Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, ikiongozwa na Wakili wa Serikali Haruna Matata, imewasili Mkoani Ruvuma na kupokelewa na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Joseph Martin Kabalo, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma tarehe 16 Septemba, 2026
Makamu wa Rais Mhe. Deogratius Ndejembi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) linalofanyika Vienna nchini Austria.
Watumishi wa NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wameshiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Songwe mkoani Songwe, ambapo jumla ya miche 4,500 ya matunda, mbao na kivuli imepandwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC, Mhandisi Mwanasha Tumbo akipanda mti eneo la Mtumba, Dodoma kuadhimisha siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Uzalendo ni kutunza mazingira, shiriki kupanda miti"
Ulichukua nchi katika nyakati ngumu, ukiamua Taifa kupitia maneno na matendo yako. Walio nyuma ya pazia wanaelewa ni mabaya mangapi umeyaepusha juu ya Taifa hili na wakati ikifika umma utakua pia.
Wewe ulikua ni mtu sahihi kwa wakati sahihi. Heri ya Siku ya Kuzaliwa Rais wangu, @SuluhuSamia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akizungumza leo tarehe 27 Januari 2026 katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Watanzania wote waliozaliwa mwezi na tarehe kama ya leo, akitambua kuwa wapo wengi waliozaliwa mwaka mmoja au miaka iliyofuatia. Akiwahimiza Watanzania wote kuungana katika zoezi muhimu la kuhuisha uhai na kuendeleza mazingira ya nchi.
Mhe Rais ameeleza kuwa zoezi la upandaji miti lililofanyika leo ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza mazingira kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Kwa msingi huo, Rais Samia ameungana na kauli mbiu ya tukio hilo inayosema: “Uzalendo ni kutunza Mazingira, Shiriki kupanda miti.”
Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi sio nadharia bali ni ukweli unaoonekana na kuathiri maisha yetu. Akiongeza kuwa, nchi zote duniani zinakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, hivyo ni jukumu la kila mtu kuchukua hatua za kulinda mazingira.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MazingiraNiUtu #DiraYaSamia
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na mwingi wa rehema kwa kunijalia kuifikia siku nyingine ya kumbukizi ya kuzaliwa na umri wa miaka 66. Kwa moyo wa dhati, nimepokea na ninawashukuru nyote kwa salamu zenu za upendo.
Nimesherehekea siku hii kwa kupanda miti. Wito wangu kwenu, tujenge na tuendeleze utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira ili nayo yaendelee kututunza sisi na vizazi vijavyo.
SERIKALI YAWEKEZA SH. BILIONI 8.05 KUIMARISHA SEKTA YA UMWAGILIAJI RUDEWA – KILOSA
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
@SuluhuSamia inaendelea kuimarisha sekta ya kilimo kupitia uwekezaji wa Shilingi bilioni 8.05 katika Mradi wa Umwagiliaji Rudewa, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Mradi huu kwa sasa umefikia takribani asilimia 40 ya utekelezaji na unaendelea kutekelezwa kwa kasi, ukihusisha ujenzi wa mifereji ya maji yenye urefu wa zaidi ya kilomita 21 pamoja na ujenzi wa vigawa maji zaidi ya 50.
Utekelezaji wa mradi huu unategemea kunufaisha jumla ya hekta 1,000 za umwagiliaji, zaidi ya wakulima 900 kutoka vijiji vya Rudewa Batini, Mbuyuni na Gongoni, na hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao na kuimarisha ustawi wa wakulima.
Kupitia mradi huu, Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wa kilimo, kupunguza utegemezi wa mvua, kuongeza kipato cha wakulima pamoja na kuimarisha usalama wa chakula nchini. #TanzaniaYetuSote #NchiYetuKwanza #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
HAPPY BIRTH DAY IN ADVANCE MH RAIS SAMIA:WATANZANIA TUMUUNGE MKONO KWA KUPANDA MITI SIKU HIYO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Mama Samia Suluhu Hassan January 27,2026 atakuwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa.Hongera Mh Rais kwa kuongeza mwaka mwingine tena.
UJENZI WA MABWENI YA WASICHANA MONDULI WAFIKIA ASILIMIA 58
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
@SuluhuSamia inaendelea kupiga hatua katika kuimarisha miundombinu ya elimu, baada ya ujenzi wa mabweni ya wasichana katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kufikia asilimia 58 ya utekelezaji.
Mradi huu unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wanafunzi 500 na kwa sasa unaendelea kuelekea Awamu ya Nne ya ujenzi, hatua itakayoongeza upatikanaji wa makazi salama kwa wanafunzi wa kike.
Ujenzi wa mabweni haya unalenga kulinda usalama wa wasichana, kuwezesha mazingira tulivu na rafiki ya kujifunzia, kuongeza fursa za makazi chuoni pamoja na kukuza ushiriki wa wasichana katika elimu ya ufundi na maendeleo ya jamii.
Hatua hii ni sehemu ya jitihada endelevu za Serikali katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na upatikanaji wa elimu bora kwa wote. #TanzaniaYetuSote #NchiYetuKwanza #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea na kujadili taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zilizo chini yake.