Apply to be part of the National Youth Policy Review Multi - stakeholders Dialogue to be held on 24th August 2018. Deadline for application is 5th August 2018. To apply click >>>>click:https://t.co/ylqsffOmxv <<<< #Usipitwe Cc: @UNATanzania@FCSTZ
Mgeni rasmi Bi. Hellen Kijo Bisimba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa @humanrightstz ameshazindua rasmi ripoti ya kitaalamu juu ya mkwamo wa mchakato wa #KatibaMpya, na wadau mbalimbali wanapata nafasi ya kuchangia mjadala unaoendelea hivi sasa hapa Kisenga, Millennium Tower
Tumeungana wadau mbalimbali hapa Kisenga, Millennium Tower katika kushuhudia uzinduzi wa ripoti ya @humanrightstz juu mkwamo wa mchakato wa #KatibaMpya
'Over expectation' ni sumu mbaya sana ambayo inawaua vijana wengi Ulimwenguni hasa barani Afrika. Vijana wengi wamekuwa wakiishia njiani katika vitu wanavyobunia ama kuanzisha kwa kuwa wanatazamia kupata kikubwa kwa muda mchache.
Safari ya mafanikio ni ndefu #MaishaNaKazi2018
"Wanawake mmezaliwa na uwezo sawa na wanaume, mkiwa na uwezo wa kutimiza mambo makubwa lakini jamii na baadhi ya watu wamewafanya muamini kuwa hamuwezi. Kataeni dhana hiyo kuwa kuwa mna UWEZO" ~ Mwl. Julius Kambarage Nyerere #MCM#MwanamkeNaUongozi
Hizi mila na desturi kwa sasa zimekuwa zikipigwa vita (baadhi) lakini si kwa maana mbaya....maana kuna zingine kama ile ya kumruhusu mtoto wa kike kuolewa ama kuoa chini ya miaka 18 ambayo inakinzana na Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ~ Consolatha Chikoti, Mwanasheria #MwanamkeTalk
Katika hatua ya mwaka 0 - 18 mtoto wa kike anakuwa chini ya uangalizi ama usimamizi wa familia yaani baba na mama. Lakini jamii inahusika zaidi, tunaposema jamii ni pamoja na familia husika ~ Consolatha Chikoti, Mwanasheria #MwanamkeTalk
Elimu ya ujinsia imepewa nafasi ndogo katika kumuandaa mtoto wa kike. Lakini elimu hii ni muhimu zaidi kwa mabinti ili kuwasaidia kujitambua yeye ni nani, na mabadiliko ambayo atakutana nayo (Kimwili, Kiakili na Kijamii) ~ Consolatha Chikoti, Mwanasheria #MwanamkeTalk
Kiongozi lazima awe na 'confidence' ambayo lazima ianzie kwenye ngazi ya familia pindi mtoto anakuwa kwenye malezi. Kama familia itashindwa kumjengea uwezo hata akitoka nje hawezi kujiamini na kufanya mabadiliko kama kiongozi katika jamii/familia yake ~ Consolatha #MwanamkeTalk
Jamii inahusika kwa kiasi kikubwa katika kumuharibu ama kumuandaa mtoto wa kike kuwa kiongozi mzuri katika jamii ama familia yake ~ Consolatha Chikoti, Mwanasheria #MwanamkeTalk
Kuna baadhi ya mila ambazo mtoto wa kike kuwa kiongozi ni changamoto. Mfano: Kabila la wazaramo na wamakonde mtoto wa kike anaandaliwa kuwa kiongozi bora wa kijamii sio kiuchumi wala kisiasa ~ Lega, Airwing Sekondari #MwanamkeTalk
Sheria ya namba 21 ya mwaka 2009 imeelezea maana ya mtoto ambaye mtu mwenye umri chini ya miaka 18. Sheria imeweka haki na wajibu ili kuhakikisha mtoto huyu anapewa nafasi ya kushiriki katika maamuzi yanayoathiri maisha yake ~ Consolatha Chikoti, Mwanasheria #MwanamkeTalk
Je, elimu ya ujinsia kwa mtoto wa kike anaipata kutoka katika familia yake? Wazazi wanatakiwa nafasi gani? ~ Mwl Makarani, Turiani Sekondari #MwanamkeTalk
Nafikiri kuna haja ya wanawake wenyewe kwa wenyewe kuanza kuweka mitazamo chanya kwao. Maana kama ninyi mtashushiana heshima....kwa wanaume Itakuwa Mara 3 zaidi #MwanamkeTalk@MwanamkeUongozi@MabalaMakengeza @miss_mshangama https://t.co/7VtGXDToRd
Kama hali ipo hivyo ni wazi kuwa hakuna ushiriki wa kutosha kwa wasichana katika nafasi za uwakilishi ndani ya Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu #MwanamkeTalk@MwanamkeUongozi @miss_mshangama @RebecaGyumi https://t.co/gE56RzDPSF