Mbunge wa Baraza la Uwakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said amesema licha ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini kuna โYudaโ ndani ya Serikali.
Simai ameyasema hayo leo Juni 2, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
โDotto Biteko aliwahi kusema Binadamu ni walewale, nataka niwaambie hawa walewale nambatiza mmoja aliyekuwepo ndani ya Serikali basi ni Yuda, nasema hivyo kwa sababu tunataka maendeleo ya Nchi yetu, je Mama kakosea wapi ? Kwa sababu ya kumwamini Mtu kumbe ni Yuda ambaye amesaliti ndugu zake hata ile familia iliyomleaโ
โYuda tumeona ameanza kuibuka kwenye Nyumba za Ibada kutafuta huruma za Wananchi na Watu mbalimbali lakini nataka niseme Wabunge wenzangu na Serikali iliyopo hapa tuamkeni, leo anapita anataka kutuaminisha kwamba Rais Magufuli alimpenda,โ amesema Simai.
Kwa mujibu wa Biblia, Yuda Iskariote ni mmoja wa Wanafunzi 12 wa Yesu Kristo anayejulikana kwa kumsaliti Yesu kwa Vipande 30 vya fedha.
#MillardAyoUPDATES