To fact checkers in TZ
This is not a time for fact checkers to stay aside and allow misinformation & disinformation to circulate on digital platforms.
This is the better time for fact checkers to open up and fight falsehood by elevating truth on digital platforms.
#EICAD2025
#LikizoSummitProgram
Katika zama hizi ambazo mashine (AI) hutumika kuzalisha, kuchakata na kusambaza taarifa.
Kama hatutakuwa makini kuna uwezekano mkubwa watoto wetu wakarithi taarifa potofu.
Hivyo kama wazazi tunao wajibu wa kuwarithisha watoto wetu taarifa zilizo hakikiwa.
Nuzulack aliyasema hayo wakati wa mafunzo ya pamoja ya wadau wa uthibitishaji taarifa August 2025
Katika mafunzo hayo wadau walitambua nyezo muhimu za kidigital ili kupambana na taarifa potofu wakati wowote.
#BeInformed#BeCritical#BeAware#HakikiTaarifa#EICAD2025
Taarifa za uongo na uzushi zime tapakaa sana katika chaguzi hizi zinazoendelea.
Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa wananchi wasiofanya uhakiki wa taarifa,
Kuchagua viongozi wanaotumia taarifa za uongo ili kupata kura na kuacha kuwapima wagombea kwa sera na uwezo wao. #EICAD
Watu upewa pesa ili kuzalisha na kusambaza taarifa potofu kwa lengo la kubadili mtizamo wa kile ambacho jamii inakiamini.
Kuelekea uchaguzi #chadema wajumbe zuieni kutokea kwa hayo kwa kufanya uhakiki wa kila taarifa kwa sasa. #EICAD#BeInformed#BeCritical#BeAware
Kuelekea uchaguzi wa ndani wa #chadema wajumbe wa mkutano mkuu ni vyema kufanya uhakiki wa kila taarifa.
Kwa maana taarifa potofu na matamshi ya chuki yana haribu maamuzi sahihi yenye manufaa kwa wengi,
Na kuleta majeraha ambayo ni ngumu kupona hata baada ya uchaguzi.
#EICAD
Jamii haiwezi kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwa na taarifa sahihi
Wanafunzi wa kituo cha Mbuji School wamepata mafunzo ya namna ya kutafuta taarifa sahihi ndani ya vyanzo vya habari
Taarifa sahihi zitawasaidia kuepuka taarifa potofu ili kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao
Taarifa potofu zina nguvu ya kubadili mitazamo ya wanafunzi kujikita katika masomo.
Hiyo #EICAD kupitia programu ya #LSP2024 imeendelea kutoa elimu ya namna ya kutambua taarifa potofu kwa wanafunzi wa kituo cha tution cha Mbuji School.
Team ya #EICAD ipo tayari kutoa elimu ya kutambua taarifa potofu kwa wanafunzi waliopo katika tuition centers kupitia LIKIZO SUMMIT PROGRAM. #LSP2024
Kaa tayari kupokea ujuzi wa kupambana na taarifa potofu ndani na nje ya mitandao.
ya kuendelea kupambana na upotoshaji wa taarifa nchini. #IDEATHON
Katika wasilisho letu sisi kama #EICAD tulizungumza namna bora ya kujenga KIZAZI THABITI kitakacho pambana na taarifa potofu ndani na nje ya mitandao kuanzia ngazi ya watoto waliopo mashuleni.
KATAA UPOTOSHAJI
Katika kuendelea kupambana na wimbi la taarifa potofu nchini, tunawashukuru sana taasisi ya #nuktafakti kwa kuandaa mkutano wa kutasimini mwenendo wa mapambano ya taarifa potofu nchini Tanzania.
Katika tukio hilo idea mbalimbali ziliwasilishwa kama sehemu ya kuibua mawazo mapya.
Katika mchakato wa uchaguzi unaoendelea nchini hivi sasa.
Ni vyema kuwa makini na kila shauri,taarifa,maoni,habari au machapisho ya wadau ndani na nje ya mitandao.
Hivyo, ni muhimu sisi sote kutafuta taarifa sahihi ili kulinda misingi ya demokrasia.
#Uchaguzi2425#becritical
Mapambano dhidi ya taarifa potofu kati ya jamii ni ushiriki wa wadau wote.
Shukrani #JamiiForums kwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kufanya uhakiki wa taarifa katika kipindi hiki cha uchaguzi wao wakiwa nyenzo muhimu katika ecosystem ya habari. #VERIFY#VERIFY ๐ค
Usambazaji wa taarifa za uongo ni katazo ndani ya #BIBLIA takatifu inaposema,
"Usivumishe habari za uongo;
usitie mkono wako pamoja na mwovu; kuwa shahidi wa udhalimu"
ili kuzuia janga la uvumaji wa taarifa za uongo ni vyema kufanya uhakiki wa kila taarifa.
#VERIFY
Uhakiki wa taarifa ni amri ndani ya kitabu kitukufu cha #QURAN inaposema,
"Akiwajia ninyi mtu mwovu na taarifa yeyote ithibitisheni kwanza,msije mkawadhuru watu kwa ujinga arafu mkawa ni wenye kujuta"
Hivyo usambazaji taarifa pasipo kuhakiki ni hatari kwetu sote,#VERIFY
Kitendo cha jamii kuamini au kuwa 'conditioned' kwamba kila taarifa kutoka redioni,tv na magazetini ndio kweli pasipo wao wenyewe kuhakiki, kinasambaza taarifa potofu nyingi sana kati ya jamii.
Ni vyema KUHAKIKI usahihi wa taarifa hiyo kabla ya kushare na wengine. #PleaseVERIFY
#Disinformation#misinformation and #propaganda is not about just creating fake news, it is also about hiding real news.
Whenever there is big story in the media look for the story they are trying to distract you from.
#EICAD
VERIFY BEFORE YOU AMPLIFY YOUR STORIES.
Taarifa potofu ina asili ya kubeba chuki dhidi ya kundi linaloitwa wengine ndani ya jamii fulani.
Kitendo cha kuongeza maneno binafsi katika habari iliyokwisha haririwa inawez kuleta upotoshaji wa taarifa kati ya wadau wa michezo.
Hivyo, HAKIKI TAARIFA OKOA SOKA LETU.
HAKIKI TAARIFA, OKOA SOKA LETU.
Taarifa potofu ni nyingi sana katika kuelekea msimu mpya wa mashindano ni muhimu sana kutumia credible source ili kupata taarifa sahihi.
Ndio maana #EICAD tunasema si vyema kusambaza taarifa pasipo kuhakiki.
Katika program ya #LSP2024 wanafunzi walifahamu kuhusu teknolojia ya Artficial Intelligence (#AI technology) yaani akili bandia.
Pamoja na faida za teknolojia ya #AI Pia teknolojia hiyo inatumika kuzalisha taarifa potofu na kusababisha mstuko na taharuki kati ya jamii.
Matumizi ya teknolojia ya #AI hapa nchini bado si makubwa sana, hofu iliyopo ni kwamba wasije wakatokea watu waka- employ hiyo teknolojia kutoka nchi nyingine na kuanza kuitumia hapa nchini ili kuchochea kasi ya upotoshaji wa taarifa hasa katika kipindi cha uchaguzi.