Indian YouTuber Abhinav Reddy met German traveller Safira in Bali. What began as a chance conversation turned into a cross-cultural friendship that led him to her peaceful village in Germany.
Their heartfelt videos, showcasing local life, family warmth and genuine human connection, are now being watched by millions. Sometimes the best journeys begin with a simple "hello." ❤️🇮🇳🇩🇪
( 📹 Source: Abhinav Reddy/FB)
1.Heshimu maelekezo ya walinzi na maafisa wa protokali wakati wote.
2.Usimkaribie kiongozi bila ruhusa au mwaliko.
3.Epuka kugusa mwili wa kiongozi isipokuwa kama yeye ameanzisha salamu ya mkono.
4.Simama kwa utulivu na uonyeshe heshima kwa lugha na mwenendo wako…….
5.Usizuie njia ya kiongozi au msafara wake.
6.Epuka kupiga picha au video kwa namna inayoweza kuathiri usalama bila ruhusa.
7.Kumbuka kuwa protokali si kwa ajili ya kujivuna, bali kulinda usalama, heshima na ufanisi wa shughuli rasmi.
Kuna baadhi ya Watanganyika ambao kwa muda mrefu wamekuwa na chuki au mtazamo hasi dhidi ya Zanzibar na Wazanzibari.
Mara nyingi hupinga karibu kila jambo linalotokea Zanzibar, hata pale ambapo ni jambo jema au lenye manufaa kwa Zanzibar. Hii imekuwa tabia inayojirudia kwa miongo kadhaa.
Mwalimu Julius Nyerere mwenyewe aliwahi kutambua uwepo wa hisia hizo na kuzitaja katika maandiko yake. Tangu miaka ya 1980 kulianza kujitokeza chokochoko mbalimbali dhidi ya Zanzibar ambazo hatimaye zilichangia kuondolewa kwa Rais Aboud Jumbe madarakani.
Baada ya hapo walimgeukia Rais Ali Hassan Mwinyi. Kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu utaratibu wa kuingia Zanzibar kwa kutumia kitambulisho au pasipoti. Shinikizo kubwa lilitoka Bara mpaka utaratibu huo ukaondolewa. Leo hii hata raia wa nchi jirani kama Uganda wanafanya biashara Zanzibar, ikiwemo maeneo ya Forodhani, bila kuwa na vikwazo vya aina ile iliyokuwa zamani.
Likaja suala la Zanzibar kujiunga na OIC. Badala ya kuachwa liamuliwe kwa kuzingatia maslahi ya Zanzibar, kulikuwa na upinzani mkubwa kutoka Bara. Wengine walifika mpaka kuleta hoja na maazimio kana kwamba Tanganyika ni dola ya kikristo.
Walitaka kuirejesha Tanganyika Mwishowe Zanzibar ililazimika kujiondoa OIC.
Baadaye likaja suala la mfumo wa vyama vingi. Katika muundo wa awali wa Muungano, Rais wa Zanzibar alikuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, kupitia mabadiliko yaliyosukumwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kutoka Bara, mfumo huo ukabadilishwa na Rais wa Zanzibar akaondolewa nafasi hiyo.
Wengi waliona hatua hiyo kuwa ni kinyume na roho ya Articles of Union ambazo zilikuwa msingi wa Muungano.
Kwa mtazamo wa baadhi ya Wazanzibari, hata mchakato wa uchaguzi Zanzibar umekuwa ukiingiliwa kutoka Bara. Wanaamini kuwa tangu uchaguzi wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1995, vyama vya upinzani kama CUF na baadaye ACT-Wazalendo vimekuwa vikipata uungwaji mkono mkubwa wa wananchi Zanzibar, lakini mabadiliko ya kisiasa yamekuwa yakizuiwa na nguvu kutoka Bara.
Kwa mtazamo huo, Zanzibar imekuwa ikinyimwa fursa ya kuona mabadiliko ya kisiasa yanayotokana na matokeo halisi ya uchaguzi.
Leo hii chokochoko zimehamia kwenye uwepo wa Rais Mzanzibari katika uongozi wa Jamhuri ya Muungano. Kumekuwa na mijadala na shinikizo mbalimbali yanayolenga Zanzibar, ikiwemo masuala ya ajira na nafasi za kazi. Kwa mtazamo wa baadhi ya Wazanzibari, hoja hizi zinaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kubadilisha demografia ya Zanzibar kwa kuongeza idadi ya watu kutoka Bara na hivyo kupunguza uzito wa wenyeji wa Zanzibar ndani ya nchi yao.
Wapo wanaoamini kuwa mwanya huo unatokana na kile wanachokiona kama udhaifu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kusimamia maslahi ya wazanzibari .masuala ya ajira, uhamiaji wa ndani na utambulisho wa Zanzibar.
Kwa mtazamo huo, lengo la baadhi ya makundi ni kuimeza Zanzibar taratibu kupitia mabadiliko ya demografia badala ya kupitia mabadiliko ya wazi ya kisiasa.
Aidha, viongozi wengi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar huwekwa madarakani kwa nguvu kutoka Bara.
Hivyo, wanaona kuwa uwezo wa SMZ kusimamia kwa uhuru maslahi ya Zanzibar unapungua na kutoa nafasi kwa shinikizo za nje kuendelea kuathiri mustakabali wa Zanzibar.
Kutokana na historia hiyo, Wazanzibari huona kwamba changamoto nyingi zinazoikabili Zanzibar leo hazitokani na Wazanzibari wenyewe pekee, bali pia na kile wanachokiona kama uingiliaji wa mara kwa mara wa Bara katika maamuzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Zanzibar.
Hoja hizi zimeendelea kuwa sehemu ya mjadala mpana kuhusu mustakabali wa Muungano, nafasi ya Zanzibar ndani yake, na namna ya kuhakikisha haki, usawa na heshima kwa pande zote mbili za Muungano zinalindwa.
Ants can build living bridges to cross rivers
Thousands of ants link their bodies together and continuously adjust the structure to help the colony reach the other side safely