Akiwasilisha mitigating factors, Lissu anasema:
"Historia haijawahi kuwa nzuri kwa Majaji wanaofunga watu wasio na hatia ili wamridhishe mteule. Hilo kosa la uchochezi mmelitafuta wenyewe Majaji kumsaidia mteule wenu."
What a Man!
6.11.2026: Hukumu ya TUNDU LISSU NA KUMBUKUMBU YA KESI YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1958. HISTORIA INATUFUNDISHA NINI?
Leo, tarehe 6 Novemba 2026, Tundu Lissu ameshinda kesi ya uhaini lakini mahakama ikasema amepatikana na hatia ya uchochezi (incitement) na kuhukumiwa kifungo cha miaka 4. Tunamshukuru Mungu kwa kesi ya uhaini kutupiliwa mbali na kumpongeza Lissu kwa umahiri na ujasiri wake hadi kujitetea. Lakini hukumu ya uchochezi inasikitisha, inafikirisha na inatukumbusha historia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye naye mwaka 1958 alikutwa na hatia ya jinai ya kashfa (criminal libel) wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Makosa haya mawili ni tofauti kisheria, lakini kesi hizi zinafanana katika jambo muhimu: zote zilihusu kiongozi mkuu wa upinzani aliyeshtakiwa na Serikali kutokana na kauli zake za kisiasa.
Turejee historia.
Tarehe 27 Mei 1958, Mwalimu Nyerere alichapisha makala katika gazeti la Sauti ya TANU, Toleo Na. 29, akiwakosoa Wakuu wawili wa Wilaya wa Serikali ya kikoloni kwa madai ya kutumia madaraka yao vibaya na kuihujumu TANU.
Akafunguliwa kesi ya jinai Na. 2207/1958 chini ya kifungu cha 187 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Serikali ya Uingereza ilitoa maelezo kuhusu mashtaka hayo katika Bunge lake (House of Commons) tarehe 26 Juni 1958.
Nyaraka za UN zinathibitisha kwamba Mwalimu alikutwa na hatia katika mashtaka mawili na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 3,000 za Afrika Mashariki, sawa na pauni 150 za wakati huo, au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini tarehe 12 Agosti 1958 na hakukata rufaa.
Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa. Wanaharakati wa kupigania uhuru huko London walihoji iwapo Mwalimu angepata haki katika mahakama za kikoloni na kudai kuwepo kwa waangalizi huru. Serikali ilikataa, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kufungua mashtaka ulikuwa chini ya mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Miaka 68 baadaye, tunajikuta tena tukitafakari maswali kuhusu uhuru wa kisiasa, matumizi ya sheria za jinai na nafasi ya mahakama katika mfumo wa kidemokrasia.
Pamoja na hukumu ya mwaka 1958, Mwalimu Nyerere aliendelea na harakati zake hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961.
Funzo muhimu ni kwamba hukumu ya jinai dhidi ya kiongozi wa kisiasa si lazima iwe mwisho wa safari yake ya kisiasa. Historia inaonesha umuhimu wa kuendeleza majadiliano (dialogue) badala ya mapambano na vurugu (confrontation).
Kwa wanaothamini demokrasia, mfumo wa vyama vingi, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria, hukumu ya uchochezi dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani inaibua maswali mazito yanayohitaji mjadala mpana wa kitaifa.
Je, mipaka kati ya ukosoaji halali wa Serikali na uchochezi wa jinai ikoje?
Je, mwanasiasa awe mpinzani au wa chama tawala atakosoa je Serikali au kudai maboresho au mageuzi bila kuhofia kutafsiriwa kuwa mchochezi?
Je, wananchi watawezaje kudai haki zao kwa nguvu ya hoja bila kuonekana wanachochea uvunjifu wa amani?
Walimu na wanataaluma tutawezaje kufundisha, kuchambua sera, kutoa mapendekezo na kukosoa mifumo ya utawala bila kuhofu kuitwa wachochezi?
Viongozi wetu wa dini watawezaje kutekeleza wajibu wao wa kinabii wa kukemea maovu na kusimamia haki bila kuonekana wanachochea waumini wao?
Uhuru wa kujieleza una mipaka yake na hauhalalishi haki ya kukashfu, kuchochea vurugu au uhalifu. Lakini ni muhimu sana kuweka mipaka iliyo wazi kati ya uchochezi wa jinai na ukosoaji halali wa kisiasa.
Iwapo sheria za jinai zitatumika kudhibiti ukosoaji halali wa kisiasa au kitaalamu, tunaweza kujikuta tunadhoofisha demokrasia, haki za binadamu, kuongeza hofu na kuzidisha mkwamo wa kisiasa na kiuchumi badala ya kuutatua.
Hukumu ya leo inatupa sababu nyingine ya kujadili kwa kina uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, haki za raia na za vyama vya upinzani na mipaka ya matumizi ya sheria za jinai katika siasa.
Ninarejea msisitizo wangu wa muda mrefu kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4Rs. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kukosoana kwa hoja
TUJISAHIHISHE
Walikusanya data kwa akili na maarifa makubwa. Tangazo lilikuwa, Leteni majina ya walioumizwa na waliouwawa wa imani yetu na wasio na imani yetu ili tuweze kuwaombea.
Mkti Tundu Lissu anasema ,
Msikubali kupita njia isiyo na haki. Mimi niko imara na sina shida hapa nilipo! Mimi nikifia humu jela, lakini nyinyi mkakaza, jueni mtawasaidia wananchi. Nikifungwa, mkakaza katika haki bado mtawasaidia wananchi. Na nikiachiwa, tukakaza wote kwa pamoja, vilevile tutawasaidia wananchi. Lolote kati ya hayo matatu lina faida kwetu kama tusipozimia mioyo. Kuweni IMARA. 😭😭😭😭
Kama wanasiasa wa ccm ndio wanaagiza makanisa kufunguliwa, watu watafutwe na kumatwa au wasitafutwe, watu wabambikiziwe kesi mbaya au waaachiwe huru.
Nani anaweza kusema tuna vyombo vya dola vyenye ueledi na vinavyofanya kazi kwa uhuru na bila upendeleo.
Huyu anaeagiza hivi akiagiza Heche akamatwe na kupotezwa nani atamkatalia.
Hapa tulipo unaweza kukosana nae kwa mambo binafsi akaagiza upewe Ugaidi au uhaini.
Shame on you.
CNN waliripoti taarifa ya MUUGUZI ambae hakutaka kutajwa jina kutoka Arusha akisema “Polisi walienda hospitali na kuchukua wagonjwa wote waliokuwa wakipatiwa matibabu ya majeraha ya RISASI na kuenda kuwapeleka Mochwari wakafie huko”.
Leo Father Kitima anaongea na vyombo vya habari anasema “POLISI walienda Hospitali ya kanisa na kutaka watu wote waliopigwa RISASI wasipatiwe huduma kabisa wafe—Manesi wa hospitali ya KANISA waligoma na kumpigia Ruwa'ichi, Askofu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam ambaye aligoma na kusema watibiwe kwanza na kama wanawataka watawachukua wakiwa wazima.”
GIRISHONI alikosoa Ripoti ya CNN kwa kusema hawana Weredi.
Badala ya kuagiza uchunguzwe wewe na vyombo vyako vya dola, polisi na watu waliokua na silaha wanaua Watanzania .. unaagiza wachunguzwe wapinzani wako, unaagiza chama chetu kuchunguzwa..
Hatuwezi kuuziwa uoga.
Mtu anayeonekana katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii jioni ya leo akionekana kubishana na watu wasiojulikana na wamebeba silaha za moto hajafahamika ni nani lakini siyo Joseph Mbilinyi (JONGWE). SUGU yupo salama. Anawakaribisha Desderia Hotel, Mbeya.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 149
Waheshimiwa Majaji, naomba niende kwenye hoja ya tano;
Naomba kurejea kesi zifuatazo High hope international group Jiangsu native produce import and export cooporation limited vs JOC Textile (Tanzania Company Limited) Misc. Commercial Application No 48 of 2020, kesi ya Sheer Illusions Ltd vs Christina Ulawe Umiro Civil Appeal 114 of 2014.
Hizi kanuni zimechapishwa Julai 11, 2025 miezi mitatu kabla ya kesi hii. Swali ni je, kanuni hizi zinaweza kutumika katika kesi iliyoanza kabla hazijatungwa? Jibu ni Sheer Illusions kwenye ukurasa wa 11 wa hukumu hiyo kuwa haziwezi kutumika kwenye kesi yangu.
Waheshimiwa Majaji hoja yangu nyingine ni kwamba kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa Jinai ambacho ndio msingi wa Kanuni hizi.
Kifungu hiki kililetwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 07 ya 2018. Hii sheria inayoruhusu kuficha mashahidi haijawahi kuchapishwa kwenye gazeti la serikali.
Kifungu cha 14 cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria kinasema ili sheria ianze kutumika lazima iwe published kwenye gazeti.
Sheria yenyewe haisemi itaanza kutumika tarehe ngapi hivyo ilipaswa kuanza kutumika siku ilipotangazwa kwenye gazeti la serikali hadi muda huu niliposimama hapa sheria hii haijawahi kutangazwa kwenye gazeti la serikali.
Waheshimiwa majaji sheria ikitangazwa katika gazette la Serikali inachapishwa kwenye website ya Serikali, official website ya ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Rais Idara ya Utumishi, huku vilevile haipo.
Ndugu zangu Watanzania huyu Lissu nawahakikishia sio binadamu wa kawaida. Haya mapingamizi pia naona kuna dalili yanaweza kuifyatua hii kesi vibaya sana. Hawa watu wafute hii kesi tutaona mengi sana wakiendelea kuiacha.
Haya anaendelea Mhe. Lissu tena.
Waheshimiwa Majaji publication in the Government Gazette ni takwa la Sheria kuwa gazette lazima liwasilishwe Bungeni, halikuwa tabled Bungeni.
Sheria ikitangazwa katika Gazette la Serikali utakuta physical copies katika maktaba ya Mahakama kuu Dar es Salaam kwenye jengo hili, napo haipo.
Vilevile kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali vilevile haipo na huko.
Mahakama Kuu kitengo cha Biashara pia haipo kwenye Hansard za Bunge pia haipo, kwenye duka la Serikali Dodoma na Dar es Salaam pia haipo kwenye Sheria ya Huduma za Maktaba inasema Sheria ikiwa gazetted and published lazima kuwekwa Maktaba Kuu ya Taifa Dar es Salaam hapo Kisutu pia haipo, kuna Sheria nyingine inaitwa Publications (Compulsory Deposit) Act Cap. 294 ambayo inalazimishwa publication must be deposited central library Dar es Salaam.
Kwenye hiyo sheria kuna Publications (Compulsory Deposit) Order GN 61 of 1964 inayosema all publications must be deposited in the central library, haipo waheshimiwa majaji.
Waheshimiwa majaji nimezungumzia tabling bungeni naomba niwaelekeze kwenye kanuni ya 37(2) Kanuni za Kudumu za Bunge GN 56 of 15/01/2016. Kanuni ya 53(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge GN No. 626 of 2020 hivyo kuchapisha sheria kwenye gazette la serikali ni matakwa ya sheria na kusambaza kwenye hizo sehemu nilizozitaja ni takwa la kisheria, haijafanyika sasa katika kanuni hizi.
Uthibitisho wa kuwa sheria imechapishwa ni sheria yenyewe, mimi na Mawakili wangu wanaonisaidia wamelitafuta hilo gazeti nchi nzima halipo. Vijana wamezunguka kila kona ya nchi hii na kwenye hayo maofisi niliyosema hawajawahi kukutana na hiyo sheria. Haipo.
Namsikiliza Mhe. Lissu halafu natafakari huyu mtu huwa anasoma haya mambo yote saa ngapi na anakumbukaje hivi?
Akili kama hii kuwepo jela badala itoe mchango wa kulisaidia hili taifa ni matumizi mabovu ya rasilimali watu wenye akili. Ipo siku tutashinda na kweli itashinda.
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja hapa ninayojaribu kusema ni kwamba kama hiyo sheria haijawa published kwenye gazeti and there is no proof anywhere na kama imetumika, imetumika kimakosa.
Part 150 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Sisi @TanganyikaLaw na @humanrightstz Tumejipanga kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa hizi kesi za kubumba atakosa uwakilishi Tanzania nzima.
Ukitaka kuona tuna taifa la namna gani? Wale wauaji hakuna hata mmoja aliyekamatwa wala kuhojiwa! “Impunity”
Hizi mambo zina mwisho tu!
Sasa ni Rasmi Desemba 09, Gen-Z tutaandamana kushinikiza serikali iwaachie vijana wote iliowashikilia kwa tuhuma za uhaini pamoja na viongozi wa kisiasa wote iliowateka na kuwafungulia mashtaka ya kipambavu ili kutawala watz kwa mkono wa chuma.
Baada ya kupata internet, nimeingia katika mitandao ya kijamii, nimeshuhudia vitu sikuwahi kufikiria vinaweza kutokea katika ardhi yangu. Milima ya maiti za vijana wadogo sana kama nyakati za Liberia ya Charles Taylor au Yugoslavia ya Slobodan Milošević. OMG! Hii ni mambo gani?
TATIZO MNACHANGANYA VIONGOZI WA DINI NA WATUMISHI WA MUNGU
Katika historia ya mwanadamu na hata katika maandiko matakatifu, yapo tofauti kubwa kati ya viongozi wa dini na watumishi wa kweli wa Mungu.
Tatizo kubwa linalojitokeza katika jamii zetu ni kwamba watu wengi huchanganya hawa wawili kana kwamba ni kitu kimoja. Hii ni hatari, maana si kila anayevaa vazi la kidini au kusimama madhabahuni ni mjumbe wa Mungu.
1. Viongozi wa Dini ni wa mfumo – Watumishi wa Mungu ni wa kweli ya kiroho
Viongozi wa dini mara nyingi wamejikita kwenye kulinda taasisi zao, mamlaka yao, na maslahi yao. Wanaweza hata kutumika kama vinyago vya nguvu za kisiasa au kiuchumi. Katika Biblia, Yesu aliwakemea vikali Mafarisayo, Masadukayo na walimu wa sheria kwa unafiki na kupindisha sheria kwa manufaa yao binafsi:
"Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafunga Ufalme wa Mbinguni mbele ya watu; ninyi wenyewe hamwingii, wala hamkubali wale wanaotaka kuingia waingie." – Mathayo 23:13
2. Watumishi wa Mungu wamesimama na Haki, hata ikiumiza
Watumishi wa Mungu, kama manabii wa zamani – Eliya, Isaya, Yeremia, na Yohana Mbatizaji – waliikemea jamii kwa uovu wake bila kuogopa. Hawakubembeleza mamlaka wala kukubali kununuliwa. Walikuwa tayari hata kufungwa, kuteswa au kuuawa kwa ajili ya kusimamia ukweli wa Mungu. Watumishi wa namna hii ni nadra sana leo.
3. Viongozi wa Dini hutafuta makundi – Watumishi wa Mungu hutafuta nafsi za watu
Viongozi wa dini hujenga maelfu ya wafuasi lakini mioyo ya watu hubaki tupu. Wanahubiri kwa faida, wakigeuza watu kuwa chanzo cha kipato. Lakini watumishi wa Mungu hujenga watu, si majengo wala majina. Huduma yao huzaa toba, haki, na ukombozi wa kweli.
4. Hadithi za Mafarisayo na Masadukayo ni onyo la historia
Yesu Kristo hakuwahi kuwa karibu na viongozi wa dini wa wakati wake. Aliwakemea kwa unafiki wao, kwa kutumia dini kama silaha ya kuwatesa wengine. Hili ni onyo kubwa kwa vizazi vya sasa – kwamba dini isipotenganishwa na mamlaka ya kiroho, inaweza kuwa chombo cha uonevu na utumwa mpya wa kiakili na kiroho.
Ni muhimu kwa jamii kutambua kuwa si kila kiongozi wa dini ni mtumishi wa Mungu. Na si kila anayesema "Bwana, Bwana" ataingia katika Ufalme wa Mungu (Mathayo 7:21). Tuwaangalie kwa matendo yao, si maneno yao. Na tuwaogope wale wanaoitumia dini kama kinga ya uovu wao.
unapokwenda kwenye Nyumba za Ibada hakikisha akili yako ni Timamu.
BAK Mwabukusi.