Entertainment & Sports News| Instagram,Facebook & Youtube DizzimOnline| Watch Dizzim TV on Azam Decorder Chn 413 and StarTimes on 110(Antena) & 201(Dishi).
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza kupelekewa taarifa kamili za wasimamizi na mshauri mwelekezi wa ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Nne baada ya kushuhudia uzembe unaosababisha usumbufu zaidi barabarani kinyume na malengo ya mradi huo.
Aidha Mh. Malisa amezitaka taasisi za ulinzi Wilaya ya Mbeya kuwatumia vijana hao wanahitimu mafunzo hayo katika shughuli za ulinzi kwa kuwapatia ajira na kuacha kutumia Askari wasiokuwa na mafunzo katika taasisi
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Beno Malisa ametoa angalizo kwa watu wanaotaka kuvuruga amani iliyopo na kuwataka kuacha mara moja kwani Mbeya ni kitovu cha amani na biashara
Ameyazungumza hayo kwenye mahafali ya kuhitimu kwa mafunzo ya jeshi la akiba(Mgambo)
yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba Jijini Mbeya ambapo ametahadharisha kuwa wanaodhani kuwa Mbeya ni kitovu cha vurugu kujitathimini kwani wakazi wa Mbeya hawatokuwa tayari kupoteza muda kuhatarisha amani iliyopo hivyo Serikali Ipo imara kulinda maslahi ya wana Mbeya.
Katika hotuba yake kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia yaliyofanyika jana jijini Lusaka, Rais Samia alisema eneo ambalo Zambia itapewa liko Kwala, mkoani Pwani.
Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya nchi hiyo.
Rais Hichilema amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari alioufanya na Rais Samia kwenye Ikulu ya Zambia iliyopo jijini Lusaka.
Rais Hichilema alisema Wazambia wamechukua hatua hiyo kama zawadi ya kuonyesha ushirikiano mwema baina ya nchi hizi mbili.
Maeneo muhimu katika makubaliano hayo yanahusu masuala ya ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye biashara na uwekezaji, gesi asilia, ulinzi na usalama, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Marais hao wanakutana kwenye mkutano wa ana kwa ana leo asubuhi na waliwaambia Wafanyabiashara hao kwamba mazungumzo yao yatajikita kwenye kuweka taratibu za kuondoa changamoto hizo.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema wameazimia kuweka mazingira yatakayofanya biashara kati ya Tanzania na Zambia zisiwe na vikwazo.
Wakizungumza katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia lililofanyika jana jioni marais hao walisema eneo moja la muhimu ni kuhakikisha magari hayakai kwenye mipaka kwa muda mrefu pasi na sababu.
Rais aliitumia nafasi hiyo kushawishi serikali na wafanyabiashara wa Zambia kuendelea kuitumia Bandari ya Dar kama kituo chake Kikuu cha usafirishaji na upasuaji wa mizigo yake.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utaifanya iwe na uwezo mkubwa na ufanisi zaidi wa kuhudumia wateja wake kutoka popote duniani.
Rais aliitumia nafasi hiyo kushawishi serikali na wafanyabiashara wa Zambia kuendelea kuitumia Bandari ya Dar kama kituo chake Kikuu cha usafirishaji na upasuaji wa mizigo yake.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utaifanya iwe na uwezo mkubwa na ufanisi zaidi wa kuhudumia wateja wake kutoka popote duniani.
Mkutano huo umehusisha Majaji Wakuu wa Nchi wanachama wa jukwaa hilo ikiwemo Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe,Eswatini, Msumbiji,Seychelles, Botswana,Angola, Zanzibar, Malawi, Lesotho, Mauritius, Zambia na Afrika ya Kusini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) uliofanyika Mkoani Arusha leo October 23,2023.