Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. @HecheJohn leo Septemba 28, 2026, amefunga warsha inayowakutanisha viongozi wa Chama ngazi ya Taifa, Kanda na Mikoa iliyofanyika Makao Makuu ya Chama, Edwin Mtei House, Mikocheni kwa siku mbili, jana na leo.
Leo Septemba 28, 2026, imeendelea warsha inayowakutanisha viongozi wa Chama ngazi ya Taifa, Kanda na Mikoa. Warsha hiyo inaendelea Makao Makuu ya Chama, Edwin Mtei House, Mikocheni. Leo ikiwa ni siku ya mwisho, warsha hiyo itafungwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. @HecheJohn.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. @TunduALissu, akiwasili katika ukumbi wa Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam asubuhi ya leo, ambapo ataendelea na hoja za mwisho za upande wa utetezi (final submissions) katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Leo, Septemba 27, 2026, CHADEMA imefanya warsha iliyowakutanisha viongozi wa Chama ngazi ya Taifa na viongozi wa Kanda. Warsha hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Chama, Edwin Mtei House, Mikocheni, Dar es Salaam.
Matukio katika picha mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni Septemba 25, 2026 Musoma Mjini, Mkoa wa Mara. Mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti bara Mhe. @HecheJohn. Katika mkutano huo Mhe. Heche aliambatana na mwenyeji wake Mhe. Lucas Ngoto, Mwenyekiti Kanda ya Serengeti.
"Kosa la mtoto wake ni lipi? huyu mtoto leo hana baba, amebaki yatima katika umri huu, kosa la baba yake ni kuwa kiongozi wa Chadema, chama ambacho kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.Leo ni mwaka mzima hawatuambii yupo wapi. Huyu mtoto akikua hii nchi mtaiongozaje" Mhe. @HecheJohn
Matukio katika picha mkutano wa hadhara uliofanyika leo asubuhi Septemba 25, 2026 Lamadi, mkoani Simiyu. Mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti bara Mhe. @HecheJohn. Katika mkutano huo Mhe. Heche aliambatana na mwenyeji wake Mhe. Lucas Ngoto, Mwenyekiti Kanda ya Serengeti.