Kadiri miaka inavyokwenda, nimejifunza jambo moja muhimu sana: maisha ya bandia ni maisha ya gharama kubwa sana. Gharama yake si fedha tu, bali pia ni gharama ya kiroho, kihisia, kisiasa na hata kimahusiano.
Ukweli ni rahisi kuishi nao. Uongo, kwa upande mwingine, unahitaji matengenezo ya kila siku.
Mwanasiasa anapoanza kujenga umaarufu wa bandia, unyenyekevu wa kuigiza, utajiri wa kuonyesha, au picha ya mtu mkamilifu asiye na dosari, anajikuta akitumia nguvu nyingi kuilinda taswira hiyo. Uongo mmoja huzaa mwingine, na maigizo ya leo huzaa maigizo ya kesho. Mwishowe, mtu haishi tena maisha ya kawaida; anaishi maisha ya kisiasa kila dakika. Na hilo linachosha sana.
Tatizo kubwa la siasa za dunia yetu ni kwamba mara nyingi tunathamini zaidi muonekano kuliko uhalisia. Watu wanajikuta wakitaka kuonekana wenye nguvu kuliko walivyo, matajiri kuliko walivyo, na wenye ushawishi kuliko walivyo. Ndiyo maana wakati mwingine tunaona misafara mikubwa, sifa za kulipwa, propaganda na maisha ya kifahari kupita kiasi. Mara nyingi si kwa sababu watu wanafurahia hayo, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wa kawaida.
Lakini taswira inapokuwa kubwa, gharama ya kuilinda nayo huwa kubwa zaidi.
Wakati mwingine watu wanaonekana kucheka mbele ya kamera, lakini ndani wamejaa hofu, wasiwasi na upweke mkubwa. Hawajui tena nani anawapenda kwa dhati, nani anawaogopa, nani anawasifia kwa maslahi, na nani anasubiri siku ya kuanguka kwao.
Nafikiri moja ya gharama kubwa zaidi za maisha ya bandia ni kupoteza amani ya ndani. Mwanadamu hakuumbwa kuigiza maisha milele. Nafsi huchoka kubeba mtu ambaye si yeye halisi.
Ndiyo maana naamini kwamba uhalisia ni nafuu kuliko maigizo. Kiongozi wa kweli hahitaji kuigiza kila siku. Anaweza kukosea kama binadamu mwingine yeyote, lakini hahitaji kuishi kwa ajili ya kuwalazimisha watu waamini picha ambayo si ya kweli.
Na kuna jambo ambalo historia imenifundisha. Wakati mwingine mtu aliyekaa ndani ya msafara mkubwa, akiwa na walinzi na heshima zote za dunia, anaweza kukosa amani kuliko mtu anayepita pembeni kwa miguu.
Kwa sababu amani haitokani na ukubwa wa msafara, wala haitokani na ukubwa wa cheo. Amani hutokana na dhamiri safi, ukweli wa ndani, na kuishi maisha yanayofanana na wewe halisi.
Mwisho wa yote, watu hawatakumbuka sana ukubwa wa magari yetu, wala ukubwa wa majumba yetu. Watakumbuka kama tuliishi kwa ukweli, kama tulikuwa waaminifu kwa dhamiri zetu, na kama tulitumia nafasi tulizopewa kuwatumikia watu kwa uadilifu na hofu ya Mungu.
Katika demokrasia:
Mahakama ni kubwa kuliko Jaji Mkuu.
Bunge ni kubwa kuliko Spika.
Taifa ni kubwa kuliko Rais.
Katiba ni kubwa kuliko chama tawala.
Hii ni kwa sababu taasisi zinapaswa kudumu, wakati viongozi ni wa muda.
1. TAIFA NI KUBWA KULIKO RAIS
Rais ni kiongozi wa muda.
Taifa ni la kudumu.
Rais anaweza kukaa madarakani miaka 5, 10 au 20.
Lakini taifa linaendelea kuwepo kabla yake na baada yake.
Mfano:
United States imekuwa na marais wengi sana.
Wamekuja:
Ronald Reagan
Bill Clinton
Barack Obama
Donald Trump
Lakini Marekani imebaki kuwa Marekani.
Rais ni mtumishi wa taifa.
Taifa si mali ya Rais.
Ndiyo maana katika demokrasia, kumpinga Rais si sawa na kulichukia taifa.
Na kumuunga mkono Rais si sawa na kuwa mzalendo.
Uzalendo ni kuipenda nchi hata pale unapokosoa serikali.
2. SERIKALI SI TAIFA
Hili ndilo eneo ambalo watu wengi huchanganyikiwa.
Serikali ni chombo kinachosimamia nchi kwa kipindi fulani.
Taifa ni wananchi wote pamoja na historia, ardhi, taasisi na mustakabali wao.
Kwa mfano:
Leo serikali inaweza kubadilika.
Lakini:
Tanzania inabaki Tanzania.
Bendera inabaki ile ile.
Wananchi wanabaki wale wale.
Historia inabaki ile ile.
Kwa hiyo:
Kuikosoa serikali si kuisaliti nchi.
Na:
Kuisifu serikali si lazima iwe kuipenda nchi.
Swali muhimu ni:
โJe jambo hili linafaidisha taifa?โ
si โJe jambo hili linaifurahisha serikali?โ
3. CHAMA TAWALA SI SAWA NA NCHI
Hili ni somo muhimu sana kwa Afrika.
Katika demokrasia:
Chama tawala ni mshindi wa uchaguzi.
Hakimiliki taifa. Hakimiliki serikali milele.
Hakimiliki uzalendo.
Taifa ni mali ya:
waliokichagua chama tawala,
wasiokichagua chama tawala,
na hata wale ambao hawakupiga kura.
Ndiyo maana katika nchi zilizoendelea kisiasa:
Ukikosoa chama tawala huonekani adui wa taifa.
Unaonekana sehemu ya demokrasia.
Tatizo linaanza pale chama tawala kinapoanza kuonekana kama taifa lenyewe. Hapo demokrasia huanza kudhoofika.
4. KATIBA NI KUBWA KULIKO CHAMA TAWALA
Katiba ndiyo mkataba mkuu wa taifa.
Katiba ndiyo inayotoa mamlaka kwa:
Rais, Bunge Mahakama.
Sio Rais anayeipa Katiba nguvu.
Ni Katiba ndiyo inayompa Rais nguvu.
Sio chama tawala kinachounda taifa.
Ni Katiba ndiyo inayoweka sheria za namna taifa litakavyoendeshwa.
Katika demokrasia iliyokomaa:
Kama chama tawala kinataka jambo ambalo Katiba hairuhusu,
Katiba ndiyo hushinda.
Kwa sababu Katiba inawakilisha taifa lote.
Chama kinawakilisha wanachama wake.
5. BUNGE NI KUBWA KULIKO SPIKA
Spika ni kiongozi wa muda.
Lakini Bunge ni taasisi ya kudumu.
Leo kuna Spika mmoja.
Kesho atakuwepo mwingine.
Lakini Bunge linaendelea kuwepo.
Hii ndiyo sababu taasisi ni muhimu kuliko watu.
Mtu anaweza kuondoka.
Taasisi inapaswa kubaki imara.
6. MAHAKAMA NI KUBWA KULIKO JAJI MKUU
Jaji Mkuu ni mtumishi wa Mahakama.
Sio Mahakama mali ya Jaji Mkuu.
Kesho Jaji Mkuu akistaafu:
Mahakama inaendelea.
Hii ndiyo maana ya utawala wa sheria.
Sheria inapaswa kuwa kubwa kuliko watu wanaozisimamia.
TATIZO KUBWA AFRIKA
Katika nchi nyingi za Afrika watu hufikiri hivi:
Chama = Taifa
Serikali = Taifa
Rais = Taifa
Kukosoa Serikali = Kuisaliti nchi
Hiyo ndiyo sababu mjadala wa kisiasa huwa mgumu.
Kwa sababu watu wanafikiri wanalinda taifa wakati mara nyingi wanakuwa wanalinda serikali au chama.
Lakini katika demokrasia yenye afya:
Taifa ni kubwa kuliko serikali.
Serikali ni kubwa kuliko chama.
Katiba ni kubwa kuliko serikali.
Sheria ni kubwa kuliko viongozi.
Dhamira ni kubwa kuliko utii wa kipofu.
Kwa lugha rahisi sana
Ukiniuliza tofauti kati ya nchi, taifa na serikali ningesema:
Nchi ni ardhi, mipaka na mamlaka yake.
Taifa ni watu wake, historia yao, utamaduni wao, taasisi zao na mustakabali wao.
Serikali ni timu ya muda iliyopewa jukumu la kuendesha taifa kwa kipindi fulani.
Ndiyo maana unaweza kubadilisha serikali bila kubadilisha taifa.
Lakini ukiharibu taifa, hata serikali nzuri haiwezi kulirudisha kwa urahisi.
Kwa hiyo kiongozi wa kweli hapaswi kuuliza:
โJe hili linaisaidia serikali?โ
Bali: โJe hili linaimarisha taifa, taasisi zake, na vizazi vijavyo?
Watoto wa Mwenyekiti Tundu Lissu wamekua wakisikia simulizi za baba yao akiteswa na hata kushambuliwa kwa risasi kwa ajili ya kupigania haki za watu wengine. Leo, mtoto wake yuko barabarani akidai uhuru wa baba yake. Ni hadithi ya kutia moyo, lakini pia ya kuhuzunisha sana.
Mhe. @HecheJohn ,
Taasisi ya @ChademaTZ2 inahitaji kuwa na institutional integrity; inahitaji kujipambanua kwa values.
Tuliposikia story za Abdul na Wenje, haraka tulihoji values.
Tunatamani kuwaona viongozi mkijitofautisha kwa kusimamia values na kuepuka masihara.
Thanks!
"Mabadiliko lazima yaje. Tuyafanye katika utaratibu wa kawaida. Tusipofanya hivyo, wale wasioridhika wanaweza kutumia njia nyingine. Na njia nyingine hizo huwa zinaleta matatizo." Jaji Joe Sinde Warioba.
UWAJIBIKAJI NI MSINGI WA UADILIFU.
Ukipewa dhamana ya kuongoza watu, huongozi kwa hisia, matamanio binafsi au mihemko ya muda.
Uongozi hujengwa juu ya Katiba, Sheria, Kanuni na misingi ya Utu na haki. Kiongozi hapaswi kufanya maamuzi kwa hofu ya vitisho, ushawishi wa marafiki, makundi ya maslahi au shinikizo la kisiasa, bali kwa uadilifu, busara na wajibu kwa Umma.
Maamuzi ya Kiongozi lazima yawe na ubora, weledi na uhalali unaostahili, yakilenga maslahi mapana ya Taifa na watu wake anao waongoza , siyo kuridhisha nafsi au kundi fulani.
Kiongozi mwenye maono hutambua kuwa mamlaka ni dhamana, na dhamana hiyo hupimwa kwa haki anayotoa, usawa anaousimamia na ukweli anaouthamini.Kiongozi anawajibika kwa kiapo chake kupitia dhamiri kwa Mungu.
Fanya maamuzi kwa kiwango ambacho hata Mungu akichungulia duniani, aone haki imetendeka, ukweli umeheshimiwa na utu wa mwanadamu umepewa thamani yake kisha atabasamu.
Je wewe katika nafasi yako Mungu akichungulia Duniani atatabasamu? au atasikitika na kujuta kukuumba?
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI NDIYO DAWA YA KULIPONYA TAIFA.
BAK Mwabukusi.