#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 301
Mhe. Lissu anaendelea na Re-examination
Mhe. Lissu: Kuhusu D1 kile kielelezo cha Kaaya kule chini kabisa kimeendikwa maelezo, ziko hizo sehemu kwahiyo alipaswa kuandika na kuandikwa maelezo.
D2 nacho pia hicho kielelezo Samwel Elibariki nacho niliulizwa maswali kadhaa angalia mwisho utaona. Ipo sehemu ya mtoa maelezo na afisa aliyeandika maelezo, hizo sehemu zote zimesainiwa na mtu mmoja.
D5 ambayo ni maelezo ya PW 6 nayo pia kuna signature moja imepita sehemu zote za aliyeandika maelezo na aliyemuandika maelezo kote ni yule yule.
Exhibit D8 ni maelezo ya PW9 nae pia vilevile. Kuna uthibitisho wa Afisa aliyeandikiwa maelezo. Uthibitisho pia wa chini yake ameandika vile vile yeye pia. Amejionya na kujithibitisha mara mbili.
D11 maelezo ya PW12 inasema Koplo Vicent nae pia alijionya na kujiandika Maelezo yake. Mtu huyo huyo.
D15 ambayo ni maelezo ya Amin Mahamba PW 16 kila page kuna mtoa maelezo na aliyeandika maelezo. Lakini imesainiwa mtoa maelezo pekee lakini aliyeandika maelezo haipo kabisa.
D14 cha PW 15 Koplo Amani kwenye kila page saini ya mtoa maelezo imejazwa na afisa aliyesimamia maelezo ipo Koplo Robert. Ndo nilisema huyu pekee ndio alifuata utaratibu. Detective Corporal Robert ndio niliandika maelezo ya Detective Coporal Amani. Huyu alikuwa sahihi.
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu wale mashahidi waliokiri kufanya uhalifu. Walikiri Polisi na baadae wakaambiwa wawe mashahidi dhidi yangu na baadae tuhuma zikafutwa. Je unawaita wahalifu walishapelekwa mahakamani hapana lakini ni wahalifu. Ufafanuzi ni kwamba watu ambao ni wamepanga kufanya uhalifu, wakakamatwa kwa kufanya uhalifu, wakakiri wanapanga kufanya uhalifu wakaja mahakamani tumepanga kufanya uhalifu na wakaachiliwa hao ni wahalifu.
Ajuaye: Ameanza kutoa ushahidi hapa tena.
Mhe, Lissu: Nimetoa ufafanuzi Jaji
Jaji Ndunguru: Haya tuendelee hebu
😂😂 Ni kama Jaji amesema bila kusema kuwa AJUAYE WEWE NI KILAZA. Kwa Maneno Mengine Jaji anasema AJUAYE NI KATUGA ambae hana maelezo mengi lakini ujinga ni ule ule.
Mhe. Lissu: Naomba niishie hapo. Kwenye hii re examination.
Kesi imeahirishwa hadi saa nane kamili tutarudi Mahakamani.
Kuendelea na Shahidi John Mnyika. DW2.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 300
Mhe. Lissu anaendelea na Re-examination
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu Ndyanabo na Mtikila na nikasema Mtikila alienda Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika na hadi sasa serikali haijatekeleza maamuzi ya Mahakama ya Haki za Binadamu za Afrika.
Jaji Ndunguru: Hiyo naona ni the obvious nayo usifafanue kabisa.
Mhe. Lissu: Haina shida. Niliulizwa sana kuhusiana na scope ya kifungu cha 39(2)(d) juu ya neno Or kati ya Overt act or deed. Ufafanuzi wangu ni kwamba act or deed is the same thing. Act something that is done and a deed is something is done.
Katuga: Huu ni ushahidi au submission. Anakoenda ni kutoa tafsiri ya overt act or deed.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naona Mahakama inisomeee ili tusivutane vutane hapa.
Jaji Karemaha anasoma kilichoandikwa, anasema kwa vile nimeandika kingereza nitasoma.
Mhe. Lissu: Basi naomba niendelee. Kuhusu mihimili mitatu na kazi zake. Nikasema moja ya kazi za Bunge ni kutunga Sheria na serikali kusimamia sheria. Ufafanuzi wangu ni kwamba kutunga sheria sio kazi pekee ya Bunge.
Mhe. Lissu: Kuhusu mashahidi wa mashitaka hawakuja kutoa ushahidi kuhusu namna nilivyokamatwa. Uhalali wa kukamatwa kwangu ni suala tofauti kwasababu sheria zimeweka utaratibu wa namna ya kukamata na ulifuatwa au laaa suala hilo lilipaswa kujibiwa na upande wa mashitaka.
Mhe. Lissu: Nimeulizwa kuhusu waandishi wengi wa habari waliokuja Tar. 03/04 niliulizwa kama waandishi hao walikuwa wanajua nilichokuwa naenda kuwaambia na kama niliwapa hotuba yangu mapema. Nikasema sikuwapa. Nataka kufafanua, waandishi wa habari huwa hawapewi taarifa hizo kabla.
Katuga: Hilo la kwamba huwa hawapewi hizi taarifa hilo sikuuliza.
Mhe. Lissu: Yeye ndo alileta habari za constructive publication
Jaji Ndunguru: Na wewe ukasema kuwa hukuwa na control ya hao watu, nafikiri hata hili majibu yako yalinyooka tu.
Mhe. Lissu: Sawa. Kuhusu maandamano na kuzuia uchaguzi. Nilisema uchaguzi usiokuwa huru sio uchaguzi.
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu adhabu ya kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code atahukumiwa adhabu ya kifo na Wakili akasema sentenced to death. Mimi nilisisitiza ni adhabu ya kifo.
Jaji Ndunguru: Hivyo vifungu vinatofautiana cha mwaka 2022 na cha mwaka 2023. Kuna sheria moja ina liable to death na nyingi shall be sentenced to death. Kwahiyo ile ya 2022 ni kwamba sio lazima upewe adhabu ya kifo lakini ya 2023 ndio haina hiyo option. Inasema direct sentenced to death.
Mhe. Lissu: Haya tuendelee. Kulikuwa na maswali kuhusiana na mashahidi wa kificho na nasisitiza hawakuwa wanajulikana kwa mtu yeyote isipokuwa aliyewaleta.
Kuna hili lingine la kwamba tuliwatoa nje waandishi na nikasema kwa yale ambayo hatukutaka yachapishwe tuliwatoa ni kwasababu walichoitiwa kilikuwa kimeshakamilika.
Naomba sasa vielelezo D1 hadi D16 kwasababu vilitumika sana kwenye cross examination.
Anasubiria kupatiwa.
Part 301 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 299
Jaji Ndunguru anamwambia Mhe. Lissu, sasa hayo uliyosema si ndio mwongozo tunapaswa kumpa?
Mhe, Lissu anasema tutafika tumechoka sana kama mwongozo wenyewe mnaopaswa kuutoa ni huo kila mara.
Yeye mwenyewe wakati anaomba ni kama alikuwa hajielewi anaomba nini hana uhakika kabisa.
Jaji anateta na wenzake kwa dakika kadhaa hapa. Sijui wanateta nini? Hizi kazi ni ngumu sana.
Wazee sio bure watakuwa na presha nyingi. Jambo tunaloona ni dogo wameshajadili karibu dakika 10 hadi sasa. 😂😂
Mhe. Lissu Mungu ambariki tu, Imagine kikundi cha Mawakili 10 wa Serikali yeye yuko peke yake pale kizimbani lakini wanateseka kiasi hiki🙌.
Majaji wako watatu nao wanashauriana dakika za kutosha, hili linatuma ujumbe mkubwa sana. Ngoja tuone.
Jaji Ndunguru anawasha MIC sasa pamoja na kwamba umesema kuwa umejibu na suala hili ni dogo lakini Mahakama ni muhimu ikatolea muongozo hili.
Sasa suala ni scope ya hiyo re examination. Sasa tutajikita kwenye scope hiyo na kama kutakuwa na new matters basi serikali wazuie au wataomba kukuuliza maswali. Mahakama pia ina nafasi ya kuuliza na hatuwezi kuzuia Re-Examination. Kazi yetu tunaijua vizuri.
Mhe. Lissu anasema naomba wasaidizi wangu wanipatie swali la mwisho lililoulizwa.
Anapatiwa sasa.
NB: Kwa kifupi walichoamua Majaji ni kwamba kwa maneno mengine wamesema KATUGA ni KILAZA na Jina KATUGA linapaswa kuanza kutumika kumuelezea MWANASHERIA yeyote ambae ni KILAZA basi aitwe KATUGA.
Majaji wanapiga story na kuangalia kompyuta zao sijui kuna nini tena, Mhe. Lissu hajaanza bado re examination.
Anasimama Ajuaye Zengeli anasema Waheshimiwa Majaji naona utaratibu unakiukwa. Shahidi anaomba washauri wake wampe sio utaratibu.
Mhe. Lissu: Kwamba naulizwa maswali lazima niwe naandika na kujibu hapo hapo inawezekana? Hili nalo lina shida kweli mimi kuandikiwa? Watu wameandika maswali na majibu hawa vijana wangu shida iko wapi? Mapingamizi ya bure kabisa.
Jaji Ndunguru: Basi endelea.
Mhe.!Lissu: Niliulizwa kuhusu nia inathibitishwa kwa matendo, nikasema sio kweli. Ufafanuzi wangu ni kwamba sio kila nia inathibitishwa kwa matendo. Nyingine ni kuchapisha.
Jaji Ndunguru: Tuendelee
Mhe. Lissu: Aliniuliza kuhusu Mahakama kutokulazimishwa au haipangiwi na baraza la umoja wa Mataifa. Ufafanuzi wangu ni kwamba Mahakama mapendekezo au maoni hayo ya vyombo vingine ni muhimu pia kuzingatia ushauri wa hizo taasisi zingine.
Katuga: Mambo ya Umuhimu asiyalete.
Mhe. Lissu: Basi niseme Mahakama huwa inaangalia maamuzi ya vyombo vingine.
Katuga: Mimi sitaki aende huko. Asililete sasa hivi.
Kwa kifupi Bwana Katuga kwa sasa ameamua kutupotezea muda humu ndani ilimradi tu.😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu tuzo na kwamba nimezileta nikasema sijazileta na ni legal principles na kwamba mimi sio mwenye wajibu wa kuthibitisha sina hatia bali mzigo wa uthibitishaji uko upande wa mashitaka. Iko hivyo.
Hiyo naona imeingia. Hawajasimama akina KITUGA.
Mhe. Lissu: Niliulizwa vilevile kwamba niliwahi kuwa Rais wa TLS na nikajibu kweli na nikaulizwa wakati unashitakiwa na kesi hii ulikuwa Rais wa TLS na je kunakupa kinga.
Jaji Ndunguru: Naona hilo ni obvious hata usilitoleee ufafanuzi.
Mhe. Lissu: Sawa basi kuna swali la njia za Kidemokrasia nilisema ipo ya Mahakama na maandamano ya kidemokrasia. Nikaulizwa ipo kwenye kifungu gani cha Katiba nikasema kifungu cha 20(1) Cha Katiba. Naomba kutoa ufafanuzi kuwa hizo njia za nje ya mahakama zinatambulika kikatiba na zimethibitishwa hivyo na Mahakama
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 28, 2026
Last time tuliishia part 297 so leo tunaendelea na -;
Part 298
Saa nne kasoro robo Mhe. Lissu anaingia na wananchi wanapiga makofi kwa pamoja.
Hii ni style mpya leo ya kumkaribisha hapa Ukumbi Na. 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Inapigwa Courtttttt harakaharaka na Jaji Karyemaha ametangulia kwa kasi sana.
Anafuatia Jaji Ndunguru na Mzee wa Burudani Jaji Kiwonde yuko nyuma yao.
Wanaingia wanakaaa.
Mwenyekiti Lissu nae anatafuta Vitabu vyake.
Karani anasoma namba ya kesi na kukaaa.
Anasimama Ajuaye Zengeli anasema anasaidia na Katuga, Mrema, Thawabu, Cathbert na Winniwa Kasawa wote ni Mawakili wa Serikali.
Na shauri limekuja kwa mshitakiwa kuulizwa maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu : Niko tayari kuendelea.
Mhe. Lissu anaomba niongee na Mawakili wangu kwanza, anaenda pale Dr. Nshala, Mahinyila, Nashon Nkungu, Dorice Kafuku,
Ajuaye: Nia ya kutenda kosa inathibitishwa na tendo?
Mhe. Lissu: Sio kweli
Ajuaye: Waheshimiwa tulikuwa na swali moja kwa shahidi na tumemaliza maswali ya Dodoso kwa shahidi huyu.
Huyu Ajuaye ni kilaza sana, ameuliza swali moja na amesema amemaliza kabisa.
Majaji wanaandika na Mheshimiwa Lissu anapanga makabrasha yake hapa.
Mhe. Lissu anaomba kufanya re-examination baada ya kuwa wamemaliza kufanya cross examination.
Anasimama Katuga kuwa naomba tutoe hoja anasema Re examination ni moja ya examination ya utoaji ushahidi. Kifungu cha 155 Sura ya 6/2023.
Kifungu cha 156(3) cha Sheria ya Ushahidi kinasema Re-Examination itafanyika kwenye mambo gani na utaratibu wa kufuata.
Nimerejea kwenye hivyo vifungu ili tupate tafsiri kuwa yale maswali aliyoulizwa ndio tutaita re examination. Alikataa uwakilisha yeye mwenyewe ni jinsi gani atajifanyia maswali ya ufafanuzi kutokana na majibu yake. Lengo ni kutoa ufafanuzi.
Waheshimiwa Majaji tunaomba mahakama ijiulize. Majibu shahidi katoa mwenyewe, na kujiuliza anajiulizaje mwenyewe.
Huwezi kuwa Jaji kwenye kesi yako. Principle zetu za kisheria ziko hivyo. Unajuaje wengine hawajakuelewa hadi utake kutoa ufafanuzi.
Haya maswali ya re-exanination yanaulizwa na nani? Hili eneo ni gumu na muangalie vifungu vya Sheria unless tutakuwa tunafungua uwanda mwingine wa ku introduce inshu mpya.
Ili kuepuka hili la usijijibu wewe na ukajiuliza wewe. Mahakama inaweza kumuuliza yenyewe. Hiyo right ya re-examination iko kwa party iliyomuita shahidi.
Jaji Ndunguru: Sasa ombi lako ni nini?
Katuga: Mahakama kama itataka kumuuliza imuulize yenyewe lakini pia imuelekeze shahidi nini cha kujibu na naomba Mahakama itoe maelekezo kwenye eneo hilo. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru: Anateta na wenzake. Naona wanachungulia PC kwenye ile ya Karyemaha. Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu: Naomba Wakili wa Serikali aiambie Mahakama kama ameleta pingamizi aseme au ameleta mapendekezo na maelekezo kwa Mahakama.
Amesema anawapa ushauri kama ni ushauri tuachane nao tufanye kazi iliyotuleta na kama ni pingamizi basi nitamjibu.
Jaji Ndunguru: mnasemaje serikali
Katuga: Labda kama alikuwa hasikilizi, mimi naomba mwongozo wa Mahakama.
Mhe. Lissu: Hakunaga kuomba mwongozo Mahakamani lakini basi ngoja nijibu huo mwongozo.
1. Re examination ni haki ya shahidi aliyekuwa examined ndo maana kifungu cha 156(1) alichotaja ni haki ya re-examination ni haki yangu basi Wakili wa Serikali alipaswa kunyamaza kimya.
2. Anasema Atajiongozaje kama hana Wakili. The fact kwamba shahidi kwamba ndo mshitakiwa haimuondolei haki ya kufanya re exanination. Sasa nitafanyaje? Nitarejea maswali niliyoulizwa nitasema majibu yangu na nitaweka ufafanuzi wangu hapo.
3. Hii inaweza kuwa ni fursa ya ku introduce new facts huwa wana rise objection kwahiyo hofu yake ni unfounded completely. Ni hofu ya bure kabisa.
4. Hamna mwongozo wa kutoa hapa na kesi ndio zinaendeshwa hivyo.
Part 299 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
"Hakuna ugonjwa ambao hauponi dunia hii,kua makini sana na unachokula au unachokunywa" Dr Sebi
Dr Sebi mwamba kabisa aliekua anatibu magonjwa yote anauliza kwanini unakula wanga? kwa nini unakula ugali,wali,mihogo? kwa taarifa yako hawa mbuzi wa sasa ,kondoo wa sasa ,ng’ombe wa sasa,kuku wa sasa hawakuletwa na Mungu Africa,vimetengenezwa maabara yaani vina mkono wa mtu
Usisahau ⚠️ kupima 🧪 H. Pylori 🦠,FIGO,dundumio 🦋,mafuta 🩸,sukari 🍬,brusela 🧫. Haya matatizo 😷 ni balaa jipya 🚨 mjini ⚠️.
#doktamathew 🩺 #fyp 🎥 #highlights ✨ #viral 🚀🔥 See less
Job Mrema; moja ya statement ulitoa ni kwamba majaji ni CCM na mahakamani hakuendeki, ilikuwa inakiuka kifungu cha 51(1)
Tundu Lissu; waheshimiwa majaji sikubaliani na yeye
Job Mrema; utakubaliana na mimi kwamba Mahakama ikishatoa Maamuzi yake inatakiwa kufuatwa?
Tundu Lissu: ni sahihi
Job Mrema; ni sahihi kwamba Mahakama kuu ilishawahi kutoa amri ya ulinzi wa mashahidi?
Tundu Lissu; ndiyo
Job Mrema; ni sahihi kwamba shauri lililo amriwa na kutoa ulinzi wa mashahidi ni tofauti na shauri hili lililopo mbele sasa hivi?
Tundu Lissu; ni sahihi
Job Mrema; ni sahihi kwamba kupitia uamuzi huo wa ulinzi wa mashahidi haijawahi kufanyiwa uamuzi wa kuondolewa
Tundu Lissu; ni sahihi
Job Mrema; kama hukufurahiswa na uamuzi huo si ungeweza kuchukua hatua?
Tundu Lissu; nilichukua hatua ndiyo maana nikaja kuwaambia majaji hapa kwamba kinachofanyika hapa ni tofauti na amri ya Jaji Mtemwa
Job Mrema; sijauliza utekelezaji wa amri. Nauliza kwamba hukuchukua hatua juu ya amri ya mahakama yenyewe
Tundu Lissu; siku chukua hatua kwa sababu nipo gerezani
Job Mrema; kwenye maelezo yako umeieleza Mahakama umekuwa mwanaharakati kwa muda fulani na ukataja baadhi ya Polisi kwamba ukasema kuna sehemu walisema maliza huyu?
Tundu Lissu; utakuwa umesikia vibaya
Job Mrema; wewe ni mwanasheria kwamba unajua kama ukiwa na malalamiko unatakiwa kutoa taarifa Polisi
Tundu Lissu; Unatoa taarifa polisi kama Polisi siyo wahusika wenyewe. Nimesema nimekuwa nikikamatwa kwa kufanyiwa vitisho na Polisi wenyewe. Nikalalamike kwao?
Job Mrema; naomba usome kifungu cha 10 cha sheria na subsection 2
Tundu Lissu: nakielewa kwamba taarifa za kufanyika kwa kosa la jinai inaweza kutolewa kwa mdomo au kwa maandishi kwa afisa wa eneo husika wa mamlaka
Job Mrema; katika eneo husika unalolalamikia ulipeleka malalamiko?
Tundu Lissu: sikupeleka kwa sababu nilikuwa nusu mfu, nilipelekwa Nairobi nikiwa sijitambui. Kwa hiyo sikuwepo. Nilikuwa Nairobi napigania uhai wangu. Nilipo rudi nilikwenda kwa RPC Muroto kwamba nimerudi nichukueni maelezo wakakataa. Nikawaambia nipeni gari langu, nikachukua gari lakini hawakuchukua maelezo yangu.
Job Mrema; Ndugu shahidi kama nilikusikia vizuri wakati unaanza kutoa ushahidi wako, ulieleza Mahakama hii kuwa umewahi kushitakiwa maeneo tofauti. Sasa utakubaliana na mimi kwamba hujaeleza hujashtakiwa kwa kesi gani, kesi namba ngapi?
Tundu Lissu; Sikubaliani na wewe nilisema kesi gani na mahala ni Kisutu, Tarime, Arusha kasoro kesi namba tu
Job Mrema: Wakati unatoa utetezi wako kama nimekusikia vizuri ulieleza Mahakama hii huwezi kuwa Rais wa TLS kama ni mtu wa ovyo ovyo. Sasa wakati unashtakiwa kwa mara ya kwanza ulikuwa Rais wa TLS?
Tundu Lissu; Nilishajibu kwamba nilishatoka tangu 2017, nilitumikia miezi mitano nikapigwa risasi.
Job Mrema; Baada ya kutoka katika Urais wa TLS ndiyo ukawa mtu ovyo?
Tundu Lissu; Sijawahi kuwa mtu wa ovyo kwa sababu nimetambuliwa kikanda na kuheshimika na Jumuiya za kimataifa
Job Mrema; Baada ya Mahakama kukukuta na kesi ya kujibu umeanza kuwa mtu wa ovyo ovyo?
Tundu Lissu; Mimi siyo mtu wa ovyo ovyo ndiyo maana jumuiya za kitaifa na kimataifa zinanitambua na kunipa heshima kila siku. Mahakama ni kwamba imesema inataka kunisikia tu
Job Mrema; Wakati unajitetea ulieleza kesi hii ya kisiasa. Je umeshitakiwa kama Tundu Antipas Lissu au mwanasiasa
Tundu Lissu; Nimeshtakiwa kama Tundu Antipas Lissu Mwanasiasa. Nisingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA
Job Mrema; Kwa mujibu wa hati ya mashtaka kuna sehemu yeyote umeshtakiwa kama mwanasiasa?
Tundu Lissu; Hati ya mashtaka haisemi hivyo lakini mashahidi wote wanamtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Mkutano wa CHADEMA na wakati wa preliminary hearing wamesema ni Mwenyekiti wa CHADEMA.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 297
Ajuaye: Ulitoa taarifa sasa wewe polisi?
Mhe. Lissu: Ilikuwa ni miezi sita kabla ya uchaguzi. Natoaje taarifa polisi wakati siku kwenye mkutano wa kampeni na nilishakwambia sikuwa nafanya public meeting.
Ajuaye: Soma kifungu cha 23 cha Political parties act
Mhe. Lissu: Soma wewe uliza swali.
Ajuaye: anakisoma je ulitoa taarifa
Mhe. Lissu: Siwezi kutoa taarifa mikutano ya ndani. NEXT?
Ajuaye: Kifungu kinasema public place or any other area
Mhe. Lissu: Hujui wewe hata kusoma kingereza kifungu kinasema public meeting conducted at any area. Sasa wewe umesoma shule gani Dada angu?
Ajuaye: Tulia kwanza. Una kifungu chochote kinachosema unaweza kufanya mkutano wa ndani bila kibali?
Mhe. Lissu: Hicho hicho kifungu cha 23 cha Sheria ya Vyama vya siasa.
Ajuaye: Maneno ya kukinukisha uliyakubali hata kama video hatujaleta?
Mhe. Lissu: Sikuongea maneno ya Uhaini mimi.
Ajuaye: Ni ukweli kwamba hata kama video haikuletwa lakini uliongea maneno ambayo yapo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Maneno niliyoshitakiwa kwamba yalikuwepo kwenye video yalikuwa ya masaa matatu hayakuwa ya uhaini.
Ajuaye: Video ni kifaa kilichobeba maandishi?
Mhe. Lissu: Kumbe iko hivyo? Mimi sijui.
Ajuaye: subiri nikiwa mshitakiwa au shahidi utaniuliza. Nitakuomba uwe Wakili wangu?
Mhe. Lissu: Siwezi kuwa na mteja kama wewe ambae anasingizia singizia watu makosa.
Ajuaye: ni kweli mahakama ndio inaweza kusema mtu fulani amefanya kosa fulani?
Mhe. Lissu: Itasema kama mtu huyu atakuwa amepelekwa mahakamani.
Ajuaye: Nani anasema walikamatwa kwasababu walikuwa na makosa?
Mhe, Lissu: Walikamatwa bila kuwa na makosa.
Ajuaye: Ulisema kama ukamataji wako ulikosewa?
Mhe. Lissu: Nilisema na Kiswaga aligoma kuandika na hapa nilisema kwenye mahakama hii.
Ajuaye: Ni very serious allegation hizo
Mhe. Lissu: Ndio ndio maana nilileta mahakamani na wewe ulikuwepo siku ile. Uliona.
Ajuaye: Wanaosimamia sheria ya uchaguzi ni serikali?
Mhe. Lissu: Sheria ya Uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Na tume ya Uchaguzi sio Serikali.
NB. Leo nimeshuhudia ni kwa kiwango gani TAIFA lina Mawakili wa Serikali ni VILAZA.
Ajuaye: Kupinga uchaguzi ni takwa la kisheria?
Mhe. Lissu: Sisi tulikuwa tunataka uchaguzi usifanyike kabisa. Mambo ya kupinga hata kwenye uchaguzi halali kuna kupinga matokeo ya uchaguzi.
Anakuja askari wa Magereza huwa ni mnaa mnaa sana. Mnoko sana. Amewafuata mawakili wa serikali kwasababu imefika saa 11 na nusu kwa sasa.
Wanajadili mawakili wa Serikali muda huu.
Mhe. Lissu: Ule utaratibu wa kuishia saa 11 kamili vipi tumeubadilisha.
Jaji Ndunguru: Tulidhani wanamaliza maswali yao ndio maana tukawa tunawaangalia tu. Sasa ngoja tuwaulize. Upande wa serikali mnasemaje?
Ajuaye: Basi tuahirishe hadi kesho.
Jaji Ndunguru anateta na wenzake.
Sasa tukutane kesho asubuhi kuendelea.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 296
Wakili wa Serikali Job Mrema: Kama kuna mgogoro si unatakiwa kwenda Mahakamani?
Mhe. Lissu: Ukiwa ni mgogoro wa kiimani unaenda kanisani na msikitini kutatua. Yakisheria ndio unaenda Mahakamani.
Job Mrema: Unakubaliana na mimi kuwa ulisema majaji hawatendi haki?
Mhe. Lissu: Hilo sio geni amelisema jaji Nyalali, Tume ya Warioba imesema. Hata na kikosi kazi pia kimesema. Hakuna jipya hapo.
Job Mrema: Ulisema Majaji ni Ma CCM na Huko Mahakamani hakuendeki?
Mhe. Lissu: Ndio.
Job Mrema: Kupandikiza wananchi chuki katika mfumo wa utoaji haki ni kosa? This is general question.
Mhe. Lissu: hiyo chuki maana yake nini sasa? Niambie kwanza.
Job Mrema: Kifungu cha 52 cha Media service Act. Kinasemaje na unakionaje?
Mhe. Lissu: Kama ukisababisha chuki, dharau au kutokuridhika na mfumo wa utoaji haki ni nia ya kichochezi.
Job Mrema: ukiwa na nia unakiuka kifungu hicho
Mhe. Lissu: Kwa maana ya kifungu cha 52(2) hukiuki lakini 51(1) C ni sawa.
Job Mrema: Kuhusu Majaji ni ma ccm na mahakamani hakuendeki hiyo statement inakiuka kifungu cha 52(1)
Mhe. Lissu: Sikubaliani na wewe kabisa.
Job Mrema: Kulikuwa na amri ya kuficha mashahidi?
Mhe. Lissu: Ndio
Job Mrema: Hukuchukua hatua.
Mhe. Lissu: Niko gerezani unataka nichukue hatua gani?
Job Mrema: Unawakumbuka mashahidi wa siri?
Mhe. Lissu: Nawakumbukaje wakati nimekwambia siwafahamu? Unawafahamu wewe. Majaji na mimi.
Job Mrema: Ni sahihi kwamba uamuzi wa mashahidi wa vificho hauwezi kuzungumziwa kwenye kesi hii?
Mhe. Lissu: ingekuwa haiwezekani hivyo vizimba hapo visingefumuliwa kipindi kile. Kwani nilipinga kwenye kesi gani ya Bibi yako?
Jaji: Haya tuendelee swali lingine.
Job Mrema: Mheshimiwa tunaendelea.
Jaji Ndunguru: Sasa nyie si mpo wengi hapo Mawakili wa Serikali mwingine aingie haraka aanze kuuliza wakati huyu anatafuta maswali yake.
Watu wanacheka😂😂
Job Mrema: Uliwasilisha chochote kuhusu kupigwa Tar. 11/08/2024 kule Mbeya?
Mhe. Lissu: Nimesema kwa mdomo na ndio maana niliapa kabla ya kutoa ushahidi.
Job mrema: Tar. 23/09/2024 ulivamiwa nyumbani kwako na polisi na hakuna ushahidi wowote ulioleta?
Mhe. Lissu: Nilisema nivamiwa na kukamatwa wakanipeleka mbweni na usiku walinirudisha nyumbani. Ulitaka nilete nini kwenye hayo maneno?
Job Mrema: Ulisema watu 466 ulisema case no zao wale wa Tarime.
Mhe. Lissu: Sikueleza.
Job Mrema: PW1 ulisema alifungua jalada tarehe 04 April
Mhe. Lissu: Nilivyosema mimi au PW 1 mwenyewe ndio alisema.
Job Mrema: PW 1 Kwahiyo umesema ilikuwa ni lazima amwambie DPP kuhusu mashitaka haya?
Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 16 na 24 cha National Prosecution Act kinasema makosa ya jinai ni DPP ndio anapaswa ku coordinate ushahidi. Sasa yeye hakufanya hivyo. Hakuwahi kumpa taarifa na alisema hivyo.
Job Mrema: Ni chombo kipi kimepewa mamlaka ya huyu ana hatia na huyu hana hatia?
Mhe. Lissu: Ilikuwaje nyie polisi mseme huyu ni mkosaji wa uhaini hata kabla ya ushauri wa DPP?
Job Mrema: Sasa kama mashitaka yalikosewa unafanya nini?
Mhe. Lissu: Najitetea kwa makosa ya kubambikizwa.
Job Mrema: Mahakama hii imetoa uamuzi kuhusiana na makosa yako?
Mhe. Lissu: Haijatoa.
Job Mrema. Amerudi kwa wenzake wanaongea kama dakika tano hivi. Jaji Ndunguru anawaangalia kwa hasira sana.
Anasimama anasema naomba kuishia hapa nimkaribishe Ajuaye Zengeli.
Ajuaye: Ni sahihi kwamba wakati mnafanya mkutano huo hamkuwa na kibali chochote?
Mhe, Lissu: Hakuna mkutano wa ndani unahitaji kibali. Pia hakuna mkutano wowote wa vyama vya siasa unahitaji kibali unatakiwa kutoa taarifa tu.
Ameingia kilaza mwingine huyu Ajuaye.🚮
Ajuaye: PGO 403
Mhe. Lissu: Soma wewe inasemaje nikujibu swali.
Ajuaye: Basi soma PGO 402
Mhe. Lissu: Inahusu mikutano ya kampeni
Watu wanacheka😂
Ajuaye: Umekielewaje?
Mhe. Lissu: Mambo ya uchaguzi na taratibu za kampeni za uchaguzi
Part 297 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 295
Katuga: Naomba niishie hapa nisiulize maswali mengine niishie hapa. Niwaachie wenzangu.
Anasimama Job Mrema. Nae kuuliza maswali.
Job Mrema: wewe ni mwanaharakati ulisema?
Mhe. Lissu: Ndio
Job: Ulianza lini?
Mhe. Lissu: Nilisema habari za nilipokuwa sekondari, jeshini na kadhalika nilielezea.
Job: Uwanaharakati ni nini?
Mhe. Lissu: Uanaharakati ni mtu anayefanya jitihada za kupigania jambo au mambo fulani.
Job: Wewe pia ni mwanasheria?
Mhe. Lissu: Ndio
Job: Huu uanaharakati unatambulika kwa mujibu wa sheria za nchi?
Mhe. Lissu: Ndio
Job: kifungu gani?
Mhe. Lissu: Kuanzia ibara ya 12 hadi 29 ya Katiba vinatoa uwanja mpana wa kufanya jitihada za kupigania mambo mbalimbali.
Job: sasa ibara ya ngapi imesema harakati ni nini?
Mhe. Lissu: Hujielewi wewe. Nimeshakwambia hizo ibara zinasema watu ni huru, ukipigania uhuru wa watu maana yake unafanya harakati. Katiba inasema haki ya Uhai na kuishi ukipigania kupinga adhabu ya kifo maana yake unafanya harakati za kupigania haki ya kuishi.
Huyu Job Mrema yeye huwa ni kilaza wa aina yake.
Job Mrema: Ni sahihi maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka na walioyasikia waliyatafsiri kadri yalivyo?
Mhe. Lissu: Hawakutafsiri kadri yalivyo.
Job Mrema: Hakuna mahali popote kwa sheria za nchi hairuhusiwi watu kujichukulia sheria mkononi?
Mhe. Lissu: Hakuna sheria inayoruhusu watu kuvunja sheria. Kuhusu Sheria za Uchaguzi nasema kwamba uchaguzi usio huru na haki basi ni haki yao wananchi kuuzuia.
Job: Ukiwa mwanaharakati una kinga ya kufuata sheria?
Mhe. Lissu: Nilishajibu hauna kinga. Kama huna maswali ukakae.
Job: Ukiwa mwanasiasa je?
Mhe. Lissu: Huna kinga.
Job: Ulisema kesi hii ya kisiasa. Je wewe umeshitakiwa kama Tundu Lissu au mwanasiasa.
Mhe. Lissu: Nimeshitakiwa kama Tundu Lissu ambae ni mwanasiasa. Nisingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA nisingekuwa hapa.
Job Mrema: Kwa mujibu wa hati ya mashitaka kuna mahali wamesema wewe ni mwanasiasa?
Mhe. Lissu: Mashahidi wote wanasema mimi ni Mwenyekiti wa CHADEMA. PH imesema mimi ni Mwenyekiti wa Chadema. Kwahiyo hati haisemi lakini huko kwingine kote ni Mwenyekiti wa Chadema.
Job Mrema: Ulisema umewahi kushitakiwa na ushahidi uliotoa hapa hujaeleza ulishitakiwa kwa kesi gani? Kesi namba ngapi ya Mahakama gani?
Mhe. Lissu: Nilielezea taarifa zakutosha kuhusu kesi hizo mahakama inajua.
Job: Ulisema huwezi kuwa Rais wa TLS halafu ukawa mtu wa hovyohovyo?
Mhe. Lissu: Hilo nilijibu zamani sana. Nilitumikia hiyo nafasi miezi mitano nikapigwa risasi.
Job: Ni sahihi ukitoka kuwa Rais wa TLS unaweza kuwa mtu wa hovyo hovyo?
Mhe. Lissu: Huyu sio mtu wa hovyohovyo. Na nina heshima zakutosha huko Duniani
Job: Umewahi kulalamika kokote kuhusu risasi ulizopigwa?
Mhe. Lissu: Anasimama sasa. Nimelalamika sana. Na wamekataa kuandika maelezo toka nikiwa hospitali Nairobi. Hawajawahi kuandika.
Job Mrema: Umejinasibu kama Mwanasheria
Mhe. Lissu: Kwani wewe hujui kama mimi ni mwanasheria? Utanifananisha na wewe?
Job Mrema: Kifungu cha 10(1) (2)cha CPA. Kinasemaje
Mhe. Lissu: Anakisoma kinahusu kuandikwa kwa maelezo.
Job Mrema: Unakielewaje?
Mhe. Lissu: Taarifa za kosa zinatolewa kwa maandishi au mdomo kwa afisa husika kwenye eneo husika.
Job Mrema: Ulikwenda kutoa taarifa?
Mhe. Lissu: Sikwenda kwasababu nilikuwa nusu mfu. Ulitaka niende lini? Nisingeweza kutoa hayo maelezo nilikuwa napigania uhai wangu.
Job Mrema: Jinai inakufa?
Mhe. Lissu: Ndio maana nilivyorudi nilienda kwa RPC Mroto Dodoma. Nikamwambia mlikuwa mnasema sikuwepo sasa nimerudi haya nihojini sasa kuhusu haya mambo. Hawakuwahi kunihoji kokote.
Job Mrema: Unapopata taarifa ya vitisho ni sahihi upeleke polisi hizo taarifa?
Mhe. Lissu: Ni sahihi kama hivyo vitisho havitoki kwa polisi wenyewe. Kama wanakutisha polisi unaenda tena polisi kutoa taarifa hizo kuwa wanakutisha. Utakuwa mwehu sio bure.
Watu wanacheka 😂😂
Part 296 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 294
Mwenyekiti ameingia tayari baada ya kumaliza kuongea na mawakili wake na break pia kwa ajili ya Chakula cha Mchana.
Alipata nusu saa pia ya kukaa na Mawakili wake na mashahidi wake wengine. Mh. Heche, Mnyika, Amani na Brenda walikuwepo nae.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa uko tayari tuendelee.
Mhe. Lissu: Niko tayari.
Katuga: Mh. Jaji naomba Exhibit D15. Makarani wanaitafuta. Ni maelezo ya PW 16. Ulisema wapelelezi hawakukuuliza maana ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: PW 1 alisema alikuhoji kuhusu maana ya maneno yako?
Mhe. Lissu: Hakunihoji hilo.
Katuga: PW 1 alisema alikupa nafasi kuhusiana na haya maneno kwanini yasiwe ya uhaini?
Mhe. Lissu: Nilimjibu mmeshanikamata na mmeshanishitaki tutakutana mahakamani ndio nilimjibu.
Katuga: PW 1 alikupa nafasi au hakukupa nafasi?
Mhe. Lissu: Alishanishtaki kwa uhaini.
Katuga: Ulizuiwa nini ulipoambiwa utoe maelezo yako?
Mhe. Lissu: Tutakutana mahakamani
Katuga: Ndio maana hukutaka kutoa maana ya maneno?
Mhe. Lissu: Sikuulizwa kuhusu maneno alisema kuhusu uhaini, nikamwambia twende mahakamani.
Katuga: Ungeweza kutoa maana ya maneno au usingeweza pale angekuuliza?
Mhe. Lissu: Sasa halikuulizwa hilo nitoleee nini? Ningejibu angeniambia.
Katuga: Ulirejea Maelezo D15 ni maneno ambayo umeyaamini na yapo kwenye kielelezo chako?
Mhe. Lissu: Maneno yapi? Unauliza mambo jumla jumla. Eleweka.
Katuga: Baada ya kuunda timu mimi na timu tulisikia
Mhe. Lissu: Tulisikiliza sio tulisikia soma vizuri wewe
Katuga: Nina miwani siku hizi sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Ukiwa na miwani ndio unasoma vizuri acha uongo.
Katuga: Yangu ni ya bei halisi
Lissu: Sasa unalipwa nini? Au unajitutumua bure tu hapa?
Katuga: Je haya maneno nimesoma ulirejea?
Mhe. Lissu: In relation na ushahidi wa PW1 ndio niliyarejea. Kuhusianisha na PW 16 alichosema.
Katuga: Kwahiyo ulikiamini kielelezo?
Mhe. Lissu: Nilikiamini kivipi? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.
Katuga: Kwahiyo ulikiamini?
Mhe. Lissu: Mimi niwaamini Mapolisi hawa? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.
Katuga: Sasa nijibu unayaamini yaliyomo humo?
Mhe. Lissu: Niamini nini?
Katuga: Uko sawa kweli?
Mhe. Lissu: Wee unanionaje?
Katuga: Naona uko sawa.
Mhe. Lissu: Sasa unaniuliza nini kama unasema niko sawa?
Jaji: Sasa wakili toka hapo. Tumeshapata majibu.
Katuga: Ulisema haya maelezo yote kuanzia D1 hadi D16 ulitaka yatumike kwa ajili yako?
Mhe. Lissu: Nilishajibu toka zamani. Kwa ajili ya kuonesha utofauti wa ushahidi. Contradiction ya ushahidi na ommission zilizofanyika.
Katuga: Kuna sehemu ulisema mahakama i exclude baadhi ya maneno yaliyopo humu?
Mhe. Lissu: Hiyo ni kazi ya submission.
Katuga: Narudia tena ulisema au hukusema?
Mhe. Lissu: Nimekwambia hiyo ni kazi ya submission.
Jaji Ndunguru: jibu tu swali shahidi umeiambia mahakama au hujaiambia.
Mhe. Lissu: Narudia tena nitawaambia wakati wa final submission nimemaliza.
Jaji Ndunguru: Haya sasa wakili wa serikali endelea mbele. Jibu ndio limeshatoka hilo na halitabadilika.
Kicheko kutoka kwa umma 😂😂😂
Katuga: Mheshimiwa Jaji naomba nirudishe kielelezo.
Anaendelea kupekua makaratasi yake. Kamaliza maswali ila anatupotezea muda tu hana lolote mshenzi huyu.
Part 295 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Nassoro Katuga; waambie waheshimiwa majaji kama ni kweli uliwaambia hawa mashahidi wa kificho hawajulikani Mahakamani isipokuwa kwa waendesha mashitaka?
Tundu Lissu: ndiyo, nimesema.
Nassoro Katuga; waambie kwamba haya maneno umesema kuonyesha ukweli wako
Tundu Lissu: kweli
Nassoro Katuga; ulileta kipingamizi jinsi kizimba cha mashahidi kilivyo?
Tundu Lissu; ndiyo
Nassoro Katuga; waambie kwamba baada ya kurebishwa majaji walikuwa wanawaona
Tundu Lissu; wanawaona lakini hawawajui majina wala chochote kuhusu wapo
Nassoro Katuga; iambie mahakama ulikuwa una refer mashahidi kwa P1 na P2
Tundu Lissu; P siyo jina la mtu ni jina bandia na hakuna mtu anaitwa P2
Mahakama; 😂🤣😂🤣😂🤣😂🤣😂🤣
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 293
Katuga: Tuahirishe kidogo kutoka kwenye D4 hivyo vielelezo tuhamie eneo lingine. Ulisema hawajaleta video kwahiyo wameshindwa kuthibitisha mashitaka yao wenyewe ulisema hivyo?
Mhe. Lissu: Ndio.
Katuga: Wakati unayasema hayo ulikuwa unayajua mashitaka yanayokukabili?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: Ulikuwa umeyaelewa?
Mhe. Lissu: Sana tu.
Katuga: Mashitaka unayokabiliana nayo kuna sehemu yoyote inayosema unashitakiwa kwa kuchapisha video?
Mhe. Lissu: nachapisha maneno kwenye video iliyosambazwa na jambo Tv.
Katuga: Kwa mujibu wa ushahidi video kiushahidi ina kitu ambacho unaona na kusikia?
Mhe. Lissu: Sawa.
Katuga: Maneno yanaonwa au yanasikiwa?
Mhe. Lissu: Maneno yanasikiwa na kuonwa kwenye kesi hii. Kwa mujibu wa sheria ya ushahidi kitu chakuonwa kinaonwa na chakusikiwa kinasikiwa.
Katuga: Kwenye hiyo video maneno unaona au unasikia?
Mhe. Lissu: Iko wapi sasa hiyo video. Ninayo hapa??
Katuga: Kwahiyo walichokileta ndio walichokisia?
Mhe. Lissu: Huwezi kutenganisha video na maneno. Kivipi sasa? Maneno yapo kwenye video.
Katuga: Kila shahidi anapaswa kuaminiwa?
Mhe. Lissu: Washahidi wa kweli ndio huaminiwa. Waongo hawaaminiwi.
Katuga: Je katika mashahidi wa Jamhuri ni kifungu gani cha Sheria kinasema lazima ulete video ndio tuseme maneno yalisemwa?
Mhe. Lissu: Hiyo ni common sense tu.
Katuga: Akija shahidi akasema niliona radi imepiga na kuua watoto lazima alete video ndio tumuamini?
Mhe. Lissu: Sasa radi na video vinahusiana. Video ilirekodiwa. Sasa radi nani ameruhusu itokeee hadi useme irekodiwe.
Katuga: kama video ikifutwa mtu aliyeona hawezi kutoa ushahidi na kuthibitisha?
Mhe. Lissu: Unakuja kuthibitisha video ipi sasa wakati huna?
Katuga: Kati ya maneno au video ameleta nini?
Mhe. Lissu: Hajaleta chochote. Maneno ya kwenye video yapo kwenye video. Hayawezi kutenganishwa.
Katuga: PW17 alikuwepo Live kwenye Mkutano wako na alisema anayoyakumbuka kwamba mtazuia uchaguzi.
Mhe. Lissu: Hakusema hivyo.
Katuga: Shahidi aliyekuwepo eneo la tukio PW17 ni lazima alete video?
Mhe. Lissu: Ni lazima kwasababu aliyaleta mambo ya video mwenyewe inabidi iwepo.
Katuga: PW 17 kuna mahali alisema alikuwa anaiona na kuisikia?
Mhe. Lissu: Alikuwa anarusha matangazo live sasa atarushaje bila kuiangalia?
Katuga: Mashahidi mapolisi hawaaminiki kwasababu waliandika maelezo yao wenyewe?
Mhe. Lissu: Hawaaminiki kwasababu hawakufuata taratibu za kuandika maelezo.
Katuga: Kila shahidi anaaminika
Mhe. Lissu: Anaaminika shahidi kwasababu ya ushahidi wake sio sura yake.
Katuga: Mimi sina nia mbaya.
Mhe. Lissu: Umenishtaki kwa uhaini halafu uwe hauna nia mbaya.
Katuga: Kifungu gani cha Sheria kinakataza Mapolisi kutoa ushahidi
Mhe. Lissu: Mashahidi ambao hawakufuata utaratibu ndio ushahidi wao hauwezi kuchukuliwa kwa uzito wowote.
Part 294 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 292
Katuga: Naomba twende kwenye D3 Lissu anasema ngoja nitafute. Ametafuta kwa muda mrefu ameipata sasa.
Katuga: D3 kielelezo alisema ananunua Ilala Boma Sokoni. Hiyo ni omission au contradiction?
Mhe. Lissu: Ni omission na ni contradiction pia.
Katuga: maneno kwamba hayamo kwenye maelezo yake kwa mujibu wa jibu hili yanakanganyana na nini?
Mhe. Lissu: Yanakanganyana na kariakoo na Posta Mpya. Wakati huku amesema Ilala Boma.
Katuga: Swali kwa PW4 kwamba alikuwa na smartphone sony Galaxy yapo au hayamo kwenye kielelezo. Alisema hayamo.
Mhe. Lissu: Ndio. Na ni Omission.
Katuga: Kuhusu kuwa na account facebook hajaandika kwenye maelezo? Unasemaje.?
Mhe. Lissu: Hakuandika ni Omission.
Katuga: Alisema amemuona Tundu Lissu kuhusu na hiyo ni Contradiction au Omission?
Mhe. Lissu: Ni Omission
Katuga: huku alisema mzozo huku amesema mabishano. Kwani utofauti ni nini?
Mhe. Lissu: Mzozo ina element za ugomvi hakuna ustaarabu mabishano ni kutofautiana mawazo. Hata marafiki wanabishana.
Wameomba break ya dakika kumi
Part 293 itaendelea baada ya break.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 291
Katuga: Kutokulipiwa na matibabu na umeeleza vitu vingi kuhusu uchaguzi. Imani yako uliposema imani yako na mahakama haipo kwahiyo huna imani?
Mhe. Lissu: Hilo ni la kuuliza kweli. Kwenye maswala haya sina IMANI KABISA NA MAHAKAMA.
Katuga: Maswala yapi?
Mhe. Lissu: Si ya Uchaguzi tunazungumzia.
Katuga: Kwahiyo hukupanga kuiomba Mahakama kutengua vifungu fulani vya Katiba?
Mhe. Lissu: Sikupanga.
Katuga: Uliamua kutafuta njia nyingine mbadala?
Mhe. Lissu: Njia ya mbadala ya Kidemokrasia.
Katuga: Jana nilikuulizia kuzuia uchaguzi ni njia ya kidemokrasia.
Mhe. Lissu: Haswaa.
Katuga: Kukinukisha ni njia ya kidemokrasia?
Mhe. Lissu: Haswaa ni njia ya kidemokrasia.
Katuga: Kuhamasisha uasi je?
Mhe. Lissu: Njia ya kidemokrasia kabisa. Mwalimu Nyerere alisema uasi dhidi ya mifumo kandamizi ni halali kabisa.
Katuga: Kifungu cha 52 cha Media Service Act iko sawa na kifungu cha 55?
Mhe. Lissu: Iko sawa.
Katuga: Sheria ya Huduma za Habari iliundwa ku regulate huduma ya habari?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: Kuzuia uchaguzi uliopo kwa mujibu wa sheria ni kuipinga serikali?
Mhe. Lissu: ni kuzuia uchaguzi. Kuipingaje tena serikali?
Katuga: Kuhamasisha uasi, kukinukisha. Ni kuipinga serikali au kuipindua serikali.
Mhe: Lissu: Hatukuwa tunazungumza habari za serikali.
Katuga: Mbona nakuuliza swali kwa heshima tu
Mhe. Lissu: Huna heshima hata kidogo. Uitoe wapi?
Katuga: Unakumbuka ulisema kuipinga serikali sio kosa?
Mhe. Lissu: Nimesema.
Katuga: Sasa ulikuwa unamaanisha nini?
Mhe. Lissu: Nassoro Katuga nimesema kifungu cha 55 hakijasema serikali peke yake
Katuga: Mimi mdogo ndio maana unanionea.
Mhe. Lissu: Wewe mdogo ungekuwa hapa? Una udogo gani wakili mkuu wa serikali?
Katuga: Ulisema mapolisi kujiandika maelezo ni kinyume cha sheria na je uliwatajia sheria.
Mhe. Lissu: Sikuwaambia lakini kifungu kipo na kinajulikana.
Katuga: Sasa mbona unaniambia sina adabu halafu wewe hujibu maswali.
Mhe. Lissu: Unataka niseme yakwako?
Katuga: Ulisema vielelezo vilivyoingia mahakamani uliviingiza wewe?
Mhe. Lissu: Viliingizwa na Mahakama.
Katuga: Kwahiyo umeridhika na content za hivyo vielelezo?
Mhe. Lissu: nimeridhika vitumike kuonesha sina hatia.
Katuga: Naomba D1 hadi D16.
WANAMTAFUTIA WAMPATIE VIELELEZO.
Katuga: Unakumbuka D1 ni kielelezo cha Kaaya ambae ni PW2 na uliomba yatumike kwa nia ya kudodosa shahidi kwa mujibu wa kifungu cha 163?
Mhe. Lissu: Kweli
Katuga: ni kweli tulisema kuhusu ommission na contradiction?
Mhe. Lissu: Nilisema.
Katuga: Ulisoma kifungu cha 163 hapa Mahakamani? Na ukasema hakuna neno omission kwenye kifungu hicho na neno pekee lililopo ni contradiction?
Mhe. Lissu: Nakumbuka.
Katuga: Ulimuuliza Kaaya ameajiriwa mwaka 2009 na ameenda Zanzibar au hajaenda? Na akajibu hayamo? Unakumbuka?
Mhe. Lissu: Nakumbuka.
Katuga: kutokuwepo kwenye maelezo yake ni contradiction au ommission?
Mhe. Lissu: Omission.
Katuga: Kwenye hiki kielelezo ni contradiction gani ipo hapo?
Mhe..Lissu: Mahakamani alisema ni Uhaini lakini kwenye maelezo amesema ni makosa ya jinai.
Katuga: Uhaini ni madai au jinai?
Mhe. Lissu: Jinai ziko ngapi sasa? Alitakiwa kueleza kuwa jinai ni ipi?
Katuga: Ni bado unasema kwenye hiyo nyaraka kuna contradiction
Mhe. Lissu: Nimeshaonesha.
Katuga: D2 unakumbuka ulimuhoji kwamba yeye ni mtaalamu wa picha aliyetangazwa kwenye GN 725 akajibu maneno hayo hayamo.
Mhe. Lissu: Ndio.
Katuga: Je hiyo ni Contradiction?
Mhe. Lissu: Ni comtradiction ndio kwasababu zilitajwa GN. mbili tofauti. Ni contradiction ya akichokisema kwenye maelezo yake ya maandishi.
Katuga: Yale majibu yote aliyosema hayamo yalikuwa ni contradiction au ommission?
Mhe. Lissu: Ni omission
Katuga: Ulisema hiyo omission inaenda kwenye root ya kesi
Lissu: Tutasema hayo mengine kwenye final submission mimi ni shahidi wa facts.
Part 292 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.