#VIDEO
📍Bangkok, Thailand
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss Grand International 2026 ambayo fainali yake inafanyika muda huu huko Bangkok, Thailand, Jihan Dimack ametoa wito kwa Mataifa duniani kudumisha amani, upendo na umoja, akieleza kuwa Watu wengi wasio na hatia wanaendelea kupoteza maisha, familia, makazi na ndoto zao kutokana na migogoro inayoendelea katika maeneo mbalimbali duniani.
Jihan amesema anajivunia kuzaliwa Tanzania, Taifa linalotambulika kwa amani, upendo na umoja ambako Watanzania wanaamini katika kuishi na kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali tofauti za asili, dini au mila, huku akisisitiza kuwa amani ni ishara ya ujasiri na sio udhaifu.
“Haijalishi unatoka wapi, tuuache ubinadamu upewe nafasi yake na tusiruhusu mioyo yetu kutawaliwa na chuki, tueneze amani na upendo, na tuishi kwa maelewano, asanteni,” amesema Jihan. #MillardAyoUPDATES #MissGrandInternational2026