Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameendelea kusisitiza kuwa nafasi za kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na JKT haziuzwi, amewakumbusha wananchi kuchukua tahadhari
DONDOO;
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akishiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Vicent Mpwaji, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemtembelea na kumjulia hali, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, katika makazi yake Kibele, Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba baada ya hafla ya uapisho wa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya, Geita, Pwani, Mwanza pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar,
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Wakuu wa mikoa ya Mbeya, Geita, Pwani, Mwanza pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2026.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha CP Salum Rashid Hamduni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2026.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2026.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2026.
Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Mhe. Jumanne Abdallah Sagini kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2026.
WAZIRI MAVUNDE AZINDUA PROGRAMU YA KESHO ILIYO NJEMA KATIKA SEKTA YA MADINI (MBT)
▪️Azindua na Zoezi la Urushaji wa Helikopta ya Utafiti wa Madini ya Barrick
▪️Maeneo ya Leseni za Vijana,Wanawake na Wenye Ulemavu Kufanyiwa Utafiti kwa Helikopta
▪️Rais Dkt. Samia Apongezwa kwa Maelekezo na Maono Yake Sekta ya Madini
▪️Baraza la Dhahabu Duniani Lavutiwa na Programu ya MBT
▪️Waziri Mavunde Aagiza Mitambo ya Uchorongaji ya STAMICO Kufika Mara Baada ya Utafiti Kukamilika
📍Nyamongo, Mara.
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amezindua rasmi Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT), maarufu kama “Kesho Iliyo Njema,” na kueleza kuwa programu hiyo ni hatua ya kimkakati ya Serikali katika kufungua milango mipya ya fursa na uwezeshaji kwa vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum kushiriki kikamilifu katika Sekta ya Madini na kwamba programu inalenga kuwasaidia walengwa kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha na kuelekea kwenye uchimbaji wenye tija, unaotumia maarifa, teknolojia na taarifa sahihi za kijiolojia, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa maeneo ya uchimbaji, leseni na fursa za kiuchumi zinazotokana na rasilimali madini.
Waziri Mavunde amebainisha hayo, leo Agosti 31, 2026, katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara, wakati akizungumza katika hafla hiyo iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa utafiti wa kina wa madini unaofanywa na Barrick Gold Corporation,
Mhe. Mavunde ametumia nafasi hiyo kumpogeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maelekezo na maono yake ya kuweka mazingira wezeshi kwa makundi hayo na kuongeza kuwa Rais Dkt. Samia ameagiza asilimia 10 ya mapato yatokanayo na makusanyo ya Sekta ya Madini kutengwa kwa ajili ya utafiti wa kina wa madini, hatua ambayo inalenga kuongeza taarifa za rasilimali madini nchini na kufungua fursa zaidi kwa wananchi.
Waziri Mavunde pia ameishukuru Barrick kwa kukubali kufanya utafiti katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo Nyamongo, akieleza kuwa ndani ya wiki mbili utafiti huo unaweza kufanyika katika eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 6,000 na kusisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhakikisha matokeo ya utafiti yanageuka kuwa fursa halisi kwa wananchi, sambamba na kumuelekeza Kamishna wa Madini, kwa kushirikiana na GST na STAMICO, kukaa na Barrick na kuhakikisha mara utafiti utakapokamilika, mitambo ya uchorongaji inafika Nyamongo kwa ajili ya hatua inayofuata ya utafiti.
Aidha, Waziri Mavunde amesema uzinduzi huo unaashiria mwanzo wa safari ya kujenga “Kesho Iliyo Njema” katika Sekta ya Madini, huku akieleza kuwa Rais wa Baraza la Dhahabu Duniani (World Gold Council) amevutiwa na programu ya MBT na kwamba vijana wa Nyamongo ndio watakaokuwa miongoni mwa vijana wa kwanza kunufaika na mpango huo.
“Tunaenda kupanda mbegu, tunaanza safari; leo mnaianza safari ya kwenda kubadilisha maisha yenu na mimi nitasimamia programu hii ili tufikie lengo,” amesema Mavunde.
Kwa upande mwingine, Waziri Mavunde amesema kuwa amedhamiria kuipima Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa ya Kimadini kwa kuhakikisha maeneo maalum yanatengwa kwa ajili ya makundi ya vijana na wanawake, huku leseni zikitolewa kwa kasi ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uchimbaji, amesema lengo ni kuona programu ya MBT ikienda sambamba na ukusanyaji wa maduhuli na kwamba angependa kuona kila siku fursa mpya za leseni zikitolewa kwa vijana kupitia programu hiyo. Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa vijana wachimbaji kuweka pembeni tofauti zao, kushirikiana na kuepuka kuwagawa vijana, akisisitiza kuwa Serikali haitakubali migogoro ya makundi iwe kikwazo cha utekelezaji wa programu hiyo.
Leo 01 September 2026, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB) amekutana na wakurugeni wa Kampuni ya Mantra Tanzania Limited mjini Dodoma kujadili maendeleo ya mradi wa mto Mkuju unaojihusisha na uchimbaji wa madini ya urani wilayani Namtumbo,Ruvuma.
Akiongoza ujumbe huo Bw. Vladislav Shulga amesema kuwa kampuni ya Mantra Tanzania Limited ipo tayari kuendelea na ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kipekee Tanzania na Afrika mapema iwezekanavyo ndani mapema Oktoba 2026 mwaka huu baada ya kuzinduliwa mtambo mdogo wa uchakataji wa Urani mwaka jana 2025.
Akizungumza katika mkutano huo,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ameitaka Kampuninya Mantra kuhakikisha hatua za uendelezaji mradi zinaendelea kwa kasi kubwa na pia ameuhakikishia uongozi wa Mantra Tanzania kuwa wataendelea kupata msaada wa serikali katika kila hatua ili kuhakikisha mradi huu unasonga mbele na kuanza uzalishaji ifikapo 2029.
Pichani ni Meneja Uendelevu wa kampuni ya Mantra Bw. Majani Moremi Wambura, kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Bw Vladislav Shulga, na Mjumbe wa Bodi hiyo Bw. Aleksandr Ryabchenko
Lusaka, Zambia
Leo nimeshiriki sherehe za uapisho wa Mheshimiwa Hakainde Hichilema kuwa Rais wa Jamhuri ya Zambia.
Kwa mara nyingine, ninampongeza Mheshimiwa Hichilema kwa kuaminiwa tena na wananchi wa Zambia.
Ninawahakikishia ndugu zetu wa Zambia kuwa Tanzania itaendelea kuthamini na kuimarisha uhusiano wetu wa kidugu, wa kihistoria na kimkakati, kwa manufaa ya nchi zetu mbili.
Mhe. Dkt. @SuluhuSamia , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisamiliama na Mhe,Netumbo Rais wa Jamhuri ya Namibia alipodhuria Sherehe za Uapisho wa Mhe. Hakainde Hichilema, Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Jijini Lusaka,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ahudhuria Sherehe za Uapisho wa Mhe. Hakainde Hichilema, Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Jijini Lusaka, tarehe 01 Septemba, 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, leo tarehe 01 Septemba 2026.