Asante sana wakili msomi Mwabukusi
Hatukukosea kukupambania ili uwe Rais TLS - asanteni sana mawakili kwa kumpa kura @Mwabuk2Boniface
Umenyooka na kueleweka! Kama wameumia wanywe sumu ๐
#FreeTunduLissu NOW ๐๐ฝ๐ฅ
Mwenyekiti wetu alisema haya miaka 12 iliyopita, kama kawaida ya watawala dhalimu wakapuuza ushauri wa mtu mwema huyu.
Ccm wanakwenda kuingiza Nchi yetu shimoni, Watanzania tunapaswa kuungana kuokoa Nchi hii.
ANAANDIKA MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA
DR. @rugemeleza
Kwa vyovyote itakavyotolewa na kusema Tume ya Jaji Chande Othmani Juu ya Vurugu na Mauaji ya October 29, 2025 ni batili na haramu tokea ilipoundwa. Kwa sababu zifuatazo:
1. Imeundwa na Samia Suluhu Hassani ambaye ndiye mtuhumiwa namba Moja kwani ndiye alitoa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji na watu ambao hawakuwa waandamanaji.
2. Samia alisema wakati wa Kampeni haramu za Udanganyifu Mkuu kuwa wanaosema hakutakuwa na uchaguzi wakumbuke kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na kuwa hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi.
3. Waandamanaji hawakuwa na silaha za moto ajabu yake walipigwa risasi kinyume kabisa na taratibu za kimataifa na nchi yetu za kukabiliana na waandamanaji ambazo ni matumizi ya mabomu ya machozi, maji ya kuwashawasha, hewa ya pilipili na ikilazimika risasi za plastiki.
4. Kuwekwa kwa zuio la kutoka nje na kutembea lililotangazwa na IGP Camillius Wambura ilikuwa kinyume Cha Sheria kwani hana mamlaka hayo.
5. Kuzimwa Kwa mtandao wa intaneti kwa siku sita ilikuwa kinyume Cha Sheria. Kwa kuzimwa kwake mauaji mengi yalitokea na yalisababisha watu kutokupata taarifa za kiwakati juu ya maovu makubwa yaliyofanywa na vyombo hivyo vya dola.
6. Kuzimwa kwa mtandao na zuio la kutoka nje sehemu nyingi za nchi yetu ilimaanisha hata wafanyakazi na mawakala wa Tume ya Udanganyifu Mkuu ya Jacobs Mwambegele haikuwa na uwezo wa kupata matokeo ya uchaguzi huo haramu. Ajabu yake Mdanganyifu huyo Mkuu asiyeheshimu kazi na maadili ya ujaji akatangaza matokeo kama kwamba uchaguzi ulifanyika na kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa katika Kila kituo na hatimaye kutumwa kwa Tume hiyo haramu!
7. Stargomena Tax ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Samia wakati wa udanganyifu huo ni mjumbe katika Tume hiyo ya Chande! Ni kanuni ya kisheria na haki kuwa huyu ana mgogoro wa kimaslahi na ni sehemu ya waliopaswa kuchunguza imekuwaje akageuka kuwa mchunguzi.
8. Jaji Othmani Chande na Jaji Ibrahimu Juma wanajua, kama wajuavyo wanasheria na wasomi wote, kuwa huwezi ukawa hakimu au muamuzi katika kesi yako mwenyewe(Nemo judex in causa sua) sasa imekuwaje wawe katika Tume ambayo ina kasoro hii kubwa? Je, si inafahamika kuwa pale Tume inapokuwa na kasoro hiyo yote iliyoyafanya hata kama ni mazuri, kisheria Huwa batili?
9. Wakati Tume inaanza kazi Samia ametoa matamshi ya kuingilia kati au kutoa majibu kwa Time ikiwa ni pamoja na kusema "nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi" na kuwa "kwa nini wazazi hamkuwazuia watoto wenu kutoka nje?". Sasa hapo nini kinachunguzwa?
10. Tume ilizuia uwazi wa watu waliotoa maelezo yao kwa kuvikataza vyombo vya habari kuendelea kutoa maelezo ya waathirika wa mauaji hayo ya kinyama yaliyofanywa na vyombo vya dola. Kukosekana kwa uwazi ulikuwa mkakati wa kuleta giza na kuzuia ukweli wa mauaji hayo kufahamika na hivyo kile kitakachosemwa na Tume kuwa eti ndicho kilichosemwa na waathirika kichukuliwe kuwa ni cha ukweli.
11. Tume yenyewe imeanza kampeni ya kuuandaa umma kupokea ripoti yake na imekuwa na wasemaji wake. Hiyo inaashiria nia mbaya ya Tume hiyo.
Ni kwa msingi na sababu hizo nasema kuwa Tume hiyo ni batili na chote kitakochotolewa nayo ni batili.
Waandishi Takamwili (The Junk Journalists).
Waandishi wetu wa habari wamegeuka wataalamu wa geopolitics. Leo wanaandika thesis ndefu kuhusu Israel na Iran โ missile trajectories, proxy wars, nuclear ambitions, who blinked first, n.k.
Hawa โwahuniโ wana uwezo wa ajabu wa kuona vumbi la mchanga katika mitaa ya Tehran na Mashariki ya Kati yote, lakini hawaoni moshi wa baruti uliopita mlangoni kwao miezi minne tu iliyopita.
Wanajua idadi ya vifo vya watoto wa Tehran kwa takwimu za nukta, lakini idadi ya Watanzania waliopotea au kupigwa risasi wakati wa uchaguzi mkuu ni "habari zisizo na uthibitisho" au "uchochezi."
Wana uwezo wa kuona kombora la Fattah-1 likifyatuliwa kutoka Isfahan, lakini macho yao yanapata upofu ghafla (glaucoma ya kisiasa) kuhusu yaliyotokea mitaani kwetu 29 Oktoba 2025.
Ukiwauliza kuhusu Oktoba 29, 2025 โ siku ambayo raia wetu walipigwa risasi kama target practice, miili ikarundikwa hospitalini au ikachukuliwa na โghost squadsโ, wanasema hawana material.
Habari za Oktoba 29, 2025 โ wanakuwa kama paka aliyemeza uji wa moto. Mdomo mzito, vidole vyao vinakuwa paralyzed, keyboard inakuwa exhibit A ya kutengeneza museum ya uoga. Shensisana.
Wachambuzi wa vita za mbali, lakini viziwi na bubu wakati damu inamwagika barabarani kwao. Wakati huo huo wanaweza kutoa maoni zaidi ya 200 kuhusu kama drone ya IRAN ililenga au la!
kizazi kinachoweza kuandika kurasa 100 kuhusu Mashariki ya Kati, lakini kikitakiwa kuripoti tukio la ukatili wa Serikali hapa nyumbani, vidole vyao vinapata kiharusi cha ghafla. Kizazi takamwili.
Ni hovyo with extra cheese, takamwili iliyopakwa rangi ya blue check na verified nonsense. Wakati raia wetu walipigwa risasi na kuuawa, wahuni walikuwa busy kuchambua SIMBA na YANGA.
Ni rahisi kulaani uvamizi wa Israel kuliko kulaani uvamizi wa mabomu ya machozi mtaani kwao. Wanalilia damu ya raia wa IRAN kuliko kutaja jina la Mtanzania aliyeuwawa kwa ajili ya kura yake.
Wanasubiri ndege za kivita za Iran na Israeli zifanye manoeuvre angani huko ili wapate cha kuandika, huku wakijifanya hawasikii vilio vya wajane na mayatima wa uchaguzi mkuu uliopita.
Briefcase journalism. Ni kizazi kilichogeuza kalamu zao kuwa kijiko cha kulia mchuzi wa serikali, wakiacha taaluma yao ikizikwa kaburini futi 6. Kizazi hiki cha wanahabari โ selective outrage
@MsigwaPeter " wapo wanao piga kelele wakisema kila mwana CCM ni shetan"
Sasa twambie kama siyo kila mwana CCM ni shetan, twambie huyo ambaye siyo shetan ni nani, ili hali anaendelea kushirikiana na mashetan, na ni active member wa mashetan, na wala hayuko bize kukemea maovu ya mashetan hao
Anaandika Mwanasheria mkuu wa CHADEMA DR. Rugemeleza Nshala.๐๐พ
Samia na wenzake wote waliotwaa madaraka ya nchi kinyume cha demokrasia kushiriki katika mchakato wa kuliokoa na kulileta Taifa pamoja. Wote hawa wanatakiwa kujiuzulu mara Moja.
1. Samia atueleze Watanzania na Dunia Nzima ni nani aliyetoa amri ya kuuawa kwa Watanzania waliokuwa wakidai uchaguzi huru na haki?
2. Je ni Sheria ipi katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayompa Raisi madaraka ya kuzuia raia kuandamana na kusema "hakutakuwa na nywinywi Wala nywinywinywi"?
3. Je, kauli yake hiyo si ndiyo ilikuwa amri kwa Jeshi la Polisi la kuwafyatulia raia risasi za kuua kuzuia wasiandamane?
4. Je, anaifahamu na kuielewa ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayosema kuwa Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwa jamii kwa mujibu wa sheria?
5. Kama anaifahamu je anakumbuka kuwa ni miongoni mwa ibara alizotuapia na kutueleza kuwa atazilinda na kuzitetea mnamo tarehe 19 Machi 2021? Na Kwa Nini hakufanya hivyo mnamo na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025?
6. Kama Raisi, wakati uchaguzi unafanyika, nani alitoa amri ya kuzimwa intaneti kwa siku tano?
7. Ni nani aliyempa mamlaka IGP Wambura kuweka zuio "curfew" kwa wakazi wa Dar es Salaam na amri hiyo kutekelezwa katika sehemu mbali mbali nchini wakati hakuna Sheria inayomruhusu kufanya hivyo?
8. Kama si yeye, alichukua hatua gani za kinidhamu na kisheria dhidi ya IGP Wambura na wote hao waliojivika madaraka wasiyo kuwa nayo kisheria?
9. Ni nani aliyetoa amri ya miili ya waliouawa kuchukuliwa na kupotezwa bila kukabidhiwa kwa ndugu zao?
10. Ni nani aliyeamuru wapendwa wetu hao kutupwa na kurundikwa kwenye na nje ya mochuari kama mizoga?
11.. Ni nani aliyezuia Taifa kuwaomboleza waliouawa kinyama na Jeshi la Polisi na vikosi vingine vya Usalama?
12. Je Samia anafahamu msemo usemao za "buck stops at the president" ikimaanisha uwajibikaji katika serikali humwangukia raisi?
13. Sasa kama anafahamu msemo huo anasubiri nini yeye na genge lake kuondoka madarakani?
MWISHO
REPOST 200
TUTAKUWEPO๐ซต๐พ๐
@MariaSTsehai@VodacomTanzania@airtel_tanzania@YasTanzania_ Kabsa, haya mamitandao yanakera, kungekuwa na alternative ntungeviacha,
Vifurush tununue sisi, na bado wanatupangia mda wa kisha, then wanazima any time wakijiskia na vifurush vyetu vinafia humo...yaaan ๐๐
@MariaSTsehai Mimi nafkri JWTZ waachwe tu kama walivyo, ktendo cha maharamia kuzidi kuwabana na kuwapa mashariti magumu, kitawapa akili ya kugundua wako kwenye box hivyo wataanza kufkri namna ya kutoka.