Imeelezwa kuwa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa matukio
ya wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 ni
Tume ambayo imeundwa Kisheria na Kikatiba na hivyo
Tume halali ambayo iko kisheria.
Hayo yamebainishwa na Wakili Msomi Sweetbert Nkuba
wakati akizungumza na wanahabari na kueleza hata uwezo
na sifa za Wajumbe zimezingatia viwango vya kisheria hasa
kwa kuweka Wajumbe kutoka nje ya Tanzania na kufanya
Tume hiyo kuwa huru na isiwe Tume ya nchi kujichunguza wenyewe.
📍BARABARA ZA AFCON
VIDEO
RC MAKALLA ATAKA WALIOLIPWA FIDIA
KUONDOKA KUPISHA UJENZI WA BARABARA ZA AFCONA
Amshukuru Rais Samia kuwezesha barabara zote muhimu kwa ajili ya AFCON
Asema Barabara hizo zitaondosha foleni na kuchochea utalii.
📍AFCON
RC MAKALLA ATAKA WALIOLIPWA FIDIA KUONDOKA KUPISHA UJENZI WA BARABARA ZA AFCON🇹🇿
Amshukuru Rais Samia kuwezesha barabara zote muhimu kwa ajili ya AFCON
Asema Barabara hizo zitaondosha foleni na kuchochea utalii
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amewataka wananchi wote waliolipwa fidia kwenye maeneo zinapojengwa barabara zote kwaajili ya maandalizi ya Michuano ya Mpira wa Miguu Mataifa ya Afrika - AFCON 2027, kuondoka ili kuruhusu Mkandarasi kuendelea na utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhe. Makalla ametoa agizo hilo leo Julai 29,2026, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa Km 9.1 kuanzia Makutano ya Ngarenaro - mzunguko wa Kisongo, Makutano ya Ngarenaro - Kona ya Nairobi na Makutano ya Ngarenaro - soko la Kilombero, kwa njia nne, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 87.9.
"Nimshukuru Mhe. Rais kwa kuwezesha ujenzi wa barabara hizi, niwaombe watalamu wasekta zote kutoa ushirikiano kuhakikisha hakuna kizuizi kwa Mkandarasi kufanya kazi, serikali ileshawalipa fidia wananchi wote kwa barabara zote za AFCON, zaidi ninawashukuru ambao wameshaondoka wameonesha uzalendo, na ambao hawajaondokaa niwaombe waondoke ili kupisha ujenzi ." Amesema Mhe. Makalla.
Aidha, CPA Makalla amebainisha kuwa, kukamilika kwa barabara hizo licha ya kuwa zitachochea shughuli za utalii na AFCON 2027 zaidi zitapunguza msongamano wa magari katika Jiji la Arusha.
📍 Zanzibar
PICHA ZAIDI
RAIS DKT. MWINYI AWAAPISHA VIONGOZI WANNE WATEULE IKULU ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wanne aliowateua hivi karibuni, wakiwemo
majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amewaapisha viongozi hao leo, tarehe 24 Julai 2026, katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
📍ZANZIBAR
RAIS DKT. MWINYI AWAAPISHA VIONGOZI WANNE WATEULE IKULU ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wanne aliowateua hivi karibuni, wakiwemo majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amewaapisha viongozi hao leo, tarehe 24 Julai 2026, katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
Viongozi waliokula kiapo ni:
1. Dkt. Mahadhi Juma Maalim
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.
2. Mhe. Valentina Andrew Katema
Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
3. Mhe. Khamis Ali Simai
Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
4. Dkt. Josephine Rogate Kimaro
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla;
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi Ali Maulid; Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ndg. Mansoura Mossi Kassim; pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini na wageni waalikwa.
📍Kunduchi, Dar es Salaam.
VIDEO
📍Kunduchi, Dar es Salaam.
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AMWAKILISHA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MAHAFALI YA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 23 Julai 2026, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mahafali ya 14 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Mahafali hayo yalihitimisha mafunzo ya ngazi ya juu ya Mkakati wa Ulinzi na Usalama, ambapo jumla ya wanafunzi 72 kutoka Tanzania na nchi mbalimbali walihitimu baada ya kukamilisha mafunzo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Rais katika hafla hiyo, Dkt. Nyansaho alisisitiza kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jukumu la kila Mtanzania, bila kujali nafasi au wajibu alionao. Alibainisha kuwa amani, utulivu na usalama wa nchi vinategemea ushirikiano wa wananchi wote katika kulinda mipaka, rasilimali na maslahi ya Taifa.
Aidha, aliwataka wahitimu wa kozi hiyo kutumia maarifa, ujuzi na uzoefu walioupata katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika maeneo yao ya kazi, huku wakisimamia kwa weledi na uzalendo ulinzi wa rasilimali na maslahi ya Taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
📍Kunduchi, Dar es Salaam.
PICHA ZAIDI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 23 Julai 2026, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mahafali ya 14 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
📍Kunduchi, Dar es Salaam.
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AMWAKILISHA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MAHAFALI YA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 23 Julai 2026, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mahafali ya 14 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Mahafali hayo yalihitimisha mafunzo ya ngazi ya juu ya Mkakati wa Ulinzi na Usalama, ambapo jumla ya wanafunzi 72 kutoka Tanzania na nchi mbalimbali walihitimu baada ya kukamilisha mafunzo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Rais katika hafla hiyo, Dkt. Nyansaho alisisitiza kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jukumu la kila Mtanzania, bila kujali nafasi au wajibu alionao. Alibainisha kuwa amani, utulivu na usalama wa nchi vinategemea ushirikiano wa wananchi wote katika kulinda mipaka, rasilimali na maslahi ya Taifa.
Aidha, aliwataka wahitimu wa kozi hiyo kutumia maarifa, ujuzi na uzoefu walioupata katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika maeneo yao ya kazi, huku wakisimamia kwa weledi na uzalendo ulinzi wa rasilimali na maslahi ya Taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
📍Burkina Faso.
RAIS IPU DKT. TULIA ACKSON ATEMBELEA WANAWAKE KITUO CHA UZALISHAJI NCHINI BURKINA FASO.
Julai 23, 2026. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mh. Dkt. Tulia Ackson ametembelea wanawake wa kituo cha uzalishaji wa sanaa cha Godé (UAP Godé) huko Kamsonghin ambapo aliambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Bunge la Burkina Faso Haoua Fofana, wajumbe wa wabunge na wawakilishi kutoka Wizara ya Familia na Mshikamano, huku akiwepo Mkurugenzi wa Mkoa wa Wizara ya Familia na Mshikamano Abdou Guebre.
📍Paris, Ufaransa.
DKT. MWIGULU AALIKA WAFANYABIASHARA WA UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA.
WAZIRI MKUU Dkt Mwigulu Nchemba amewaalika wafanyabiashara kutoka Ufaransa wawekeze nchini Tanzania kwani ina fursa ya kutengeneza ajira, kuhamisha ujuzi na kujenga uchumi wa viwanda kwa faida ya nchi zote mbili.
“Leo tumefanya mjadala wa kibiashara na sote tumeshuhudia makubaliano yakisainiwa baina ya Tanzania Private Sector Foundation na International Chamber of Commerce (ICC). Makubaliano haya siyo tu mkataba wa kawaida bali ni daraja la kutupeleka kwenye mafanikio makubwa huko mbele,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumatatu, Julai 6, 2026) wakati akizungumza na washiriki wa mjadala wa kibiashara baina ya Tanzania na Ufaransa (Tanzania-France Business Roundtable) uliofanyika kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini Paris, Ufaransa.
“Kwa hiyo ninawahimiza wafanyabiashara wa Ufaransa mtumie vyema fursa hii ya kipekee. Maamuzi yatakayofanywa leo ndiyo yatakayoamua mwelekeo wa sekta za uchumi za kesho kwa nchi zetu. Wale watakaowekeza nchini Tanzania hivi sasa, hawatakuwa tu sehemu ya mageuzi ya uchumi wetu, bali watakuwa washirika wa thamani katika kujenga moja ya uchumi wenye ushindani mkubwa zaidi barani Afrika kwa vizazi vijavyo.”
Dkt. Mwigulu amesema Ufaransa inao utaalamu wa hali ya juu na wa kiwango cha kimataifa katika teknolojia, uhandisi, nishati, miundombinu, viwanda, masuala ya fedha, na huduma za afya.
“Kwa upande wake, Tanzania inao utulivu wa kisiasa, nafasi yake ya kijiografia imekaa kimkakati, inazo rasilimali nyingi za asili, fursa shindani za uwekezaji, usimamizi thabiti wa uchumi pamoja na nguvukazi ya vijana wengi na yenye ari kubwa barani Afrika.”
Amesema maeneo hayo yana nguvu na yanakamilishana kwani katika umoja wake yanajenga fursa za kipekee za kukuza maendeleo endelevu na ustawi wenye manufaa ya pande zote mbili.
“Tunapoanza kwa ujasiri kutekeleza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Serikali yetu itaendelea kuwa thabiti katika kuhakikisha kunakuwepo mazingira yanayotabirika, yenye uwazi na rafiki kwa biashara, ambapo uwekezaji unalindwa, ushirikiano unathaminiwa, na mafanikio yanawanufaisha wadau wote,” amesisitiza.
Waziri Mkuu pia alishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Chama cha Kimataifa cha Biashara cha Ufanransa (ICC) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ambapo Mtendaji Mkuu wa TPSF, Bw. Deo Massawe alibadilishana hati hiyo na Naibu Katibu Mkuu wa ICC, Bw. Julian Kassum.
Mapema, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, aliwaeleza washiriki wa mjadala huo kwamba kitendo kilichofanyika leo kinaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inasisitiza ushiriki wa sekta binafsi kwa asilimia 70 katika kuchochea maendeleo ya uchumi.
Kwa upande wake, Rais wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula alisema Tanzania ipo katika nafasi ya kipekee ya kuwa kitovu cha mageuzi ya uchumi barani Afrika chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kwa miaka mingi, Ufaransa imekuwa mshirika muhimu wa Tanzania katika uwekezaji. Hata hivyo, kwa sasa tunapaswa kuelekeza nguvu zetu katika kujenga ushirikiano wa muda mrefu utakaokuza uhamishaji wa teknolojia, kukuza sekta ya utalii, huduma za kifedha pamoja na uchumi wa kidijitali. TPSF iko tayari kuwezesha ushirikiano huo kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Ufaransa,” alisema.
Baadhi ya kampuni za Ufaransa zilizoshiriki mjadala huo zinajihusisha na usimamizi wa nishati ya jua (ikiwemo mifumo ya taa za barabarani), usafirishaji, maji, nishati, ujenzi, viwanda, mazingira na ufugaji wa viumbe maji (ikiwemo uzalishaji wa mwani wa baharini). Kampuni nyingine ni waendeshaji wa huduma za satelaiti wanaotoa suluhisho bunifu kwa huduma za utangazaji wa sauti na picha, intaneti ya kasi (broadband), huduma za data, usafiri wa baharini na anga. Aidha, kulikuwa na wazalishaji wa mabomba maalumu yanayotumika katika sekta ya mafuta na gesi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde; Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi; Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UNESCO, Balozi Saidi Othman Yakubu; Mtendaji Mkuu wa MEDEF International, Bw. Philippe Gautier; Rais wa Baraza la Biashara la Ufaransa na Afrika Mashariki, Bi. Celine Gouveia; pamoja na wajumbe kutoka sekta binafsi ya Tanzania na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa.
📍Kenya
▪️WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AKUTANA NA RAIS WA IFAD, NAIROBI
▪️Wajadili Kilimo himilivu na uendelezaji wa Kilimo Biashara
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 11, 2026 amekutana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Alvaro Lario, jijini Nairobi, Kenya, ambapo wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika sekta ya kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwigulu amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na IFAD katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo himilivu cha tabianchi, maendeleo ya kilimo biashara, mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya kilimo pamoja na uwezeshaji wa vijana na wanawake kiuchumi.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na IFAD katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kilimo ikiwemo mpango wa kuongeza uzalishaji wa alizeti ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.
“Kimekuwa ni kikao kizuri kwa sababu tumekuwa na ushirikiano nao kwa muda mrefu, ambapo katika kipindi kilichopita tumeshirikiana nao katika miradi mbalimbali, na hasa miradi katika sekta za uzalishaji”.
“Lakini pia tumedhamiria kuendelea kushirikiana katika kuendeleza mazao ya mchanganyiko ambayo katika miaka ya nyuma ilikuwa inachukuliwa kuwa ni mazao ya chakula peke yake, kwasasa mazao haya niya biashara na tunayafanya sehemu ya kukuza biashara ambayo Tanzania inafanya na nchi nyingine”
Ameongeza kuwa Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na IFAD katika sekta ya mifugo na mazao ya baharini kwa upande wa Zanzibar.
“Sambamba na hayo, tunategemea kushirikiana nao katika utekelezaji wa kilimo endelevu ambacho kinasaidia kampeni yetu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi nchi”. Amesisitiza Dkt. Mwigulu
Kwa upande wa Rais wa IFAD Alvaro Lario, amesema kuwa wataendelea kuhakikisha mipango na utekelezaji wa IFAD vinaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2050
“Kwasasa tunasubiri kusikia vipaumbele ya Tanzania ili tujue namna gani tunaweza kusaidia katika maeneo vya utoshelevu na usalama wa chakula pamoja na uongezaji thamani wa mazao”
📍Bungeni,Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano naMazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akizungumza naMbunge wa Jimbo la Katavi Mhe. Thomas Kampala wakati wa kikao cha Bunge bungeni jijini Dodoma leoMei 11, 2026.
📍Tegeta, Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali, Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuph Makamba katika makazi yake Tegeta Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Mei 2026.
📍Kenya
▪️DKT. MWIGULU AWASILI NCHINI KENYA
▪️Kumuwakilisha Rais Dkt. Samia mkutano wa ushirikiano wa Afrika na Ufaransa.
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 10, 2026 amewasili Nairobi, Kenya ambako anatarajia kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit) utakaofanyika Mei 11–12, 2026.
Lengo la mkutano huo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na viwanda.
Aidha, mkutano huo unalenga kukuza uwekezaji mpya kati ya Afrika na kampuni za Ufaransa, kujenga ushirikiano unaotajwa kuwa wa usawa, pamoja na kujadili mageuzi ya mfumo wa fedha na maendeleo endelevu ya Afrika.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unawakutanisha wadau wa maendeleo, wawekezaji pamoja na sekta binafsi, na umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Samoei Ruto, na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Mheshimiwa Emmanuel Macron.
📍Kigoma
▪️Mkandarasi wa Mradi wa Umeme Malagarasi Matatani Baada ya Waziri Kutoridhishwa na Kasi ya Ujenzi
▪️Aagiza Ukaguzi Maalum Kufanyika Kuchunguza Matumizi ya malipo ya awali aliyopewa mkandarasi
▪️Meneja Mradi atakiwa kuondolewa mara moja eneo la mradi mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amesema hajaridhishwa na mwenendo wa mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Megawati 49.5 katika maporomoko ya maji ya mto Malagarasi kutokana na kuchelewa kwa utekelezaji wa kazi pamoja na kushindwa kuendana na masharti ya mkataba kwani amekuwa akitoa visingizio badala ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mkataba.
Mhe. Ndejembi amebainisha hayo Mei 10, 2026 wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa kuzalisha umeme megawati 49.5 katika maporomoko ya mto Malagarasi mkoani Kigoma.
Amesema Serikali imeshamlipa mkandarasi huyo zaidi ya dola milioni 20 kama malipo ya awali lakini kiwango cha kazi iliyofanyika hakiendani na fedha zilizotolewa; Mkandarasi alitakiwa kujenga eneo la makazi ya wafanyakazi pamoja na barabara za mradi lakini hadi sasa hajatekeleza majukumu hayo, jambo linaloashiria uzembe katika utekelezaji wa mradi huo muhimu wa kimkakati.
Aidha, amesema Serikali haitatoa nyongeza ya fedha wala kuruhusu mabadiliko ya gharama za mradi kwani mkandarasi aliwasilisha gharama zake hapo awali; Baadhi ya wakandarasi wamekuwa na tabia ya kuomba kazi kwa gharama ndogo ili wapate zabuni na baadaye kuanza kuomba nyongeza ya fedha, jambo ambalo halitakubalika katika utekelezaji wa mradi huo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Ndejembi ameagiza meneja wa mradi huo kuondolewa mara moja kwa kuwa sehemu ya vikwazo vinavyochelewesha utekelezaji wa kazi huku akiagiza kufanyika kwa ukaguzi maalum wa matumizi ya fedha za malipo ya awali zilizotolewa kwa mkandarasi ili kubaini fedha hizo zimefanya kazi gani na kama hazijaelekezwa katika miradi mingine.
"Mradi huu wa Megawati 49.5 una umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Kigoma, Katavi, Kagera na maeneo ya jirani kwani utaongeza nguvu kwenye gridi ya Taifa na pia utaimarisha upatikanaji wa umeme wa nchini kwani Serikali inataka kuona umeme unapatikana hivyo haitakuwa tayari kuvumilia ucheleweshaji unaosababishwa na wakandarasi wasiozingatia wajibu wao.
Mhe. Ndejembi ametoa muda wa wiki mbili kwa TANESCO kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za awali na taarifa kuwasilishwa kwa hatua zaidi.
Pia amempongeza Mkurugenzi wa TANESCO kwa juhudi za kufanya vikao na mkandarasi huyo huku akieleza kuwa atazungumza na Waziri wa Mambo ya Nje ili kufikisha wasiwasi wa Serikali kwa Balozi wa China kuhusu uwezo wa kampuni hiyo kutekeleza mradi huo.
kwa upande wake Mkurugenzi Myendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange ameeleza kuwa mradi wa kufua umeme wa megawati 49.5 unatekelezwa na Kampuni ya Dangfang Electric International Corporation(DEC) kutoka China ambapo ujenzi wa mradi huo ulianza April 30, 2024 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 30, 2027 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 300 pindi utakapokamilika.
Amesema baadhi ya wakandarasi wamekuwa wakipunguza viwango vya utekelezaji (specification) ili kupunguza gharama na kukidhi matakwa ya zabuni, jambo ambalo limechangia kuchelewa kwa kazi hivyo amesisitiza kuwa tayari wamepokea maelekezo ya Waziri na wanaenda kuyafanyia kazi kwa kuwa mradi huo upo nyuma kwa asilimia kadhaa.
📍Dar es Salaam
▪️DKT. MWIGULU KUMUWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA USHIRIKIANO AFRIKA NA UFARANSA, NCHINI KENYA
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 10, 2026 ameondoka nchini kuelekea Nairobi, Kenya ambako anatarajia kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit) utakaofanyika Mei 11–12, 2026.
Lengo la mkutano huo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na viwanda.
Aidha, mkutano huo unalenga kukuza uwekezaji mpya kati ya Afrika na kampuni za Ufaransa, kujenga ushirikiano unaotajwa kuwa wa usawa, pamoja na kujadili mageuzi ya mfumo wa fedha na maendeleo endelevu ya Afrika.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unawakutanisha wadau wa maendeleo, wawekezaji pamoja na sekta binafsi, na umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Samoei Ruto, na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Mheshimiwa Emmanuel Macron.
📍Ngara, Kagera
Taswira mbalimbali za Waziri wa Nishati Mhe, Deo Ndejembi akiteta jambo na Mkurungenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Nchini -TANESCO Bw. Lazaro Twange kwenye hafla ya uwekwaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka pamoja na ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Benaco, mradi unatarajiwa kuunganisha Mkoa wa Kagera katika Gridi ya Taifa.
📍Ngara, Kagera
▪️Serikali yaanza utekelezaji wa mradi wa umeme kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa
▪️Waziri Ndejembi aweka jiwe la msingi la njia ya kusafirisha umeme Kyaka - Benaco
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka pamoja na kituo cha kupoza umeme cha Benaco, ambao utaunganisha Mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa, hatua itakayomaliza changamoto ya kukatika kwa umeme katika wilaya za mkoa huo.
Waziri Ndejembi ameweka jiwe la msingi la leo tarehe 9 Mei 2026 wilayani Ngara mkoani Kagera, ambapo amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuukamilisha ndani ya miezi 24 kama mkataba unavyoelekeza.
“Tunachotarajia ni kuona ndani ya miezi 24 Mkoa wa Kagera umeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na changamoto za umeme zilizowasolishwa na Mhe. Mbunge wa Ngara ziwe historia kwa wananchi hawa,” amesema Ndejembi.
Akizungumza na wananchi, Waziri Ndejembi amesema kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Benaco hadi Kyaka unalenga kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika wakati wote.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu umekuwa ukitegemea umeme kutoka nchi jirani, hivyo kupitia mradi huo Mkoa wa Kagera utaunganishwa moja kwa moja na Gridi ya Taifa, hatua itakayoongeza uhakika wa nishati na kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii.
Aidha, Waziri Ndejembi amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati na kueleza kuwa Wizara itaendelea kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote.
Katika hatua nyingine, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja inapatikana transfoma yenye uwezo mkubwa pamoja na kuendelea kufanya marekebisho katika njia za kusafirishia umeme ili kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Ngara wanapata umeme wa uhakika katika kipindi wanachosubiri mradi huo ukamilike.
“Wananchi wa Ngara wanataka kupata umeme wa uhakika ambao haukatikikatiki, sasa nikuagize Mkurugenzi wa TANESCO na timu yako kuhakikisha tunapata transfoma mpya mara moja yenye uwezo mkubwa ya kuhakikisha tunapata umeme katika Wilaya ya Ngara, nakupatia mwezi mmoja,” amesema Ndejembi.
Ameongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kuongeza ajira, kuhamasisha uwekezaji na kukuza shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji pamoja na uendelezaji wa viwanda katika ukanda wa ziwa, kwani ni fursa muhimu kwa wananchi wa Kagera na mikoa jirani.
Waziri Ndejembi ameziagiza TANESCO na mkandarasi kutoa fursa za kazi kwa wananchi wa maeneo yanakotekelezwa mradi katika wilaya za Ngara, Karagwe na Missenyi ili waweze kuwa sehemu ya mradi huo na kujiinua kiuchumi na kibiashara.