@millardayo Ajira mpya kwa wabunge tayar mil.18 kwa mwezi na services nyingine nyingi za kutosha na mil 200 baada ya miaka mi5 ngoja tusbiri za walimu wenzangu kama zitatoka laki 5 na mili 60 baada ya miaka 40
NIMEIKUTA MAHALI- INAFIKIRISHA
Lissu ni Muasi au Mhaini?
Muasi ni mtu anayepinga au aliyekinyume au asiyemtiifu kwa Watawala au Kikundi Fulani. Lakini sharti Muasi awe sehemu ya hicho Kikundi.
Yaani kwa mfano kama wewe ni CHADEMA alafu ukapinga Jambo Fulani ndani ya CHADEMA ambalo wengi walilikubali basi wewe unageuka kuwa MUASI katka jambo husika.
Mtu wa CCM hawezi kuwa MUASI wa CHADEMA na mtu wa CHADEMA hawezi kuwa MUASI wa CCM kwa Sababu Kanuni ya uasi lazima mtu awe sehemu ya kikundi husika au sehemu husika.
Mfano; Muislam hawezi KUWA Muasi wa Ukristo na mkristo hawezi KUWA Muasi katika uislam.
UHAINI.
Uhaini ni kitendo cha kutaka kupindua serikali au ufalme au utawala Fulani au kitendo cha kutaka kusababisha Vita ambayo vita hiyo inalenga kupindua serikali au utawala au ufalme Fulani.
Mtenda uhaini sio lazima awe sehemu ya kikundi/utawala au sehemu ya nchi.
Hii ni kusema Raia wa Tanzania anaweza kufanya kosa la uhaini nchini Marekani lakini Raia wa Tanzania hawezi kuwa Muasi wa Marekani. Na ikitokea akajiunga na waasi wa Marekani Basi hataitwa Muasi isipokuwa ataitwa MAMLUKI.
Uasi ni Moja ya Mbinu zinazotumika katika kufanya Uhaini. Kwa sababu huwezi kuwa Mhaini ndani ya nchi yako kama haujawa MUASI.
Unaanza uasi ndipo unafuata Uhaini.
Je kila uasi ni Uhaini?
Hapana! Sio kila Uasi ni uhaini.
Mfano, Wamasai wa Ngorongoro walifanya Uasi dhidi ya serikali wakakataa kuhama kutoka Ngorongoro kuelekea Tanga. Ule ni Uasi. Yaani kutokutii amri ya Serikali.
Je Lisu na wenzake Kupinga uchaguzi Mkuu ni Uasi?
Ndio Lisu Kupinga uchaguzi Mkuu ni Uasi.
Je Lisu na wenzake Kupinga Uchaguzi Mkuu ni Uhaini? Hapana, Sio Uhaini.
Kupinga uchaguzi Mkuu sio kupindua serikali. Sio kutaka kuangusha utawala wala sio kutaka kuleta vita isipokuwa maamuzi ya serikali ya namna ya kushughulikia upingaji huo ndio huweza kuleta matokeo mazuri au Mabaya.
Lisu na wenzake wanasema NO REFORMS NA ELECTION wakimaanisha kama Sheria na Kanuni Fulani walizopendekeza hazitafanyiwa maboresho au kuwekwa Basi hakutakuwa na uchaguzi.
Hii ni kumaanisha Lisu na wenzake hawapingi uwepo wa uchaguzi isipokuwa wanataka Reforms ili uchaguzi ufanyike kwa Haki na Uhuru.
Katika ulingo wa Sheria na Haki, Lisu na wenzake wapo upande sahihi. Kwa sababu;
1. Hawajapinga uchaguzi isipokuwa wanataka Reforms katika uchaguzi ili ufanyike.
2. Wanataka HAKI na Uhuru katika uchaguzi.
Je Kupinga uchaguzi ni Kupinga serikali?
Hapana, Uchaguzi sio wa serikali bali ni uchaguzi wa wananchi kuchagua Serikali.
Uchaguzi Mkuu unahusu wananchi zaidi kuliko serikali inayochaguliwa au iliyopo madarakani.
Ikiwa uchaguzi Mkuu utaihusu serikali iliyopo madarakani au ile inayoenda kuchaguliwa hauwi tena uchaguzi kwani uchaguzi humaanisha Uhuru wa Haki katika kufanya Maamuzi ya kuchagua.
Je Lisu kuchochea Uasi katika Kupinga uchaguzi Mkuu bila reforms ni KOSA?
Sio Kosa kwa Sababu Lisu ni Mwananchi lakini pia kiongozi wa CHADEMA ambacho kimesajiliwa Tanzania. Anahaki ya Kutaka reforms za Haki zitakazowawezesha Watanzania wote kuwa Huru na kuchagua kwa Haki viongozi wataounda serikali itakayowaongoza.
Kwa maoni yangu hatua sahihi ambazo zingepaswa kuchukuliwa ambazo zinatija na za HAKI;
1. Serikali ingeunda tume ya kuunda hizo reforms za uchaguzi ambapo wadau wote wangehusishwa katika uundaji wa hizo reforms. Reform lazima ziguse maslahi ya wananchi ambao watafanya uchaguzi na sio vyama vya siasa.
2. Uchaguzi wa mwaka ungesogezwa mbele kwa hoja ya dharura kuwasilishwa bungeni. Ili kupisha mchakato.
3. Mijadala na midahalo mbalimbali ingeitishwa na elimu kutolewa.
4. Vyombo vya Dola havipaswi kuwatumikia Wanasiasa isipokuwa vitumikie wananchi kwa kufuata Sheria.
5. Mchakato wa Katiba MPYA ungeendelea pale ulipoishia.
Je Lisu ni Muasi au Mhaini?
Hii ni tungo tata- mjadala uendelee
Ijumaa Kareem.
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato
Robert Heriel
Mtunzi wa makala hii