Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa KIA kwaajili ya kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu hayati. Cleopa David Msuya yatakayofanyika tarehe 13 Mei 2025 Wilayani Mwanga
Rais Dkt. @SuluhuSamia akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa KIA kwa ajili ya kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya yatakayofanyika Wilaya ya Mwanga, tarehe 13 Mei, 2025.
Kampuni ya Tembo Nickel Ltd imethibitisha ratiba ya kuanza rasmi ujenzi wa Mgodi wa Kabanga Nickel uliopo wilayani Ngara,Kagera.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Lifezone Metals inayomiliki kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Finland ukiimbwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko Mei 15, 2025 ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahimiza Waandishi Waendesha Ofisi kujiweka tayari ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia kwa kuendelea kujifunza na kuwa wabunifu zaidi kwa kuwa ustadi katika TEHAMA unakuwa ni sifa muhimu katika majukumu yao.
Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura awamu ya Pili
Katika mikoa ya:-
Arusha
Kilimanjaro
Manyara
Tanga
Dar es Salaam
Morogoro
Pwani
Mtwara
Lindi
Singida
Dodoma
Mjini Magharibi
Kaskazini Unguja
Kusini Unguja
Kaskazini Pemba na
Kusini Pemba
Kuanzia tarehe 16 - 22 Mei 2025
🌿 Ulinzi wa Milima ya Matogoro – Chanzo cha Maji, Hewa Safi, na Fursa za Utalii Songea 🌄
Matogoro si tu mlima, ni pumzi ya Songea. Misitu yake ni kinga dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, chanzo cha maji na matumaini ya uchumi wa kijani. Vijana, wazee – sote tuna wajibu wa kulinda urithi huu wa taifa.
#katibanasheria #MSLAC #SSH #kaziiendelee #SONGEA #RUVUMA #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #Matogoro
Mpango wa elimu ya msaada wa kisheria ulioanzishwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni hatua muhimu ya kuwezesha wanyonge kupata haki zao bila vikwazo vya kifedha. Kupitia mpango huu, gharama zote za mawakili zimelipwa na Rais Samia, hatua inayolenga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anaweza kufikia haki zake bila kujali hali yake ya kiuchumi. Huu ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya Rais Samia katika kulinda haki za wanyonge na kuimarisha misingi ya usawa wa kijamii.