Mimi nina roho ndogo sana,
Hii video nimeitazama jana nikashindwa kuimaliza, nimerudia leo asubuhi, mchana leo nikapata ujasiri nikasikiliza yote.
Huyu ni mwanamke kama mimi, amejaliwa mtoto mmoja wa kipekee kama ilivyo kwangu.
Lakini mwenzangu mtoto wake hajawahi kurudi nyumbani yeye wala mwili wake tangu October 29.
Mama anamuomba Samia awaonyeshe Makaburi angalau wawe wanaenda kuwaangalia watoto wao.
Anakumbuka vile alimsomesha kwa kuuza uji mpaka anakua, kwamba mapito yote aliyopitia kumlea alikuwa akimlea ili Samia aje kumuua.
Huyu ni mmoja tu, niambie ni akina mama wangapi wanapitia haya anayopitia huyu mama aliyebebeshwa mateso ya kudumu kwa kutokuanua matanga ya mwanae mpaka siku ya kufa kwake.
Ila Samia, iko siku yako.😭
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 208
Wakili wa Serikali
Cathbert: Eeh nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P9 : Nilienda kituo cha Polisi na nilipofika waliniambia ya kuwa nahitajika kama Shahidi hivyo natakiwa nihojiwe tena
Cathbert: Eeh endelea shahidi
Shahidi wa kificho P9 : Walinihoji na kuniandika maelezo yangu na baada ya kumaliza waliniruhusu kuondoka na kuniambia ya kuwa ntapohitajika watanitafuta na aliyenihoja na kuniandika maelezo ni mmoja na mwingine alikuwa akichangia kuniuliza maswali mbalimbali.
Cathbert: Aliyekuhoji kama shahidi alikuhoji kwa ajili ya jambo gani?
Shahidi wa kificho P9 : Alinihoji juu ya kuhamasisha kuzuia uchaguzi na hilo jambo lilianzaje ambapo nilimueleza ya kuwa niliona clip katika mtandao kuhusu huo uhamasishaji na hiyo clip ilikuwa ni ya Lissu akihamasisha kuzuia uchaguzi.
Cathbert: Wahe. Majaji kwa Shahidi huyu ni hayo tu.
Anasimama Wakili wa Serikali Mkude
Mkude: Tuna Hoja hapa kwa kuwa Shahidi kamaliza na muda uliofika tulikuwa tunaomba kama hakuna pingamizi kwa upande wa Lissu tuweze kuendelea kesho na Cross Examination
Mhe. Lissu: Sina Objection
Mahakama : Mhe. Lissu hizi dakika 19 hazitoshi kumaliza Cross yako
Mhe. Lissu: Wahe. Majaji naweza kwenda kwenda ila siwezi ku-promise ya kuwa nitamaliza
Mahakama : Basi for consistency nzuri ya ushahidi tuharuhusu kuendelea kesho asubuhi na mapema na ile hoja ya submission on the notice of List of Additional tunaifanyaje?
Mhe. Lissu: Nilikuwa naomba tukimalizana na P9 kwa kesho tuendelee na mashahidi wengine kisha mwisho turudi kwenye hoja za hiyo submission on Notice of List of Additional.
Mkude: No objection.
Mahakama imehairishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi.
Mnisamehe sana leo updates zimesuasua kwasababu afya yangu imeyumba kidogo.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 207
Wakili wa Serikali Cuthbert anaendelea kumuongoza Shahidi wa kificho P9.
Cathbert: Unakumbuka nini kuhusu 3/4/2025?
Shahidi wa kificho P9 : nilikuwa nyumbani kwa tarehe hiyo na nilikuwa nikiperuzi kwenye mitandao
Catherbert: Simu ilikuwa ni ya Aina gani?
Shahidi wa kificho P9 : Simu yangu ilikuwa ni Samsung 8 Pro na nilikuwa naperuzi kwa kuingia katika Akaunti ya IG ambao ni mtandao wa kijamii ambao unakuhitaji uwe na Akaunti ya kuweza kuingia na pia uwe na simu janja pamoja na bundle la internet ili kuangalia vitu humo Instagram.
Cathbert: Kwenye IG unaangalia Nini humo?
Shahidi wa kificho P9: picha na video
Cathbert: Eeh baada ya kufungua?
Shahidi wa kificho P9 : Baada ya kufungua IG na kuingia niliona video ya Lissu ambayo ilitumwa katika Akaunti ambayo nimeisahau.
Cathbert: Eeh uliona nini katika hiyo video?
Shahidi wa kificho P9 : Nilimuona Lissu akihamasisha kufanya vurugu na kuzuia uchaguzi.
Cathbert: Mazingira ya Video yalikuwaje?
Shahidi wa kificho P9 : Mazingira yalikuwa ni ya ukumbi
Cathbert: Na Lissu alikuwa vipi?
Shahidi wa kificho P9: Lissu alikuwa kavalia Kombati la Chadema, ndani kavaa Tshirt nyeusi pia kulikuwa kuna bendera ya Taifa na bendera ya Chadema.
Cathbert: Huo uchaguzi alikuwa anauongelea kuuzuia ni upi?
Shahidi wa kificho P9: Ni uchaguzi wa Raisi, Wabunge na Madiwani.
Cathbert: Lissu alisema atauvuruga uchaguzi kwa namna gani?
Shahidi wa kificho P9 : Alisema atafanya vurugu na kuzuia uchaguzi ili usifanyike kwa kusema ya kuwa "Ni lazima tukichafue"
Bwana P9 nae anaendelea hapa kutueleza mambo yake.😂
Cathbert: Eeh baada ya wewe kusikia hotuba hiyo ulichukua hatua gani?
Shahidi wa kificho P9 : kwa ukweli kwa kipindi kile mimi kama mfuasi wa Chama nilihamasika
Cathbert: Unakumbuka nini kuhusu tarehe 4/4/2025?
Shahidi wa kificho P9 : Hiyo tarehe nilikuwa nyumbani na majirani zangu tulikutana na kujadili hilo suala tuliloliona katika video kwa kusema ya kuwa kama Mwenyekiti kasema tukichafue na tuzuie uchaguzi itakuwaje sasa hivyo tukawa tunafanya majadiliano.
Cathbert: Eeh nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P9: Baada ya hapo kuna Jamaa yangu aliniomba namba yangu ya simu na kila mtu akaendelea na shughuli zake
Cathbert: Unakumbuka nini kuhusu tarehe 5/4/2025?
Shahidi wa kificho P9 : Hiyo tarehe nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ya kuwa yeye ni mteja na anahitaji fundi Umeme wa kumfanyia kazi nyumbani kwake, na baada ya hapo nikamuelekeza nilipo ambapo akasema Sawa.
Cathbert: Eeeh nini kiliendelea
Shahidi wa kificho P9: Basi nkaenda sehemu tuliyopanga tuonane na nilivyofika akajitambulisha ya kuwa yeye ni Afisa wa Polisi na akanionyesha kitambulisho chake cha kazi na kusema anatokea kituo cha Polisi Mwanjelwa.
Cathbert: Eeh baada ya Utambulisho?
Shahidi wa kificho P9 : Aliniambia kwa sasa niko chini ya ulinzi kwa kosa la uchochezi na hivyo twende kituo cha Polisi
Cathbert: Eeh baada ya kufika kituo cha Polisi?
Shahidi wa kificho P9 : Alinikabidhi kituo cha Polisi ambako nilihojiwa na baadae jioni ndugu zangu walikuja kuniwekea dhamana na nikaambiwa natakiwa kuripoti kila siku ya ya Jumatatu
Cathbert: Unakumbuka nini kuhusu tarehe 22/4/2025?
Shahidi wa kificho P9: Nilipigiwa simu majira ya Asubuhi na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Askari Polisi na ninahitaji Kituo cha Polisi Mwanjelwa.
Part 208 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 206
Ubishani unaendelea kati ya Mhe. Lissu na Wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: Mshitakiwa kama aliandika kwenye maelezo yake kufanya vurugu na yeye akajibu kuzuia uchaguzi ndiyo kufanya vurugu zenyewe, namuomba shahidi atueleze alivosema kuzuia uchaguzi ndiyo kufanya vurugu alimanisha nini.
Mhe.Lissu: naomba mahakama imsomee record wakili labda itamsaidia kumuongoza vizuri.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashitaka bado mnasimamia hilo.
Wakili Mkude: kwasababu mshitakiwa amesema twende kwenye swali specific naomba tusomewe ili iweze kutuongoza.
Jaji Ndunguru : mshitakiwa aliuliza Mwenyekiti Tundu Lissu alisema “tukafanye vurugu" maneno hayo yapo kwenye statement yake D12 shahidi akaseme hayapo.
Wakili wa Serikali: sawa waheshimiwa Majaji, shahidi umeulizwa kuwa ulitakiwa kuripoti Polisi Kila baada ya siku tatu na ukaulizwa kama maneno hayo yapo kwenye maelezo yako ukajibuje?
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Wakili wa Serikali; shahidi kutoka kwenye kielelezo hicho soma mstari wa 12 kutoka juu.
Shahidi wa kificho P3 : ilipofika jioni walikuja ndugu zangu wakanidhamini huku nikitakiwa kuripoti Kila baada ya siku tatu.
Mhe.Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba niweke pingamizi kwa hilo swali, shahidi amezungumzia jambo la kuripoti mara mbili, mara ya kwanza ni alipochukuliwa maelezo ya kwanza na kudhaminiwa kwenye ushahidi wa leo amesema aliambiwa kuripoti kila baada ya siku tatu alipoandika maelezo ya mara ya pili, hakuna sehemu nyingine amezungumzia jambo hilo hivyo basi wakili anapaswa kuuliza katika maeneo hayo.
Jaji Ndunguru : Upande wa mashitaka.
Wakili wa Serikali: shahidi aliulizwa na akajibu na wote tumesikia.
Jaji Ndunguru : upande wa mashitaka kuna shida hapo.
Wakili wa Serikali: hapana shida Mheshimiwa Jaji.
Mahakama inaangua kicheko 😃😃😃
Wakili wa Serikali: Shahidi umeulizwa maswali mengi kuhusiana na kwamba kama wewe ni mwanachama wa CHADEMA, kama mshitakiwa anakufahamu, kama ulijiandikisha na kujiorodhesha. Shahidi wakati unajiunga na CHADEMA ni nani alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Jaji Ndunguru : wakili hilo ni swali jipya kabisa, tuzingatie record.
Mhe.Lissu: Mawakili kama hamna maswali si mnanyamaza.
Jaji Ndunguru : tuendelee. Shahidi umeshamaliza kutoa ushahidi wako Sasa unaweza kuondoka.
Wakili wa Serikali anasema wako na Shahidi mwingine ambae ni P9 huyu nae ni Shahidi wa kificho.
Anaingizwa kwenye kila kibanda umiza, naambiwa ukiingia mle ndani ya iko kibanda joto ni kali sana kama upo Sudan
Huyu P9 na ni Shahidi wa 14 wa Jamhuri
Umri - 35
Dini - Mkristo
Anapewa Bible then anakula kiapo.
Mkude Wakili wa Serikali anasema Wakili Cathbert Mbilinge atamuongoza P9 shahidi wetu.
Wakili Cathbert: Shahidi wewe ni mkazi wa wapi?
Shahidi wa kificho P9: mimi ni mkazi wa Mbeya na shughuli zangu ni za fundi Umeme na ninafanya mbeya yote kwa maana ya popote ntapohitajika.
Wakili wa Cuthbet : Ulikuwaje fundi Umeme
Shahidi wa kificho P9 : Nilipita chuo cha ufundi veta kusoma mafunzo ya Umeme 2008 to 2010 kwa Umeme wa viwandani na majumbani.
Cathbert: Shahidi unakumbuka nini kuhusu mwaka 2024 kwa mambo ya siasa
Shahidi wa kificho P9 : nakumbuka kwa masuala ya kisiasa kwa 2024 nilivutiwa na sera za Chama cha CHADEMA na hivyo nikawa mfuasi wa Chama.
Cathbert: Ulichukua hatua gani baada ya kuvutiwa na sera za Chadema?
Shahidi wa kificho P9 : Nilianza kufatilia kwa karibu shughuli, hotuba na mikutano ya CHADEMA.
Cathbert: Ni tukio gani ulilolifatilia kwa karibu?
Shahidi wa kificho P9 : nimefatilia matukio mengi ikiwemo maandamano ya Amani ambayo yalikuwa kutoka Uyole kwenda Kabwe, Isanga kwenda kabwe na Airport Songwe kwenda Kabwe.
Cathbert: Ni viongozi gani walioongoza hayo matukio
Shahidi wa kificho P9 : Kiongozi wa kutoka Uyole kwenda Kabwe alikuwa ni Lissu, Isanga kwenda kabwe alikuwa Heche na wa Airport Songwe kwenda Kabwe simkumbuki.
Part 207 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 205
Mhe. Lissu anaendelea na Cross Examination.
Mhe. Lissu: katika maelezo yako kuna sehemu yoyote umesema mwenyekiti Tundu Lissu amesema tufanye vurugu?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana hakuna hayo maelezo
Mhe. Lissu: unafahamu maana ya neno uasi.
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: Ngoja nikwambia, waheshimiwa majaji namsomea shahidi maana ya uasi kutoka katika kamusi ya Kiswahili…swali langu kaka, waeleze waheshimiwa majaji kwa kuwapinga wenye mamlaka au taratibu zilizopo ni uhaini?
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: Shahidi mimi ninasheria ya uchaguzi hapa ya urais, madiwani na ubunge, sheria hiyo haina popote iliposema kuzuia uchaguzi ni kosa la jinai, wewe unasemaje?
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: hapa nina sheria kuu ya makosa ya jinai na hakuna popote iliposema kuzuia uchaguzi ni kosa la jinai, wewe unasemaje?
Shahidi wa kificho P3 : mimi sijui.
Mhe. Lissu: umeeleza mahakama kwamba ulipokamatwa tarehe 4 april 2025 na kwenda kuandikwa maelezo kwa tuhuma za kupanga njama za kuzuia uchaguzi, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : kweli.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji hizo tuhuma ziliishia wapi?
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama umefunguliwa mashtaka ya jinai ya kupiga watu mawe na kupanga njama za kufanya vurugu
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: ulipaanga njama na mapolisi ujifanye mwanachadema uje kutoa ushahidi hapa?
Shahidi wa kificho P3 : si kweli
Mhe. Lissu: kama si kweli kwanini hujafunguliwa mashtaka
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: kwa muda wote wa miezi mitano uliyokua unaenda kuripoti polisi, walikua wanakwambia nini?
Shahidi wa kificho P3 : walikua hawaniambii chochote, wananiambia niende
Mhe. Lissu: waambie majaji kama wakati wote unaripoti polisi waliwahi kukuuliza chochote kuhusu tuhuma zako za kupiga watu mawe?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: nani alikulipia nauli ya kutoka Mbeya mpaka Dar es salaam
Shahidi wa kificho P3 : nimejilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: hapa Dar es salaam umefikia wapi?
Shahidi wa kificho P3 : nimefikia guest
Mhe. Lissu: nani anakulipia?
Shahidi wa kificho P3 : najilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama mpaka leo hii kuna kiongozi au mwanachama wa chadema aliyekutishia chochote juu ya maisha yako
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: waambie washeshimiwa majaji kama kuna kiongozi au mfuasi yoyote wa CHADEMA ametishia familia yako
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: Kuna polisi ameleta kiapo mahakamani akisema kwamba shahidi kama wewe umetishiwa maisha.
Shahidi wa kificho P3 : Hapana mimi sijawahi kutishiwa maisha.
Mhe. Lissu: sina maswali tena kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru : Re-examination upande wa mashitaka.
Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umeulizwa swali kuhusu huyo askari Polisi aliyekukamata, mheshimiwa Jaji naomba kielelezo, shahidi Sasa naomba usome kielelezo ukurasa wa mwisho mstari wa tatu.
Shahidi wa kificho P3 : wakati tunaendelea kubishana alikuja mtu aliyejitambulisha kwangu kuwa yeye ni Askari Polisi.
Wakili wa Serikali; kwa hiyo alijitambulisha kwako kuwa yeye ni?
Shahidi wa kificho P3 : kuwa yeye ni Askari Polisi.
Wakili wa Serikali: Shahidi umeulizwa swali na mshitakiwa kwamba kama kuna neno katika maelezo yako ‘kufanya vurugu’ ukajibu yapo, alivyokuonesha ukasema kuzuia Uchaguzi ndiyo kufanya vurugu zenyewe, sasa onesha uhusihano kati ya maneno kufanya vurugu na kuzuia uchaguzi.
Mhe.Lissu: waheshimiwa Majaji Sasa naona Wakili anataka kuelezea mambo ambayo shahidi ameyakataa, anataka kuintroduce kitu kipya.
Kama Mahakama itamruhusu kufanya hivyo nitaomba nimcross examine shahidi upya kwenye suala hilo.
Part 206 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 204
Mhe. Lissu anaendelea na Cross examination.
Mhe.Lissu: ulivosogea pembeni akakwambie twende kituoni ukatoe maelezo, waeleze waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo?
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Mhe.Lissu: badala yake yapo maneno yanayosema kwamba alikuja mtu aliyejitambulisha kuwa ni Askari Polisi na kunikakamata. Ni sahihi
Shahidi wa kificho P3 : ndiyo ni sahihi.
Mhe.Lissu: kwa hiyo hapakuwepo na maongezi alifika na kukukamata.
Shahidi wa kificho P3: sahihi
Mhe.Lissu: umesema ulipofika kituoni alikuweka mahabusu na baadae ukahojiwa kuwa unahamasisha uasi sasa waeleze waheshimiwa Majaji kama kuna maneno kwanini ulikuwa unahamasisha uasi.
Shahidi wa kificho P3: hapana hayapo.
Mhe.Lissu: Ahsante.
Mhe. Lissu: Twende tarehe 17 April 2025 waeleze waheshimiwa majaji kama katika maelezo yako kuna sehemu umesema kuwa aliyekuandika maelezo mwanzo ya terehe 4 april 2025 ndio aliyekuandika maelezo tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : Hayapo.
Mhe. Lissu: umesema ulipoandika maelezo mara ya pili akakwambia uendelee kuripoti kila baada ya siku tatu, yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana.
Mhe. Lissu: umesema kwamba wewe kazi yako ni dereva wa boda boda kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : kweli
Mhe. Lissu: waambie waheshimiwa majaji kama umeonyesha leseni
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe. Lissu: boda boda ni pikipiki kweli si kweli
Shahidi wa kificho P3 : Ni kweli
Mhe. Lissu: Umewaambia usajili wa hiyo pikipiki?
Shahidi wa kificho P3: Hapana
Mhe. Lissu: umewaonyesha waheshimiwa majaji kadi ya usajili wa hiyo pikipiki
Shahidi wa kificho P3: Hapana.
Mhe. Lissu: Shahidi naomba unisaidie, kwasababu kijiwe chako hatukijui kwasababu kimefichwa, kadi huna, leseni huna, je pikipiki umeleta?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: kwa hali hii kuna mtu ataweza kuthibitisha kwamba wewe ni dereva boda boda?
Shahidi wa kificho P3 : Mimi sijui.
Mhe. Lissu: unasema uliwahi kushiriki maandamano aliyowahi kuongozwa na Mbowe, ulijiandikisha sehemu yoyote.
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: Hata uliwahi kupigwa picha ukiwa kwenye maandamano hayo.
Shahidi wa kificho P3 : hata sijui
Mhe. Lissu: Unasema uliwahi kushiriki katika kongamano la vijana, uliwahi kujiandikisha?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: Uliwahi hata kujiandikisha kwa viongozi wa BAVICHA Mkoa wa Mbeya?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana.
Mhe. Lissu: sasa kwanini tusiseme wewe ni pandikizi la akina Kingai na mapolisi wake.
Shahidi wa kifichoP3 : Kimya
Mhe. Lissu: unasema ulishiriki mkutano wangu, ulijiandikisha popote?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: sasa weleze waheshimiwa Majaji wataamini vipi kuwa wewe ni mfuasi wangu na mwanachama wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : Mimi sijui sasa, kama unanikataa mm sio mfuasi wako sawa.
Mhe. Lissu: sikukatai kaka, mimi sikujui na ninaogopa watu wasiojulikana kwasababu wanateka watu, wanabambikia watu kesi na kuua kwahiyo tutajua kama sio wewe mmoja wapo?
Shahidi wa kificho P3 : mimi sijui.
Mhe. Lissu: umesema ulikua na vijana wenzako kijiweni ukiwashawishi, waeleze waheshimiwa majaji kama umetaja orodha yao na majina yao.?
Shahidi wa kificho P3 : sijawataja.
Mhe. Lissu: Umeeleza kwamba ulikamatwa na askari Polisi, umemtaja kwa jina huyo askari polisi? Au hata namba yake tu na cheo je?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: tunaendelea, ninachukizwa na nyie mapandikizi ya polisi mnaletwa hapa halafu mnafichwa ndani ya kizimba, ngoja tuendelee.
Mhe. Lissu: unasema mlifikia uamuazi wa kupiga watu mawe watakaoenda kupiga kura, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : kweli
Mhe. Lissu: na huo ulikua ni uamuzi wako binafsi, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : Lakini kutoka na ushawishi wako.
Mhe. Lissu: kuna mahali popote katika maelezo yako umesema Mwenyekiti Tundu Lissu amesema tupige watu mawe?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Part 205 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 203
Mhe. Lissu anaendelea na Cross Examination,
Jaji Ndunguru: upande wa mashitaka.
Mkude: No objection.
Jaji Ndunguru : turejee kifungu 194 cha CPA.
Mkude: kifungu cha 194 kwa ujumla wake ni kuhusu protection ya ushahidi, kwa sababu shahidi au mshitakiwa anaweza akaomba impeachment, pale anapoomba shahidi apewe kielelezo hivo tunaweza kuendelea mheshimiwa Jaji.
Mhe.Lissu: Iko hivyo waheshimiwa Majaji, sikuwa nataka kuona jina lake kwenye kielelezo hicho bali nataka asome maelezo yake.
Mhe.Lissu: kwa hiyo shahidi ulitaka kuficha ukweli mahakamani.
Shahidi wa kificho P3 : hapana.
Mhe.Lissu: mbona haukusoma kama wewe ni mwanachama wa CHADEMA na umeiandika kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : mimi ni mfuasi wa CHADEMA labda askari aliyeandika maelezo yangu alikosea.
Mhe.Lissu unaidanganya mahakama, soma kama ilivoandikwa.
Shahidi wa kificho P3 : mimi ni mfuasi/ mwanachama wa CHADEMA.
Mhe.Lissu: Sasa ulikuwa unaficha nini. Shahidi swali langu la pili kwenye maelezo yako umesema kongamano hilo halikufanyika kwa sababu tulitawanywa uwanjani.
Sasa waeleze waheshimiwa Majaji kama kwenye maelezo yako kuna sehemu umeandika kuwa kongamano hilo halikufanyika kwa sababu tulitawanywa uwanjani.
Shahidi wa kificho P3 : kongamano hilo halikufanikiwa.
Mhe.Lissu: hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Mhe.Lissu: shahidi umesema kwa bahati mbaya au nzuri kongamano hilo halikufanyika lilizuiliwa na serikali kweli au si kweli.
Shahidi wa kificho P3 : kweli.
Mhe.Lissu: wewe mfuasi wa CHADEMA kongamano la CHADEMA shughuli halali ya chama kuzuiliwa kwako ni bahati nzuri.
Shahidi wa kificho P3: sijui, mimi sielewei
Mhe.Lissu: ndiyo maana nikakuuliza tutajuaje kama wewe siyo pandikizi.
Shahidi wa kificho P3 : hilo swali nimeshalijibu tuendelee.
Mhe: Lissu: usijali tutaendelea kwenye maelezo yako ya Leo umesema ulikuwa na simu, Sasa kwenye hayo maelezo yako ya Polisi kuna sehemu uliandika kama ulikuwa na simu.
Shahidi wa kificho P3 : haipo.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama unajua au haujui kuwa unaweza kufuatilia YouTube kwa kutumia compyuta.
Shahidi wa kificho P3 : sijui, mimi sina utaalamu huo wa kutumia compyuta.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama unajua kuwa unaweza kufuatilia YouTube kwa kutumia Television.
Shahidi wa kificho P3 : utaalamu huo sina.
Mhe.Lissu: unajua kama unaweza kufuatilia YouTube kwa kutumia tablet.
Shahidi wa kificho P3 : sijui huo utaalamu.
Mhe.Lissu: Kwenye maelezo yako kuna sehemu umeandika kuwa ulikuwa na simu
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe.Lissu: kwenye maelezo yako umesema uliyasikia maneno yangu kupitia video YouTube, kuna mashahidi wengine wamesema video hiyo ilikuwa na masaa 3 na madakika, waeleze waheshimiwa Majaji kama kuna sehemu umeandika video hiyo ilikuwa na muda gani.
Shahidi wa kificho P3 : hakuna
Mhe.Lissu: umesema umemfahamu mheshimiwa Lissu kupitia mitandao ya kijamii. Waeleze waheshimiwa Majaji kama kwenye maelezo yako umeandika hilo jambo.
Shahidi wa kificho P3 : hapana hayapo.
Mhe.Lissu: umesema mwezi march 2025 ulihudhuria mkutano uliohutubiwa na Mheshimiwa Tundu Lissu katika viwanja vya Ruanda nzovwe, waeleze waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3: hayapo
Mhe.Lissu: umesema wakati ukiwahamasisha vijana wenzako hapo kijiweni alikuja mtu aliyejitambulisha kuwa ni Askari Polisi na kukuita pembeni kwamba njoo tuongee, waeleze waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : napitia kidogo
Mhe.Lissu: haujapaona hadi mwishoni kwenye paragraph ya mwisho.
Shahidi wa kificho P3 : naomba nikusomee, alikuja mtu aliyejitambulisha ni Askari Polisi.
Mhe.Lissu: swali langu ni kwamba hayo maneno akaniita pembeni akaniambia njoo tuongee, hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P3 : hayapo.
Part 204 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 202
Mhe. Lissu ameanza kumfanyia Cross examination Shahidi wa kificho P3.
Mhe. Lissu: shahidi hapo ulipo unaweza kuniona?
Shahidi wa kificho P3 : hapana
Mhe. Lissu: kwa taarifa yako hata mm siwezi kukuona kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : sahihi.
Mhe. Lissu: nataka nikuhoji kutokana na ushahidi wako na nashukuru umesema wewe ni mfuasi wa CHADEMA, sasa naomba uwaeleze majaji, mfuasi wa CHADEMA anakua na kutambulisho gani?
Shahidi wa kificho P3 ; anakua hana kitambulisho kwasababu anakua bado hajawa mwanachama.
Mhe. Lissu: mimi kiongozi wa CHADEMA na mtu yoyote aliyeopo hapa mahakamani atajuaje kama wewe ni mfuasi wa CHADEMA, huna kitambulisho na pia sikuoni?
Shahidi wa kificho P3 : hilo ni suala la imani
Mhe. Lissu: twende taratibu kaka, waeleze majaji kama wafuasi wa chadema huwa wanaorodheshwa mahali ili kuwatambua.
Shahidi wa kificho P3 : binafsi sijajua huwa wanaorodheshwa wapi?
Mhe. Lissu: kwahiyo hujaorodheshwa?
Shahidi wa kificho P3 : sahihi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama wafuasi wa CHADEMA kuna mahali huwa wanaenda kujitambulisha ili wajulikane
Shahidi wa kificho P3 : hakuna.
Mhe. Lissu: hapo ulipo kwenye kiboksi na mimi hapa nilipo kama kuna namna mimi naweza nikaelewa au kujua kama wewe ni mfuasi wa CCM na sio CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : sijui utajuaje ila mm ni mfuasi wa CHADEMA
Mhe. Lissu: na nitajua kama ww sio pandikizi la Polisi kwasababu hujajiandikisha popote wala huna chochote cha kukutambulisha kuwa ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3 : itabidi uamini tu na uiamini mahakama tukufu kwasababu mimi sijui kwa kweli utawezaje kunitambua.
Mhe. Lissu: mfusi wa CHADEMA huwa anaalama usoni au kifuani kuwa yeye ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P3: sijui
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama uliandika maelezo Polisi tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : ndio
Mhe. Lissu: ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P3 : ndio
Mhe. Lissu: naomba shahidi apewe maelezo yake ya tarehe 17 april 2025.
Mkude: Hatuna pingamizi.
SHAHIDI ANAPEWA MAELEZO YAKE.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama hayo ndio maelezo uliyoyaandika tarehe 17 april 2025?
Shahidi wa kificho P3 : ngoja kidogo nayapitia.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama hayo ni maelezo yako?
Shahidi wa kificho P3 : ndio yenyewe
Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji nataka ku-impeach credit ya shahidi huyu, nitamsomea maelezo yake, nitaonyesha maeneo ambayo nataka kumhoji halafu nikimaliza nitakuomba uyawasilishe kama kielelezo.
Shahidi wa kificho P3 : sawasawa.
Mhe.Lissu: anamsomea shahidi maelezo yake.
Mhe.Lissu: waeleze waheshimiwa Majaji kama nilichokisoma ndicho kilichoko kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P3 : ndiyo ulichokisoma ndicho kilichoko kwenye maelezo yangu.
Mhe.Lissu: Sasa shahidi nataka nikuhoji kwenye eneo unalosema wewe ni mfuasi wa CHADEMA na maeneo mengine kadri nitakavyokuhoji kutokana na ushahidi wako.
Mheshimiwa Lissu anamsomea shahidi maeneo yote anayotaka kumhoji.
Maeneo 8.
Mhe.Lissu: Sasa hili nikuhoji sawasawa naomba uwaeleze waheshimiwa Majaji kama ungependa maelezo yako yapokelewe kama kielelezo mahakamani.
Shahidi wa kificho P3: ndiyo napendelea iwe hivyo.
Mhe.Jaji: itakuwa D12
Mhe.Lissu: ahsante waheshimiwa Majaji, naomba shahidi apewe kielelezo D12
Mhe.Lissu: Sasa swali langu la kwanza ni kwamba kwenye ushahidi wako leo umeieleza mahakama kuwa wewe ni mfuasi wa CHADEMA tangu mwaka 2021, ni kweli au si kweli.
Shahidi wa kificho P3 : ni kweli.
Mhe.Lissu: kwenye kielelezo D12 wasomee waheshimiwa Majaji pale unapoanzia mimi pia ni........ endelea hadi nitakapokwambia inatosha.
Shahidi wa kificho P3 : mimi pia ni mfuasi wa chama hicho.....
Shahidi anasitasita katika kusoma.
Mhe.Lissu: naomba pia nipewe kielelezo hicho naona kama shahidi anatupoteza.
Part 203 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 201
Anasimama Wakili wa Serikali Mkude anasema tunashahidi mwingie wa kulindwa ni P3,
Mpaka sasa huyu ni shahidi wa 13.
Shahidi ameingia kwenye kijumba cha mbao tayari.
Sasa anajitambulisha.
Shahidi wa kificho P3 : Nina miaka 35
Shahidi wa kificho P3: dini yangu muislamu
Shahidi wa kificho P3: naishi halmashauri ya Mbeya mjini, mtaa wa Mwamtengule kata ya Syesye
Shahidi wa kificho P3: najishughulisha na kazi ya dereva boda boda
Shahidi wa kificho P3: shughuli zangu nafanyia katika halmashauri ya jiji la Mbeya.
Shahidi wa kificho P3: nina miaka nane tangu naendesha boda boda
Shahidi wa kificho P3: mimi ni mfuasi wa CHADEMA
Shahidi wa kificho P3: nimekua mfuasi tangu 2021 mpaka sasa bado ni mfuasi
Shahidi wa kificho P3: nimewahi kushiriki matukio baadhi kama kongamano la kutoka Mbalizi mpaka Kabwe tulipoenda kumpokea Mhe. Mbowe mwaka 2024.
Tukio lingine ni kongamano la vijana lakin bahati mbaya au nzuri hatukufanikiwa kwasababu serikali ilizuia.
Shahidi wa kificho P5: tarehe 4 april 2025 nakumbuka kijiweni kwangu kwenye boda boda nilikua nachezea simu yangu nikapata kuona hotuba fupi ambayo Mhe. Tundu Lissu akizungumzia uchaguzi uliopangwa kufanyika 2025.
Shahidi wa kificho P3 : hotuba niliiona youtube.
Shahidi wa kificho P3 : namfahamu Tundu Lissu kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuwa nafatilia sana chama cha CHADEMA tangu mwaka 2021.
Katika chama Tundu Lissu ni mwenyekiti wa CHADEMA, baada ya kusikiliza ile hotuba pale kijiweni nikaanza kuwashirikisha wanachama wenzangu wa boda boda na kuanza kuwashawishi wengine wenye mapenzi na CHADEMA kufanya yale mh. Tundu Lissu ameyasema.
Niliwashawishi tuwe kitu kimoja kupambana kuzuia uchaguzi 2025, tulipanga kuzuia uchaguzi kwa namna ya kwamba watu watakaoenda kupiga kura kuwafanyia fujo ikiwepo kupigwa mawe, ushawishi nilikua naufanyia katika kijiwe changu cha pikipiki, baada ya kushawishi wenzangu kuna baadhi waliliridhika na ushawishi wangu na baadhi hawakuridhika.
Shahidi wa kificho P3 : baada ya hapo alitokea mtu mmoja akanipoint kwenye kijiwe na akaniomba tuongee mara moja, nikaenda kumsikiliza na akajitambulisha kuwa. Yeye ni ofisa wa polisi, akaniambia nahitajika twende kituo cha polisi kwa mahojiano yangu mimi na yeye nilivyofika kituo cha polisi wakaniambia nitoe viatu na mkanda na wakaniweka mahabusu.
Wakili: Shahidi P3 baada ya kukaa mahabusu nini kilifuata
Shahidi wa kificho P3 : baada ya muda mchache nikapelekwa kwenye chumba kingine wakaanza kunihoji kwamba nilikuwa naongea nini pale kijiweni, kwanini nilikuwa nahamasisha kufanya uasi.
Wakili: walikuuliza kwa nini unahamasisha uasi gani kama unakumbuka.
Shahidi wa kificho P3: kwanini nahamasisha uasi wa kuzuia uchaguzi wa 2025.
Wakili: Sasa shahidi baada ya maelezo hayo nini kilifuatia.
Shahidi wa kificho P3: waliniambia nitafute mtu wa kunidhamini ili niweze kuendelea na taratibu nyingine.
Wakili: ikawaje.
Shahidi wa kificho P3: nilimpata ndugu yangu akaja kunidhamini.
Wakili: nini kilifuata
Shahidi wa kificho P3: nilipata ndugu yangu akaja kunidhamini. Nikaambiwa niwe naripoti Kila baada ya siku tatu.
Wakili: ulikuwa unaripoti wapi.
Shahidi wa kificho P: nilienda kuripoti Kituo cha Polisi Ilonga.
Wakili: ulivoenda kuripoti ikawaje.
Shahidi wa kificho P3: nikaingia ndani kituoni na kukutana na huyo askari aliyeniandika maelezo toka mwanzo.
Wakili: huyo Askari aliyekuandika maelezo kutoka Mwanzo anaitwa nani kama unakumbuka.
Shahidi wa kificho P3 : namkumbuka kwa jina moja anaitwa Amani.
Wakili: baada ya kukutana na Amani mlifanya nini.
Shahidi wa kificho P3: aliniandika maelezo tena na kuniambia naendelee na utaratibu wa kuripoti.
Wakili: waheshimiwa Majaji wa Mahakama kuu kwa Shahidi huyu ni hayo tu
Part 202 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 200
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi Coplo Vicent.
Mhe. Lissu: waeleze wahesimiwa majaji kama kuna mtu yoyote alishuhudia ukiandiika hayo maelezo
Shahidi Coplo Vicent : hakuna niliandika mm mwenyewe
Mhe. Lissu: uliambiwa na OCS ukamkamate P9 kwamba anahamasisha watu kuchochea na kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025, waeleze waheshimiwa majaji ulimkamata kwa kosa gani?
Shahidi Coplo Vicent: wakati namkamata alikua hafanyi kosa lolote.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama kwenye maelezo yako umetaja jina la mkuu wa kituo cha polisi Mwanjelwa?
Shahidi Coplo Vicent : hapana
Mhe. Lissu: kwenye maelezo yako umeeleza mahali popote kwamba huyu P9 alifanya makosa katika sehemu mbalimbali na majina yake?
Shahidi Coplo Vicent ; hapana
Mhe. Lissu : naomba kamusi, tuangalie neno “kijiwe” kwasababu umelitaja nataka tujue kijiwe maana yake nini kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili. Sasa jiji la mbeya lina vijiwe vingapi?
Shahidi Coplo Vicent: sifahamu.
Mhe. Lissu: waambie waheshimiwa majaji kama umetaja hivyo vijiwe?
Shahidi Coplo Vicent : sijataja
Mhe. Lissu: tarehe ya P9 aliyofanya makosa
Shahidi Coplo Vicent : ni tarehe 5 april
Mhe. Lissu: eleza kama umeeleza hayo kwenye maelezo yako.
Shahidi Coplo Vicent : anasoma
Mhe. Lissu: kwa akili yako hicho ulichosoma kinaonyesha alifanya makosa lini?
Shahidi Coplo Vicent : Hapana
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama kwenye maelezo yako umeeleza huyu P9 alikua anapanga njama na nani kwasababu njama haipangwi na mtu mtu mmoja?
Shahidi Coplo Vicent : sijaeleza
Mhe. Lissu: waeleze majaji kwa ufahamu wako kuna kosa la kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike?
Shahidi Coplo Vicent : kosa lipo
Mhe. Lissu: kwa sheria gani au kwasababu wewe ni polisi.
Shahidi Coplo Vicent : mm sijui lkn hapo kosa lipo
Mhe. Lissu: acha ubabaifu nakuonyesha sheria ya uchaguzi wa rais, madiwani na wabunge ya 2024, hii haina sehemu yoyote kama hiyo unachokisema ni kosa, wewe unasemaje?
Shahidi Coplo Vicent : mimi sijui.
Mhe. Lissu : na kwenye sheria ya jinai Penal Code je?
Shahidi Coplo Vicent: Kwenye Penal Code lipo
Mhe. Lissu : waheshimiwa naomba shahidi asome hiyo sheria na atuonyeshe hilo kosa.
Renatus Mkude: shahidi hii sheria ni ya kiingereza sasa utaweza kuona?🤣🤣
Mhe. Lissu: Naomba Penal code yangu tusipotezeane muda kingereza hujui na hilo kosa hutaliona.
Mhe. Lissu : waeleze majaji baada ya kumpeleka P9 kituoni ulisema uliendelea na shughuli zako, waambie. Majaji kama unafahamu huyu P9 hajapelekwa mahakamani mpaka leo
Shahidi Coplo Vicent : sifahamu
Mhe. Lissu: utashangaa nikikwambia kwamba baada ya kukamatwa aligeuzwa kuwa shahidi katika kesi hii
Shahidi Coplo Vicent : siwezi kujua.
Mhe.Lissu: Je unafahamu kama P9 ni shahidi katika kesi hii na utashangaa nikikwambia hakufunguliwa mashitaka yeyote badala yake amegeuzwa shahidi katika kesi hii.
Shahidi Coplo Vicent : sifahamu
Mhe.Lissu: je unafahamu kosa ninaloshitakiwa nalo.
Shahidi Coplo Vicent : ndiyo unashitakiwa kwa kosa la uhaini, kutokana na matendo yako.
Mhe.Lissu: matendo yangu yapi.
Shahidi Coplo Vicent: nayafahamu machache kutokana na kauli zako, ninazifahamu chache.
Mhe.Lissu: mitandaoni kuna kauli zangu nyingi sana, kuna video nyingi mno ni zipi hizo chache unazozifahamu.
Shahidi Coplo Vicent : yaani uchaguzi wa mwaka huu daaah!!!!!
Mhe.Lissu: je umeiswailisha video hiyo ili Majaji waione
Shahidi Coplo Vicent: hapana sijaiwasilisha.
Mhe.Lissu: waheshimiwa Majaji kwa upande wangu sina maswali zaidi.
Mhe.Jaji: upande wa mashitaka re-examination.
Wakili wa Serikali: shahidi eleza onyo katika maelezo huwa inatumikaje.
Shahidi Coplo Vicent : huwa inatumika kumuonya mtuhumiwa.
Wakili: wewe unaruhusiwa kusaini mwenyewe.
Shahidi Coplo Vicent: ndiyo naruhusiwa.
Wakili: ni hayo tu mheshimiwa.
Mhe.Jaji: shahidi unaruhusiwa kuondoka.
Shahidi anavuta pumzi kubwa kisha anaondoka.
Part 201 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 199
Mhe. Lissu anaendelea na Cross examination.
Mhe.Lissu: Sasa shahidi naomba uwaeleze waheshimiwa Majaji kama niliyoyasoma yanalingana na maelezo yako ya police.
Coplo Vicent: ndiyo yanalingana.
Mhe.Lissu: Sasa shahidi naomba nikupitishe kwenye Maeneo ambayo nataka nikuhoji.
Mheshimiwa Lissu anamsomea shahidi maeneo anayotaka kumhoji.
Mhe. Lissu: ili niweze kukuhoji sawasawa waeleze waheshimiwa Majaji kama ungependa maelezo yako yapokelewe kama kielelezo.
Coplo Vicent: kwa jinsi ambavyo umenihoji naomba nisahihishe kwanza, naomba nirekebishe.
Mhe.Lissu: bado sijaanza kukuhoji, tutafika huko kubali kwanza maelezo yako yapokelewe.
Coplo Vicent: sawa nakubali yapokelewe kama kielelezo.
Mhe.Jaji: itakuwa D11
Mhe.Lissu: sawa mheshimiwa.
Mhe.Lissu: mheshimiwa Jaji naomba shahidi apewe kielelezo D11
Mhe.Lissu: Sasa shahidi hicho ni kielelezo mahakamani na swali la kwanza katika ushahidi wako Leo umesema wewe ni Askari police na unafanya kazi katika kituo cha Polisi Central Mbeya,
Sasa katika hayo maelezo yako naomba uwaambie waheshimiwa Majaji kama kuna sehemu umeandika kuwa unafanya kazi katika kituo cha police Central Mbeya
Coplo Vicent: hapa hakuna.
Mhe.Lissu: Shahidi swali langu la pili linahusu matukio ya tarehe 5 mwezi wa 4 mwaka jana, katika ushahidi wako unasema uliitwa na Mkuu wa kituo cha Polisi Mwanjelwa na kukuelekeza kwamba ukamkamate P9 kwa kuwa anahamasisha kwenye vijiwe mbalimbali na kuchochea uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike. Nataka nijue kama huo ndiyo ushahidi wako.
Coplo Vicent: bila shaka.
Mhe.Lissu: nataka uangalie kwenye maelezo yako uyasoke kuanzia pale unapoelekezwa ukamkamate P9, kama kuna maneno kwamba P9 alikuwa anahamasisha kwenye vijiwe mbalimbali uchaguzi mkuu usifanyike nataka kujua kama maneno hayo yapo.
Coplo Vicent : yapo.
Mhe.Lissu: naomba usome kuanzia hapo kwenye nakumbuka......
Coplo Vicent anasoma.
Mhe.Lissu: hayo maneno anahamasisha na kuchochea Uchaguzi Mkuu usifanyike hayo maneno yapo?
Coplo Vicent: hiyo haipo.
Mhe.Lissu: ahsante sana
Mhe.Lissu: Sasa shahidi kwenye ushahidi wako umesema baada ya kujitambulisha kwake wewe ni Polisi ulimuonesha kitambulisho chako, na ukaongozana nae hadi kituo cha Polisi Mwanjelwa. Kweli au si kweli.
Coplo Vicent: kweli
Mhe.Lissu: waambie Majaji kama hayo maneno yapo.
Coplo Vicent: Hayapo.
Mhe.Lissu: Sasa shahidi naomba uwaambie waheshimiwa Majaji ni nani aliyeandika maelezo yako.
Coplo Vicent : niliandika Mwenyewe.
Mhe.Lissu: shahidi waeleze waheshimiwa Majaji kama wakati wa kuandika maelezo huwa kuna sehemu ya onyo.
Coplo Vicent : huwa hakuna onyo.
Mhe.Lissu: hakuna Yale maneno kuwa nitasema ukweli, ukweli mtupu nikisema uongo nishitakiwe.
Coplo Vicent : hyo siyo onyo.
Mhe.Lissu: hiyo huwa ni nini.
Coplo Vicent : huwa ninajiambia nitasema ukweli, najiandika maelezo.
Mhe.Lissu: huo ndo utaratibu wenu Mapolisi, mnajiambia wenyewe.
Mhe.Lissu: unaifahamu PGO.
Coplo Vicent : ndiyo
Mhe.Lissu: shahidi unaifahamu PGO number 236.
Coplo Vicent: siifahamu.
Mhe.Lissu: Mhe.Jaji naomba shahidi apewe PGO
Mhe.Lissu: Shahidi soma PGO 236.
Coplo Vicent : hii PGO ni ya kingereza siwezi kusoma.
Mhe.Lissu: Wambura ameandika kingereza anaamimi nyote mnajua kingereza kwahiyo huwezi kusoma kwa sababu ni kingereza.
Coplo Vicent : kuna ya kiswahili.
Mhe.Lissu: ujue kingereza au usijue swali langu utalijibu. Naomba PGO yangu.
Mhe.Lissu: shahidi kwenye kielelezo D11 pale mwishoni kuna udhibitisho wa majina yako na sahihi yako. Umeyaona hayo maneno
Coplo Vicent: Hayapo hayo maneno.
Mhe.Lissu: Mheshimiwa Jaji naomba shahidi aoneshwe sehemu ya udhibitisho wake kwenye D11, kifungu cha 10.3.C
Coplo Vicent: wapi, hapa mwisho kabisa au.
Mhe.Lissu: kipindi unaandika haya maelezo kulikuwepo na kufungu cha 10.3.C
Coplo Vicent : ndiyo kulikuwepo mwaka Jana.
Mhe.Lissu: ni nani alikushuhudia wakati ukiandika maelezo yako
Coplo Vicent : hakuwepo mtu yeyote
Part 200 itaendelea post inayofuata,
Naomba repost
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 198
Anaingia jamaa mmoja mrefu, kavaa kaundasuti nyeusi anakitambi ila sio mnene wala mwembamba anaingia hapa.
Jaji anauliza Shahidi unaitwa nani?
H937 Detective Vincent
36 umri,
Mkristo,
Anapewa biblia kwa ajili ya kuapa anasema atasema Ukweli, Ukweli mtupu. 😂
Ataongozwa na wakili wa Serikali hapa.
Wakili: anauliza jina na anapoishi?
Coplo Vincent.: Anajitambilisha na anasema anaishi Mbeya.
Wakili: Sehemu gani?
Coplo Vincent : Anasema Mbeya mjini.
Wakili: Unafanya kazi gani?
Coplo Vincent : Police Wilaya ya Mbeya
Tangu mwaka 2012.
Wakili: Umejiunga mwaka gani?
Coplo Vincent.: Anajibu 2012
Mafunzo ya awali ya upolice kule Moshi 30/3/2012 baada ya kuhitimu nilipangiwa Mkoa wa Rukwa.
Wakili: Majukumu yako ya kila siku ni yapi?
Coplo Vincent: kupeleleza kesi kukamata na kutoa ushahidi Mahakamani katika kitengo cha upelelezi nina miaka Miaka 6.
Wakili: Sasa ieleze Mahakama mnamo Tarehe 5/4/2025 ulikua wapi?
Coplo Vincent : Nilikua kituoni Mwanjelwa naendelea na majukumu yangu.
Wakili: Unakumbuka Nini?
Coplo Vincent : Niliitwa na Mkuu wa kituo na kupewa maelelekezo ya kumtafuta P9.
Wakili: Alikua anakabiliwa na nini mpaka uende kumtafuta?
Coplo Vincent : P9 alikua anahamasisha vijiweni uchaguzi 2025 usifanyike hivyo nikaenda kumkamata.
Wakili: Baada ya kupewa maelekezo hayo ulifanyaje?
Coplo Vincent : Mkuu wa kituo alinipatia namba ya simu ya P9, Mkuu wa kituo hizo namba alizipata kupitia msiri wake ambaye alimletea.
Wakili: nini kiliendelea baada ya kupata mawasiliano ya mtu unayetakiwa kumkamata.
Coplo Vincent: baada ya kufuatilia shughuli zake nikagundua kuwa ni fundi umeme, hivyo nikatumia njia ya kujifanya kama mteja ili niweze kumkamata.
Wakili: nini kilifata?
Coplo Vincent: tulikubaliana kukutana maeneo ya kabwe ili niweze kumpeleka eneo la kazi.
Wakili: nini kilifuatia?
Coplo Vincent : baada ya hapo nikawa nimefika Kabwe kwani hapakuwa mbali, kweli nikakutana nae.
Wakili: baada ya kukutana nae nini kilifuatia.
Coplo Vincent : Nilimwambia mimi shida yangu siyo umeme, nikajitambulisha kuwa mimi ni Askari police nikamuonesha kitambulisho changu.
Wakili: baada ya kuonesha kitambulisho nini kilifuata?
Coplo Vincent : Nilimwambia nimekuja kumkamata anakabiliwa na tuhuma za kufanya uchochezi pamoja na kuhamasisha vurugu za kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Mwisho wake ulikuwaje.
Coplo Vincent: bahati nzuri alikuwa muelewa, sikutumia nguvu nyingi hakuwa mtu wa vurugu niliongozana nae hadi kituo cha police kati Mbeya then nikaendelea na majukumu yangu.
Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka anasema Waheshimiwa Majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.
Jaji anasema karibu Mshitakiwa kwa ajili ya maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu: umesema unaitwa Coplo Vicent ni sawa?
Coplo Vincent : Mimi naitwa coplo H937 vicent.
Mhe. Lissu; ukienda kwa baba yako na mama yako utawaambia unaitwa coplo H937 Coplo Vicent.? 😂
Coplo Vincent: Hapana.
Mhe. Lissu: nasikia wewe ni homeboy wangu.
Coplo Vincent: Ni kweli.
Mhe. Lissu: bila shaka uliandika maelezo yako ya shahidi na ukionyeshwa utayatambua?
Coplo Vincent: ndio.
‘Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake.
Mkude: waheshimiwa hatuna pingamizi.
Shahidi Coplo Vincent anaonyeshwa maelezo yake.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maelezo ni yako.
Coplo Vincent: ni sahihi ni yangu.
Mhe. Lissu: waheshimiwa nataka ku-impeach credit ya huyu shahidi nataka kuhoji sifa au uaminifu wake, namsoea maelezo yake kisha nitasoma maeneo nayotaka kum-contradict na nitaomba akubali yapokelewe kama kielelezo.
Part 199 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 197
Katuga anasema: Kuna chama kinasema lazima mashahidi wote wa kificho watajulikana, sisi ni rai yetu kwamba ipo siku hata mimi nitakuja kuambiwa nilishawahi kuwa shahidi wa kificho, kwahiyo tunaomba mahakama itolee maamuzi ili kuondoa shida ya kupunguza uaminifu wa mahakama;
Wengine ni mawakili kabisa wanazungumzia hii kesi kwa upotoshaji tena ni wanasheria wakubwa kabisa wanaheshimika katika jamii.
Mhe. Lissu anasimama: waheshimiwa majaji mimi nawaomba msikubali huo mualiko mnaopewa na mawakili wa serikali, malalamiko yao ni malalamiko ya kijinai ambayo hayajafanyika mbele yenu, hamjayaona, hamjayasikia na wala hamjaambiwa ni kitu gani, Hayo mambo yote hayajatokea mbele yenu mahakama ikiwa inaendelea.
Mkiambiwa mtolee maamuzi juu ya mambo hayo mtakua mmefungua mambo yasiyowezekana.
Kama wanahisi kuna jinai waende kwenye mahakama proper wakafungue kesi, kama ni mawakili kuna utaratibu wa kudeal na mawakili wanaokiuka taratibu za kiuwakili.
Kwahiyo mnaalikwa kwenye uwanja ambao hauna rules, sio uwanja wa kisheria.
La mwisho na hii ni hofu yangu wanataka giza katika kesi kubwa kama hii, kwenye kesi ya uhaini hawataki kuwe na mjadala wanazungumzia Umma kitu ambacho hakiwezekani, mnataka kuwafunga, mtafunga nchi nzima na hamtaweza. Ni hayo tu waheshimiwa.
Katuga anasimama: tuliialika mahakama chini ya kifungu 114, sisi tunasisitiza vinavyoendelea ni kutoa uthibitisho wa mashahidi wa kificho na sisi inatupa shida katika kuleta mashahidi wetu, tusipovisema ivi vitu proceedings hazitakuwa sawa.
Kuna vingine hatuvisemi kwanini mashahidi hawaji yeye anaulizia kila siku lakini ni vitu kama hivyo.
Katuga anadai hizi proceedings za kinachondelea Mahakamani zinachapishwa pia mtandaoni sasa hii haiwezi kuwa sawa.😂
Mawakili wa Serikali wanataka kesi iwe Gizani mazima ili Watanzania na Dunia isijue nini kinaendelea kwenye shauri hili.
Kwa kifupi hawa ndugu wmaechanganyikiwa na mambo yanavyokwenda. Wanaona wako uchi kabisa. Kila kitu chao kiko hadharani. Naona hapa wanataka kusema mashahidi wanagoma kuja kwasababu wanaogopa kuwekwa hadharani.
Nafikiri wangekuwa wakweli waseme mashahidi wanaogopa kudhalilishwa hata kama hawaonekani kwenye kile kibox chao. Naona joto la mle kwenye mambao ukichanganya na maswali wanahadisiana huko waliko. 😂😂
Kumbuka hizo discussion Majaji wamesema wanazifanya off record kwanza. Ni kama zinapigwa soga ili kuona ni vitu vya msingi au sio vya msingi. 😂
Majaji wamemaliza kuteta sasa.
Jaji Nduguru anasema amesikia hoja zote anasema siku zote anasisitiza Matumizi ya kifungu 114 kama kunamambo hayako sawaa hawawezi kusubiri mtu aliibue jambo hilo. Wao pia wanaona na watachukua hatua.
Hivyo anaendelea kusisitiza kifungu Cha 114 na kusema tujiepushe na uvunjifu wa kifungu hicho.
Matumizi ya kifungu Cha 114 ni domain ya Mahakama itatumia kifungu hicho endapo itaona kunaulazima wa kukitumia hivyo tuendelee mashahidi.
Wakili wa Serikali anasemaa anasema tuendelee na mashahidi Leo ni shahidi wa wazi wa 12 wa upande wa mashitaka.
Kwa Maneno mengine tukitafsiri kilichosemwa na Majaji ni kwamba wamewaambia Jamhuri acheni umbea. Fanyeni Kesi. Msitufundishe kazi. Tunajua tunachofanya. 😂😂😂
Wamenywea sana hapa.
Ngoja tukomae na huyo Polisi anaekuja muda huu.
Part 198 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 19, 2026
Jana tuliishia Part 195 so leo tunaendelea na-;
Part 196
Majaji na mtuhumiwa ndio wanaingia ndani ya Chumba cha Mahakama almaarufu Ukumbi Na. 1 hapa Mahakama Kuu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, John Heche alifika mapema sana hapa Mahakamani majira ya saa 3 asubuhi.
Jaji anamuita kalani asome namba ya shauri anasoma hapa.
Jaji anasema Wakili wa Serikali unasemaje?
Anasimama Renatus Mkude anatambulisha kikundi chake cha kila siku anachoshirikiana nacho kuiwakilisha Jamhuri.
Mshitakiwa anasema yuko tayari pia.
Jamhuri wanadai wanamambo mawili.
1. Notice of additional substance of Evidence chini ya kifungu cha 308 (1) Taarifa ya ushahidi wa ziada.
2. Jambo la pili
Mwenendo wa shauri linaloendelea na kauli zinazotolewa kuhusu mashahidi wanaotoa ushahidi Mahakamani.
Anasima Mh. Tundu Lissu kurespond kwenye hayo Mambo mawili yaliyosemwa na Mawakili wa Serikali.
Kuhusu hiyo Notice yao
utaratibu wa kisheria hauruhusu.
Anasimama Katuga anasema mtuhumiwa afate utaratibu kwamba mawakili wa Serikali wameregister Notice
Hivyo jukumu lake ni kujibu kuwa mtuhumiwa yupo tayari kusikiliza?
Mhe. Lissu anasema kama wameleta notice basi wafahamu kwamba nitakua na lakusema baada ya submission yao.
Waendelee tu sitaacha kitu, wajue hilo.
Majaji wanashauriana kwa muda mrefu kidogo hapa, tunasubiri nini kitakachoendelea.
Mhe.Jaji: tunajaribu kuangalia kama hii notice iko ndani ya mfumo na tumeona ni kweli iko ndani ya mfumo.
Katuga: tunaomba tuisubmite kwanza ili tuweze kumuombea shahidi tuliyenaye leo kwa sababu shahidi tuliyenaye leo si miongoni kati ya mashahidi tuliowaombea.
Mhe.Lissu : kiutaratibu ili waweze kusubmit notice ni lazima wafate utaratibu kwa sababu hawajafuata utaratibu tuendelee na mashahidi waliopo.
Mhe.Jaji: tutaendelea na mashahidi waliopo lakini hatuwezi kuacha notice hii bila kuizungumzia ili iweze kuingia kwenye utaratibu wa Mahakama, wakati tukiendelea na mashahidi waliopo kesho tuweze kuanza na hii notice.
Mhe.Lissu: siku ya jana tuliambiwa Shahidi aliyepaswa kuendelea ambaye ni mpelelezi Mkuu alipata msiba hivyo ataendelea leo, sasa wanatwambia kuwa huyu shahidi wanayemuombea notice anayo maelezo ya ziada ni kwa nini tusiendelee na mashahidi waliopo kwanza wakati wakifuata utaratibu.
Katuga: wameshimiwa Majaji naomba tuendelee na submission ya hii notice kwanza kabla ya kuendelea kusikiliza mashahidi wengine ili tujue kama tutaruhusiwa kumleta huyu Shahidi.
Majaji wanaendelea kujadiliana hapa.
Mhe.Jaji: kwa sababu tayari tunao mashahidi wengine hii issue ya notice ibaki reserve isubirie kwanza tutaizungumzia baada ya kumaliza mashahidi waliopo, hivyo tuendelee na mashahidi waliopo kwanza.
Mkude: Mhe.Jaji tunaomba tuadress mambo yanayoendelea katika premise ya mahakama kuhusu mashahidi kabla hatujaendelea.
Mhe.Jaji: mshitakiwa ameomba kujua ni mambo gani hayo, yasijekuwa mambo ya kutupotezea muda yanayohitaji tuanze kuandika rulling kwanza na kutuzuia kuendelea.
Wakili Mkude: mheshimiwa Jaji kuna mambo yamekuwa yakiendelea na mshitakiwa amekuwa akiadress baadhi ya mambo. Tangu kesi ianze kuna mambo yamekuwa yakijadiliwa kuhusu mashahidi wanavotoa ushahidi wao, katika mitandao ya kijamii mambo yamekuwa yakizungumzwa namna mashahidi wanavotoa ushahidi wao, wengine wakiitwa waongo, hatukatazi kureport muenendo wa kesi lakini usiathiri proceedings. Kifungu 114 cha Penal Code.
Kwa kifupi hawa jamaa hawataki mashahidi na ushahidi wao uzungumzwe nje ya Mahakama. Hawataki habari za kwamba mashahidi ni waongo. 😂😂 yaleyale ya kutaka kesi iwe gizani kwa kila kitu.
Hata hii kuripoti tu wanaona wananchi mnafaidi sana, wanataka Mahakama izuie.
Part 197 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.