Jukwaa la #JamiiCheck hufanya kazi ya Kuhakiki Taarifa zinazopatikana ndani na nje ya Mtandao ili kubaini kama zina Ukweli, Uzushi au Nadharia
Jukwaa hili huwa na 'Logo' yenye rangi 4 ambazo ni Njano ikimaanisha Taarifa mpya inayosubiri kuhakikiwa, Kijani ikimaanisha Taarifa iliyohakikiwa na kukutwa na Ukweli, Nyekundu ikimaanisha Taarifa iliyohakikiwa na kukutwa haina Ukweli pamoja na Kijivu ikiwakilisha Taarifa iliyohakikiwa na kukutwa ni Nadharia
Tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhakiki wa Taarifa, hakikisha unatumia Jukwaa hili uwe sehemu ya Watu wanaopambana na Usambazaji wa #TaarifaPotofu Mtandaoni
Kufikia Jukwaa, bofya https://t.co/W8HIxVoqeH
#FactCheckingDay #FactsMatter #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
Taarifa zinazohusu fedha, talaka na mastaa huenea haraka mtandaoni kwa sababu huibua hisia.
Kabla ya kuamini au kusambaza, hakikisha taarifa imethibitishwa na chanzo kinachoaminika.
Zaidi Soma https://t.co/OjTwCth3fK
#JamiiCheck#FactsCheck#FactsChecking#VisitJamiiCheck #FactsMatter
JamiiCheck imejiridhisha kuwa video inayosambazwa mtandaoni ikidai Baraza la Wazee la CHADEMA (BAZECHA) limejitoa chamani imepotoshwa. Uchunguzi umebaini Video hiyo ni ya mwaka 2019 na imekatwa kisha kuunganishwa kwa namna inayobadili muktadha wake halisi.
Katika video halisi, aliyekuwa Mwenyekiti wa #BAZECHA, Hashim Juma, alikuwa akizungumzia uamuzi wa chama kususia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019, na si kutangaza kujitoa kwa baraza hilo.
Zaidi soma https://t.co/ydrjdjh9Ht
#JamiiCheck #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #FactsMatter
Inaelezwa kuwa changamoto kubwa inayowakabili wananchi wengi ni ukosefu wa taarifa sahihi na elimu kuhusu maeneo na njia bora za uwekezaji wenye tija.
Ili kufanya maamuzi yenye tija na manufaa ya kiuchumi, kuna umuhimu mkubwa kwa wadau kuendelea kutoa elimu endelevu itakayowawezesha wananchi kuelewa mifumo salama na fursa sahihi za kuelekeza mitaji yao.
#JamiiCheck #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #FactsMatter
Video inayomuonesha raia wa China akidaiwa kutembea juu ya maji si halisi. Uchunguzi umebaini kuwa video hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde (#AI).
Uchambuzi wa video unaonesha kutokuwepo kwa mwingiliano wa kawaida kati ya mwili wa mtu huyo na maji. Pia, hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha uwepo wa viatu vinavyomwezesha mtu kutembea juu ya maji kama inavyoonekana.
Zaidi soma https://t.co/kXc43DpdTp
#JamiiCheck #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #FactsMatter
Hata hivyo, Watu wenye matatizo ya #Figo wanatahadharishwa kuwa waangalifu wanapokunywa maji ya madafu kwa kiasi kikubwa, kwani yanaweza kusababisha mwili kuhifadhi madini ya #Potassium kwa kiwango kinachozidi mahitaji, hali ambayo inaweza kuwa hatari kwa afya.
Zaidi soma https://t.co/WbnJiS2ldn
#JamiiCheck #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck #FactsMatter