Mothers do not fear death.📌
What they fear most is leaving their children behind, knowing that no one will ever love them as they do..
Happy Mother's day, My lovely Mom
Kwaheri Dkt. Ayub Rioba Chacha. Umetuachia TBC dhoofu.
Sio kazi ndogo kuitumia miaka (10) kugeuza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa idara ya uenezi ya tawi la CCM. Shirika ambalo Watanzania wengi sasa hawajisikii fahari kamwe kufuatilia shughuli zake.
Wakati dunia ikikimbizana na teknolojia ya 4K na uandishi wa kiuchunguzi, TBC chini yako ilikuwa 'bize' kuboresha teknolojia ya kusafisha makosa ya serikali kwa kutumia sabuni yenye manukato ya propaganda.
Siku ya uzinduzi wa Meli ya M.V Mwanza, Mtangazaji wa TBC alisema meli hiyo itafanya safari zake katika nchi mbalimbali itakwenda Kenya, Uganda, Burundi, DR Congo, Zambia, Malawi na Sudan Kusini,
Uongozi wa TBC ukajitokeza kutoa ufafanuzi kwamba mtangazaji alichokusudia kukisema ni MV Mwanza itasafırisha mizigo ambayo baadaye itapakiwa katika vyombo vingine vya usafıri kuzifıkia nchi zilizotajwa.
Pamoja na malezo na ufafanuzi huo kutoka kwa uongozi wa TBC, bado mtamgazaji alichukuliwa hatua za kinidhamu baada ya maneno yake. Hapo ndiyo nilihitimisha mtazamo wangu, Mmechanganyikiwa.
Utetezi wako kuhusu TBC kuonesha matangazo ya mpira (AFCON na WORLD CUP) yasiyokuwa na ubora wa picha kwamba ni fitina tu, ulituonesha sasa umefika kikomo cha kuendelea kuwa Mkurugenzi wa TBC.
Shukrani kwa kuhakikisha TBC haifanyi kazi yake ya msingi kama chombo cha habari cha umma. Ilikuwa kazi ngumu kuhakikisha Watanzania hawapati habari za kweli. Lakini wewe uliishinda changamoto hiyo.
Wakati mashirika ya habari ya serikali kama Al Jazeera (Qatar), NHK (Japan), BBC (UK), DW (German), France 24 (France), ABC (Australia) yanajaribu kujitenga na siasa, TBC ilichagua njia tofauti. Njia ya propaganda.
British Broadcasting Corporation (BBC) haina hofu ya kuikosoa serikali ya Uingereza. Kipindi chao cha Panorama au mahojiano ya asubuhi ya Radio 4 huwabana mawaziri mpaka wanashindwa kujibu.
Waandishi wa BBC hawasubiri tamko la serikali ili kutoa habari; wao ndio wanatafuta habari. BBC inajiona inawajibika kwa walipa kodi, wakati TBC chini yako inajiona inawajibika kwa mteuzi wako na watawala.
Mashirika ya Kimataifa yanalazimika kuwa bora ili visipoteze wasikilizaji. TBC chini yako imejiona haina kitu cha kupoteza kwa sababu ina uhakika wa ruzuku kutoka Serikalini bila kujali ubora wa maudhui.
Wakati mashirika ya utangazaji ya umma huko duniani yanajitahidi kusimamia uhuru wa habari, TBC chini yako iliamua kuwa jukwaa halali la propaganda za Serikali. Nafikiri Ulichagua propaganda kwa kuwa zinalipa..
Umeondoka ukiacha nyuma kivuli cha taasisi kuliko taasisi yenyewe. TBC iliugua kwa muda mrefu, na wewe kama mkurugenzi (Daktari), uliandika dawa ile ile kila siku—dawa iliyozidisha ugonjwa badala ya kuponya.
Chini ya uongozi wake, TBC ilifanikiwa kwa njia ambazo hakuna mkurugenzi mwingine angeweza: TBC sasa ni runinga ambayo Watanzania hawaitazami. Mafanikio makubwa. Kufikia zero audience si kazi ndogo!
Chini ya uongozi wako, TBC ilifanikiwa kuacha kuwa chombo cha habari na kuwa mdomo wa mapambio. Habari ikianza, unajua tu ni nani amepiga chafya ‘White House’ na nani amekata utepe wa choo cha shule.
Umeifanya TBC kukaa mbali na kero za wananchi kama vile muuguzi anavyokimbia mgonjwa wa kipindupindu. Wananchi wanalia kukosa ajira, TBC inakuonyesha kipindi cha maendeleo ya viwanda vya kufikirika
Ni ufundi wa hali ya juu kuiacha TBC mahututi kiasi kwamba hata kulinganishwa na redio mbao ni matusi kwa redio mbao hizo. Leo hii, TBC inazidiwa viewership na 'online garbage media' zenye kamera moja tu.
Umeifanya TBC kuwa chombo ambacho watu wanatazama pale wanapotaka kujua kama kuna “teuzi” au kuna “salamu za rambirambi” au labda wanataka kufuatilia gwaride la maadhimisho ya UHURU.
Gari la umma linapaswa kubeba kila mtu: mawazo mbadala, upinzani, na asasi za kiraia. TBC chini yako ilichagua kubeba “watawala pekee,” huku ikiwaacha wananchi barabarani na kero zao, watajijua huko.
Tulitegemea ushauri kwamba, Mkurugenzi wa TBC ateuliwe na bodi huru baada ya ushindani wa kitaaluma. TBC, uteuzi ni wa kisiasa, hivyo “dereva” lazima amsikilize aliyempa gari badala ya abiria (wananchi).
Kuwe na Bodi Huru ya Utangazaji. Wakurugenzi wasiteuliwe na mwanasiasa, bali wafanyiwe usaili na bodi ya kitaaluma. Hii itawapa ujasiri wa kuruhusu habari zenye kukosoa bila hofu ya kutumbuliwa.
Hutakiwi hata kuwasuta hao ambao wanakuona/wanakuita ‘chawa’. Mazingira ya utendaji shughuli zake TBC ukiwa Mkurugenzi Mtendaji zinasadifu hicho ambacho wakosoaji wako wanakiona kama ‘uchawa’
Tulitegemea TBC ikiwa chini yako, kwa muktadha tuliokufahamu nao ukiwa mhadhiri UDSM, lazima iache kufanya kazi kama State Broadcaster (ya utawala) na ianze kuwa Public Broadcaster (ya wananchi).
Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) ilipaswa kuwa Public Broadcaster (inayotumikia maslahi ya umma), lakini sasa inafanya kazi kama State Broadcaster (inayotumikia maslahi ya utawala uliopo).
Kama TBC ingekuwa gari, umeiacha kama gofu—haina injini wala matairi, lakini inapiga honi za kelele. Ni kitu kilichosimama tu kinachojidai kuwa chombo cha maendeleo. Ni kushindwa kimuundo na kitaalamu.
Martin Maranja Masese (MMM) / Mtikila.
Kipato kinapo ishia kwenye chakula na malazi, kiuhalisia kazi unayo Fanya inakuwa si fursa ya maendeleo, bali ni juhudi za kubaki hai, ambayo ni fursa na maendeleo Kwa muajiri wako. Hari hii ilikuwa na jina lake Karne ya 16, iliitwa Utumwa".
#MwalulesaSenior