Baadhi ya Wanaume huweza kuonesha dalili zinazofanana na za Ujauzito wakati wake zao wakiwa na Mimba. Hali hii inajulikana kitaalamu kama Couvade Syndrome na huambatana na dalili kama Kichefuchefu, Kutapika, Maumivu ya tumbo, Uchovu, Kuvimbiwa na Mabadiliko ya Hisia. Ingawa si ujauzito halisi, dalili hizi hujidhihirisha mwilini kama mwitikio wa kihisia unaoendana na ujauzito wa mwenza.
Mabadiliko haya huweza kuchochewa na ukaribu wa kihisia kati ya wenza, hasa pale Mwanaume anaposhiriki kikamilifu katika safari ya Ujauzito kama kuhudhuria Kliniki, kushiriki maandalizi ya Mtoto au kuonesha hisia kubwa juu ya ujio wa Mtoto.
Hali hii si Ugonjwa wala hatari kiafya, na mara nyingi dalili huanza kupungua kadri Ujauzito unavyokaribia mwisho au pindi mtoto anapozaliwa. Hata hivyo, ikiwa dalili zinakuwa nzito au zinasababisha usumbufu mkubwa, ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu
Kula sana Usiku kunaweza kukufanya uote Ndoto mbaya. Hii ni kwa sababu tumbo linapokuwa limejaa kupitiliza, Mwili hushindwa kupumzika vizuri.
Chakula kingi kinapomeng’enywa wakati wa Usiku huongeza Joto la mwili na kuharibu mzunguko wa Usingizi. Hali hii huathiri Ubongo na sehemu ya Mzunguko wa Usingizi ambapo ndoto nyingi hutokea.
Pia, kula vyakula vizito kama vya Mafuta au Sukari nyingi kabla ya kulala huongeza uwezekano wa kuota ndoto za ajabu au za kutisha.
Ni vizuri kula mapema na kwa kiasi, walau Saa 3 kabla ya Muda wa Kulala ili mwili upate muda wa kupumzika vizuri Usiku.
Kabla ya kugusa Sehemu zako za Siri, hasa wakati wa Kujisafisha, Kujikuna au wakati wa Faragha, hakikisha unaosha mikono yako kwa Sabuni na Maji safi.
Mikono michafu inaweza kusababisha maambukizi ya njia ya Mkojo, Fangasi, Muwasho kwenye Uume au Uke, Kutokwa na uchafu usio wa kawaida na Maumivu wakati wa Kukojoa au tendo la Ndoa.
Hili ni jambo rahisi, lakini lina mchango mkubwa sana katika kulinda afya yako ya Uzazi.
Mojawapo ya tiba rahisi ya asili inayosaidia kulainisha Choo ni Juisi ya Ukwaju.
Ukwaju una nyuzinyuzi nyingi za asili ambazo huchochea mfumo wa usagaji chakula kufanya kazi vizuri. Pia una Asidi za Asili zinazosaidia kusafisha njia ya chakula, kuondoa gesi tumboni na kurahisisha kutoka kwa kinyesi bila maumivu. Hii hufanya Ukwaju kuwa tiba nzuri na salama kwa wale wanaosumbuliwa na matatizo sugu ya Choo Kigumu na Kuvimbiwa.
Tengeneza juisi ya ukwaju nyumbani kwa kutumia mabonge ya ukwaju yaliyolowekwa kwenye maji moto, kisha changanya vizuri na epuka kuweka sukari nyingi. Kunywa glasi moja ya juisi hii asubuhi au jioni unapojisikia Umevimbiwa au Choo kimefunga. Ili kupata matokeo bora zaidi, hakikisha unakunywa maji ya kutosha siku nzima.
Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 21 anayesoma Chuo Kikuu cha Hanoi, Vietnam, amepata changamoto ya Ugonjwa wa Figo uliopelekea zishindwe kufanya mazi baada ya kutumia vinywaji vya kuongeza nguvu kwa wingi ili aweze kusoma hadi usiku wa manane.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyochapishwa na Jarida la VnExpress International, baada ya kutumia kiasi kikubwa cha Energy Drinks kila siku ili ahimili masomo yake, alianza kupatwa na dalili kama vile kuvimba kwa Miguu, kutapika kila mara na Uchovu uliokithiri ambapo baada ya kufikishwa Hospitalini, Madaktari walibaini tayari Figo zake zilikuwa zimefeli na sasa ataanza kupata huduma ya Kusafisha damu kwa Mashine mara 3 kwa wiki.
Kwa Tanzania, matumizi ya vinjwaji hivi yameongezeka sana siku za hivi karibuni huku vikihusishwa na Madhara mengi kwa Afya ikiwemo Uraibu, Kuharibika kwa Figo pamoja na magonjwa ya Moyo
Broccoli na Cauliflower ni mboga zenye uwezo mkubwa wa kuboresha afya ya Ubongo na Ngozi.
Kwa upande wa Ubongo, mboga hizi zina virutubisho kama choline, vitamini K na Viondoa Sumu ambavyo husaidia katika kuimarisha Kumbukumbu, kuzuia uharibifu wa Seli za Ubongo na kupunguza hatari ya Magonjwa ya Akili. Virutubisho hivi huongeza uwezo wa kufikiri na kulinda mfumo wa Neva dhidi ya uchakavu wa mapema.
Kwa upande wa Ngozi, Broccoli na Cauliflower zina vitamini C kwa kiwango kikubwa, ambayo husaidia katika uzalishaji wa Collagen, Protini muhimu kwa ngozi laini na yenye afya. Pia zina Viondoa Sumu vinavyopambana na mionzi hatarishi inayoathiri ngozi na kusababisha mikunjo na kuzeeka mapema. Kula mboga hizi husaidia ngozi kubaki na mvuto wa Ujana kwa muda mrefu.
Karanga, Korosho na Mbegu za maboga ni vyakula vyenye virutubisho muhimu vinavyoweza kusaidia kuboresha ubora wa shahawa.
Vina madini kama zinki, Magnesiamu na Selenium ambayo huhusika katika uzalishaji wa mbegu za kiume zenye afya. Pia, vyakula hivi vina mafuta yenye afya na Viondoa Sumu vinavyosaidia kupunguza madhara ya sumu mwilini na kuimarisha uzazi.
Kwa kula kwa wingi vyakula hivi pamoja na lishe bora, Mwanaume anaweza kuongeza nguvu na uimara wa mbegu za kiume, hivyo kuboresha afya ya uzazi kwa ujumla.
Karanga, Korosho na Mbegu za maboga ni vyakula vyenye virutubisho muhimu vinavyoweza kusaidia kuboresha ubora wa shahawa.
Vina madini kama zinki, Magnesiamu na Selenium ambayo huhusika katika uzalishaji wa mbegu za kiume zenye afya. Pia, vyakula hivi vina mafuta yenye afya na Viondoa Sumu vinavyosaidia kupunguza madhara ya sumu mwilini na kuimarisha uzazi.
Kwa kula kwa wingi vyakula hivi pamoja na lishe bora, Mwanaume anaweza kuongeza nguvu na uimara wa mbegu za kiume, hivyo kuboresha afya ya uzazi kwa ujumla.
Kutokwa na damu wakati wa Ujauzito mara nyingi ni hali ya dharura hivyo ni muhimu kumwona Mtaalamu wa afya haraka iwezekanavyo kwa uchunguzi na Matibabu.
Katika Ujauzito wa miezi ya mwanzo, kutokwa damu kunaweza kuwa ishara ya mimba kutoka (Miscarriage) au mimba ya nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic Pregnancy), hali ambazo zinahitaji matibabu ya haraka.
Katika miezi ya katikati au mwisho wa Ujauzito, damu inaweza kuashiria matatizo kwenye kondo la Uzazi kama Placenta Previa (Kondo kufunika mlango wa kizazi) au Placental Abruption (Kondo kujitenga mapema), hali zinazohatarisha maisha ya Mama na Mtoto.
Mwanamke Mjamzito akitokwa na damu, haijalishi ni kidogo au kingi, anapaswa kwenda hospitali mara moja kwa uchunguzi. Usisubiri kuona kama itaisha yenyewe. Ni bora kuchukua tahadhari mapema ili kuzuia madhara zaidi.
Kunywa mchanganyiko wa Limao na Tangawizi kila siku asubuhi kunaweza kuleta faida nyingi kwa afya.
Mchanganyiko huu husaidia kusafisha mwili kwa kutoa Sumu (Detox), kuboresha mmeng’enyo wa chakula, kuongeza kinga ya mwili kutokana na vitamini C ya limao na viambata vya kupambana na Uvimbe Joto vilivyopo kwenye Tangawizi.
Pia husaidia kupunguza uzito, kuongeza nishati asubuhi na kupunguza maumivu madogo madogo mwilini kama vile ya tumbo au viungo. Ni kinywaji rahisi lakini chenye nguvu ya kiafya.
@maila_kasorii Habari, inashauriwa asubiri siku 42, wakati ambapo maji na uchafu wa uzazi huwa umekoma kutoka ukeni. Hata hivyo, muda unaweza kuwahi au kuongezeka zaidi kwa kadri ya utayari wa kimwili na kihisia wa mwanamke mwenyewe.
Kutokufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kusababisha upatwe na tatizo la Choo Kigumu ambalo linaweza kutokea bila kujua hasa sababu yake ni nini.
Mwili unapokosa harakati, utumbo nao huwa na mwendo mdogo wa kusukuma chakula na kinyesi, hali inayosababisha mtu kuchelewa kwenda chooni au kupata choo kigumu. Mazoezi husaidia kuongeza mzunguko wa damu na kufanya misuli ya tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri, hivyo kurahisisha kutoka kwa kinyesi.
Watu wanaokaa muda mrefu bila kusimama au kutembea, kama vile ofisini au nyumbani, wako kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo hili. Ili kuepuka choo kigumu, ni vizuri kufanya mazoezi mepesi kila siku kama kutembea kwa dakika 30, kuruka kamba, au kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo.
Wanawake wanaokumbwa na changamoto ya kutopata Hedhi wanashauriwa kutumia Nanasi na Papai ili kurejesha na kurekebisha Hedhi zao
Papai lina kiasi kikubwa cha beta-carotene, ambacho husaidia mwili kuzalisha homoni ya Estrogen yenye Jukumu muhimu katika kuandaa na kuchochea ukuta wa mji wa mimba (Uterasi), hivyo kusaidia kutokea kwa Hedhi kwa wakati. Aidha, huongeza mikazo ya asili ya misuli ya Uterasi, jambo linalosaidia kurahisisha kutoka kwa damu ya Hedhi, hasa kwa wanawake wanaokumbwa na kuchelewa au kukosa kabisa Hedhi.
Kwa upande mwingine, Nanasi lina kiungo hai kinachoitwa Bromelain, ambacho husaidia kulainisha tishu za Uterasi na kuongeza mzunguko wa damu kwenye nyonga. Bromelain pia huchangia katika usawa wa Homoni kwa kupunguza Uvimbe na Msongo wa mawazo, hali ambazo mara nyingi husababisha kutokupata Hedhi kwa wakati.
Kwa pamoja, ulaji wa mara kwa mara wa Matunda haya kwa kiasi kinachofaa unaweza kusaidia kwa njia ya asili kurejesha au kudhibiti mzunguko wa Hedhi kwa Wanawake wanaokosa au kuchelewa kupata
Akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2025/26 leo Juni 12, 2025, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kupunguza Ushuru kwenye vinywaji vya 'Energy Drinks' ili kuweka unafuu kwa wazalishaji wa ndani, kuongeza ushindani na kuchochea uwekezaji nchini.
Dkt. Mwigulu amependekeza vinavyozalishwa ndani ya nchi kutoka shilingi 561 kwa kila lita hadi shilingi 134.2 kwa kila lita.
Hii inakuja baada ya kuwepo wa Changamoto kubwa inayohusu afya ya Umma ikisababishwa na Unywaji uliokithiri wa vinywaji hivi vinavyopendwa zaidi na Vijana ambavyo huhusishwa na Magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza hasa yale yanayohusisha Mfumo wa Moyo na Figo.
Akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2025/26 leo Juni 12, 2025, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kuongeza Ushuru kwenye vinywaji vya Kilevi vya ndani na nje ili kukusanya pesa zitakazosaidia kutunisha Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote
Amependekeza kufanyika kwa Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta sura 220 ili kutoza kiasi cha Tsh. 10 kwa kila lita ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya taa.
Aidha, kila tiketi ya Usafiri wa Treni inayotolewa itatozwa Tsh. 500 huku tiketi za Ndege zikitozwa Tsh. 1000
Akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2025/26 leo Juni 12, 2025, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kuanza kutoza ushuru wa Tsh. 50 kwa kila kilo ya Crips zinazozalishwa nchini na Tsh. 100 kwa zile zinazozalishwa nje ya Nchi.
Aidha, Ice Creams zitatozwa pia Ushuru kwa kiwango cha 5% kwa zinazotengenezwa nchini na 10% kwa zinazotoka nje ya nchi.
Lengo ni kupunguza changamoto za kiafya, ikiwemo Kiribatumbo kinachotesa Watanzania wengi, ambacho huchangia kutokea kwa magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza ikiwemo Shinikizo kubwa la Damu na Kisukari
Kwa afya bora ya Mtoto, hasa mwenye umri wa chini ya Miaka 5, yai lililochemshwa ndilo chaguo linalofaa zaidi kuliko yai la kukaanga.
Yai la kuchemsha hupikwa bila mafuta, Jambo linalolifanya kuwa salama na lishe safi kwa mtoto, tofauti na yai la kukaanga ambalo mara nyingi hutumia mafuta mengi ambayo si rafiki kwa afya ya mtoto mdogo. Aidha, huwa rahisi kumeng’enywa na tumbo la mtoto, na husaidia kupunguza uwezekano wa matatizo ya tumbo au mzio. Mbali na hilo huhakikisha halina vimelea hatari kama Salmonella, hivyo kumkinga mtoto dhidi ya maradhi yanayoweza kusababishwa na mayai ambayo hayajapikwa kikamilifu.
Kwa upande mwingine, yai la kukaanga linaweza kuwa na ladha nzuri lakini si chaguo bora kwa mtoto mdogo, hasa linapotengenezwa kwa mafuta mengi au linaongezewa viungo vikali na chumvi, ambavyo vinaweza kudhuru afya ya Mtoto.
Kwa ujumla, wazazi au walezi wanashauriwa kumpatia mtoto yai lililochemshwa vizuri kama sehemu ya mlo wake wa kila siku ili apate protini ya kutosha kwa ukuaji wa mwili na ubongo. Ingawa yai la kukaanga linaweza pia kuliwa na watoto, inashauriwa liwe limetengenezwa kwa kiwekewa mafuta mengi, viungo na chumvi.
Asubuhi sana (Alfajiri), mwili wako huwa katika hali ya joto la chini baada ya usingizi. Ukioga maji ya baridi na kuanzia Kichwani kunaweza kusababisha kusinyaa ghafla kwa Mishipa ya Damu, jambo linaloweza kupunguza mtiririko wa damu kwenda kwenye Ubongo na kusababisha Kizunguzungu, Kudondoka au hata kupoteza fahamu kwa muda mfupi
Njia salama ni kuanza kwa kumwagia maji kwenye miguu na mikono ili mwili upate muda wa kuzoea halijoto ya maji kabla ya kulowanisha Kichwa.
Fuatilia historia ya Ukoo wako ili ufahamu Magonjwa yaliyowahi kuwapata wanafamilia kama Babu, Bibi, Wazazi, Mashangazi au Wajomba.
Magonjwa kama Kisukari, Shinikizo la damu, Saratani, Kiharusi na matatizo ya Moyo yanaweza kuwa hutokea kwa watu wengi wa Ukoo wako.
Kwa kujua historia hii utaweza kuchukua tahadhari mapema kwa kubadili Mtindo wa Maisha, kula lishe bora, kufanya mazoezi na kupunguza Msongo wa mawazo au hata kuchukua hatua zingine stahiki.
Taarifa hizi husaidia kuishi kwa uelewa, kujitunza zaidi na kupunguza hatari ya Kuugua. Afya yako iko mikononi mwako, anza na historia ya ukoo wako.
Mwanaume, kagua Korodani zako mara moja kila wiki. Ukaguzi wa Korodani ni hatua rahisi lakini muhimu sana katika kuhifadhi afya yako. Kwa kufanya ukaguzi huu nyumbani, unaweza kugundua Mabadiliko au dalili za mapema ya Magonjwa kama Saratani ya Korodani hivyo kuokoa maisha yako kwa kupata Matibabu mapema.
Kwa kutumia vidole viwili, kagua korodani moja moja na uitambue kama kuna Uvimbe, Uchungu au usawa usio wa kawaida. Fanya ukaguzi polepole mbele ya Kioo, huku ukitafuta uvimbe wowote mgumu au mabadiliko ya saizi na umbo la Korodani zako. Kumbuka kufanya hivyo kwa kila Korodani peke yake ili kulinganisha.
Ni muhimu kufanya ukaguzi huu kila wiki, hasa kwa walioko katika umri wa miaka 15 na kuendelea kwani Saratani ya Korodani ni ya kawaida zaidi katika kundi hili la umri.
Ukigundua dalili kama Uvimbe, Maumivu au usumbufu usioelezeka, haraka wasiliana na daktari kwa uchunguzi zaidi na ushauri wa kitaalamu.