#TANZANIA: WAKATI WANAWAHUBIRIA AMANI YA MCHONGO, SISI CHADEMA TUNASEMA FREE LISSU NA KATIBA MPYA - BRENDA
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano wa CHADEMA Taifa, @BrendaRupia akiwahutubia wakazi wa Nachingwea mkoani Lindi leo Juni 18, 2026 amesema wakati @ccm_tanzania wanawahubiria amani aliyoiita ya mchingo wao @ChademaTZ2 wanasema haki kwanza, na wanataka Lissu aachiwe huru na ipatikane Katiba mpya kwanza ndipo amani ya kweli itatawala.
Zaidi: https://t.co/zwCZe8vDMg
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Taifa, Sharifa Suleiman, amesema kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, yuko ndani akikabiliwa na kesi ya uhaini kwa sababu ya kupigania haki za wanyonge na kutetea maslahi ya wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Nachingwea mkoani Mtwara leo Alhamisi Juni 18, 2026, Sharifa amesema chama hicho kinaamini kuwa Lissu si muhaini, bali ni kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wananchi.
"Takribani mwaka mmoja sasa Mwenyekiti wetu wa CHADEMA Taifa yupo ndani kwa tuhuma za kesi ya uhaini. Tundu Lissu si muhaini, bali amefika pale kwa sababu ya kutetea wanyonge," alisema Sharifa.
Katika mkutano huo, Sharifa amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kudai katiba mpya, akieleza kuwa ndiyo suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa dawa katika hospitali na changamoto nyingine za kijamii na kiuchumi.
Amesema licha ya Tanzania kuwa na rasilimali nyingi, wananchi wengi bado hawajanufaika ipasavyo na matunda ya rasilimali hizo, huku wanawake wakibaki kuwa miongoni mwa makundi yanayoathirika zaidi.
Aidha, amewataka wananchi kusimama kwa pamoja kudai haki, usawa na maendeleo kupitia mchakato wa kupata katiba mpya, akisisitiza kuwa mabadiliko hayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa.
Sharifa pia ametoa wito wa kuachiwa huru kwa Tundu Lissu, akisisitiza kuwa wanachama na wafuasi wa chama hicho wataendelea kutumia njia za kikatiba na kisheria kudai haki hiyo.
Akihitimisha hotuba yake, amesema taifa lenye haki ndiyo taifa lenye amani na maendeleo ya kweli, huku akisisitiza kauli mbiu ya chama hicho ya kudai katiba mpya sasa.
"Mimi nilikuwa bungeni miaka kumi, ni mchaga, si mlisikia Spika (Job Ndugai) alisema nilikopa hela kwamba nina stress ya madeni? Mimi nilienda kule nikakwarua zote kwasababu nilijua wale wasela hawachelewi kubadilisha sera halafu nikapoteza kiinua mgongo, nikawalia timing palepale nikaenda kwa Mtunza hazina, akaniambia ninaweza kukopa mpaka milioni 300 nikamwambia leta, akaniambia kuna nyingine naweza kopa Milioni 150, nikachukua, wanakuja kushtuka wale wamenikopesha ziada Milioni 200, ikawa kama Milioni 600 hivi, wanakuja kuangalia kwenye akaunti wanakuta sifuri."
"Ndugai alimind sana, Ndugai akanifukuza bungeni mwaka ili wasinilipie marejesho ili vitu viuzwe na baadae benki wakaniandikia barua ya kutaka kushikilia vitu vyangu kwani Bunge limekataa kunilipia, nikawajibu nikiwataka watafute muda na saa niwatembeze kwenye mali zangu wachague wanazozitaka ili waunganishe na mkopo wao, nikishindwa kulipa wauze."
"Ndugai akanitangaza kuwa nina stress, nina presha ya madeni, nikasema poa, na kwenye akaunti hawazioni maana zilipita tu. Wakanifukuza bunge mwaka, Bashiru Ally aliyekuwa Katibu Mkuu akaniambia Magufuli anataka niwe Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM na watanilipia madeni yangu yote! Nikasema sitaki, mimi sio Blueband. Wakaniambia vitu vyangu vitauzwa? Nikawaambia vitauzwaje wakati mimi mchaga? Nitaendesha hata Haice. Sasa nikatoroka kwenda Canada, nikarudi, sina deni, Ndugai kafa, Magufuli kafa na Bashiru sio Katibu Mkuu tena, huyo sio Mungu?"
"Sasa ndugu zangu tukitoka hapa tunarudi Ifakara, kama watekaji wapo hapa tutaanza safari muda sio mrefu kwahiyo wanaweza kukaa katikati hapo porini ila nawaonya Mungu wangu mimi ni kiboko mtakufa! Kama umepewa dili la utekaji hilo dili likatae utakufa na aliyekutuma atakufa, hatutaki mazishi wiki hii."Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema akihutubia kwenye mkutano wa hadhara, Mlimba Mkoani Morogoro leo Juni 18, 2026.
Waridhiane na nani? Hivi hawana hata chamber ya aibu hawa?
Kuna tetesi akiwa RC Mbeya anajua Redrack Chaula na Dioniz Kipanya walivyopotea maridhiano si yaanze kwa kuwaweka huru?
Bila Lissu na wote waliotekwa na walio mahabusu kuachiwa hakuna maridhiano.
#TANZANIA: BAWACHA TUTATUMIA NGUVU YA ZIADA LISSU AACHILIWE - SHARIFA
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa, Sharifa Suleiman leo Juni 18, 2026 akizungumza na Wakazi wa Nachingwea mkoani Lindi amesema wao kama Wanawake watafanya jitihada za kila namna kumtoa Mwenyekiti wao wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini, "BAWACHA tutatumia nguvu ya ziada Lissu aachiliwe huru"
Zaidi: https://t.co/poRUb5y7RN
VIDEO:
Ni kama vile 'Kiapo kwa Watanzania' ambacho viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2) 'wanakitoa'
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara John Heche @HecheJohn anasema viongozi wa CHADEMA wameamua kuwa mstari wa mbele 'kuwapigania' Watanzania huku wakijuwa kile alichokiita kuwa ni 'hatari' iliyopo mbele yao
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika leo, Alhamisi Juni 18.2026, Nachingwea, Mkoani Lindi Heche amesema viongozi wa chama hicho wamekubali kuwaacha watoto wao yatima kwaajili ya maslahi ya Watanzania wote.
"Vyombo vya dola vikiwemo baadha ya askari Polisi kupiga risasi na kuua watu Oktoba 29, 2025 kwa sababu wanathamini tembo kuliko watu. Serikali ya CCM inawaona Tembo kama ndio watu halafu watu kama wanyama." Mhe. @jjmnyika@ChademaTZ2
"Serikali ya CCM imeua watu kama matendo ya Serikali ya Mjerumani wakati wa vita vya majimaji, matendo ya kuwinda raia kama unawinda Tembo." Mhe. @jjmnyika
VIDEO:
Akiwa Nachingwea, Mkoani Lindi, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2) Tanzania Bara John Heche @HecheJohn ameoneshwa kukerwa na uwepo wa miundombinu mibovu ya Barabara, hatua ambayo imepelekea kukosoa vikali mipango ya serikali katika kushughulikia changamoto za aina hiyo,
Sambamba na hilo, Heche ametulia jukwaa la Mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nachingwea kutoa ushauri kwa serikali namna ya kumaliza tatizo hilo, na hapa anagusia Barabara ya Masasi -Nachingwea - Liwale
"Nitoe ushauri kidogo kwa Ridhiwani Kikwete, amtafutie mama yake kazi ya kufanya, CCM tunakwenda kuifuta Kanda hii ya Kusini." MHE. BELCHOMAS PONERA, Kaimu Mwenyekiti Kanda ya Kusini
Mkazi wa Mbeya anayejulikana kwa jina la Mzee Msinga amesema amewahi kuwa mwanachama wa vyama mbalimbali vya siasa ikiwemo TANU, CCM na TLP kabla ya kujiunga na CHADEMA, ambapo anadai kuwa ameona chama hicho ndicho kinachotoa matumaini makubwa kwake.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Juni 15, 2026 katika Kata ya Bonde la Songwe, Jimbo la Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mzee Msinga alitoa madai kuhusu kile alichokiita vitendo vya ukatili alivyodai kufanyiwa yeye na familia yake na baadhi ya askari polisi kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025.
Mzee Msinga alidai kuwa askari walifika nyumbani kwake, wakaharibu mali ikiwemo geti na kuwafanyia vitendo vya ukatili watoto wake, hali ambayo amesema ilisababisha baadhi yao kupata ulemavu na wengine kubaki na makovu ya kudumu. Aidha, alihoji uhalali wa vitendo hivyo na kuwataka wahusika kuwajibika.
Kauli hizo zilitolewa mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kisiasa.
Hata hivyo, madai hayo ni ya Mzee Msinga na hayajathibitishwa na mamlaka husika. Serikali na Jeshi la Polisi hawakuwa wametoa maelezo kuhusu tuhuma hizo katika mkutano huo.
Mama Samia, pengine wanaokuzunguka wanakudanganya sana. Na msingi wa uongo huo kwao unaweza kuwa biashara kubwa sana. Wanaweza kuwa wanatumia intimidation kama strategy muhimu kwa maslahi yao. Lakini ukweli ni kwamba siasa za aina hii za kuongeza presha na taharuki hazileti faida ya muda mrefu kwa nchi, bali kwa watu wachache tu wanaonufaika na hali hiyo.
Kuhusu Mh Tundu Lissu, kumuweka mahabusu au kumdhibiti kisiasa hakutaondoa changamoto za kisiasa, bali kunaendelea kuongeza taharuki zaidi ndani na nje ya nchi. Hasara kubwa si yeye kufanya siasa akiwa nje, bali ni kuendelea kumuweka mahabusu.
Kwa mtazamo huu, hii sio faida , bali inaweza kuwa faida kwa watu wanaonufaika na mvutano huu. Ndiyo maana wakati mwingine huonekana kuna mkakati wa kupandisha presha ili maslahi fulani yaendelee kunufaika. Hofu nayo ni biashara , tena Tax free.