusu ujazo wake kabla ya kuingia sokoni.
Akizungumza katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kuhusu majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake iliyofanyika Mei 13, 2026 Bungeni Dodoma, Kihulla alisisitiza kuwa jukumu la WMA ni kuhakiki na kusimamia usahihi wa vipimo katika sekta zote, ikiwemo nishati.
Hata hivyo amewahimiza wananchi wakiwemo wabunge kuchukua tahadhari zaidi wakati wa kununua gesi.
“Kabla ya kununua gesi, hakikisheni mtungi huo unapimwa na muuzaji mbele yenu ili kujiridhisha kuhusu ujazo wake. Epukeni kununua gesi kutoka kwa wauzaji wasio na mizani, kwa sababu hutaweza kujua kama gesi uliyonunua ina ujazo sahihi kama ilivyoandikwa kwenye mtungi”, alisema Kihulla.
Akitoa mwongozo wa jinsi ya kutofautisha uzito ulioandikwa kwenye mtungi, Kihulla ameeleza kuwa kila mtungi wa gesi una maelezo mawili muhimu ya uzito ambayo mwananchi anapaswa kuyafahamu ambayo ni Net Weight na Gross Weight.
“Net Weight ni uzito wa gesi pekee iliyomo ndani ya mtungi. Hii ndiyo kiasi unacholipa. Gross Weight ni uzito wa gesi pamoja na uzito wa mtungi tupu.”
Alisema wakati muuzaji anapima mtungi uliojaa gesi, mnunuzi anapaswa kuangalia kama uzito unaooneshwa kwenye mzani unalingana na jumla ya net weight iliyoandikwa kwenye mtungi pamoja na uzito wa mtungi tupu. Ikiwa mzani unaonesha chini ya jumla hiyo, basi kuna upungufu wa gesi.
Amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni kuwa wananchi wengi bado hununua gesi kwa mazoea bila kujali kama muuzaji ana mzani na amepima mtungi huo au la.
Pia amebainisha kuwa baadhi ya wananchi huagiza vijana wa bodaboda kuwanunulia gesi ili kurahisisha usafirishaji, bila wao wenyewe kuwepo ili kujiridhisha. Hali hiyo inawafanya kukosa uhakika kuhusu ujazo halisi wa gesi wanayonunua.
Katika ufafanuzi wake, Kihulla pia amezungumzia upimaji wa tochi za barabarani zinazotumiwa na askari kupima mwendo wa magari. Amesema WMA huhakiki tochi hizo ili kuhakikisha zinapima kwa usahihi na haki inatendeka kwa wamiliki wa magari.
“Hata hivyo, nawasihi wananchi kuwa endapo mtatilia shaka au kubaini kuna tatizo la usahihi wa vipimo popote pale, msisite kuwasiliana na WMA kwa hatua za haraka,” alisema.
Awali, kupitia wasilisho la video, Kihulla alieleza kuwa WMA inasimamia matumizi sahihi ya vipimo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo, miundombinu, madini, maji, ujenzi, nishati na usafiri.
Aidha, alisema Wakala hiyo inajiandaa kuanza uhakiki wa vipimo katika maeneo mapya ikiwemo sekta ya mawasiliano hususan kuhakiki usahihi wa bando za intaneti na dakika za simu zinazotolewa na makampuni ya mawasiliano ili kuongeza wigo wa ulinzi wa mwananchi.
Amesema, lengo ni kuhakikisha mteja anapata kiasi halisi cha data au dakika alichonunua, bila kupunguzwa au kupotea kabla ya muda wake kuisha.