"Ni heri utingwe na majukumu kuliko usiwe nayo. Majukumu hutuepusha na shari na mitihani mingi ya maisha na hutufungulia riziki. Usipotingwa nayo, utakuwa na muda mwingi wa kuhangaika na maisha ya wengine. Itakugharimu. Shukuru Mungu unayo". ~Togolani Mavura.
Ipo Siku Watakusubiri Nyumbani Wakisema Tunasubiri Mwili Wa Marehemu,Na Hawatakutaja Kwa Majina Yako Wala Cheo Chako. Na Wale Watakao Kuwa Makaburini Wanahangaika Ni Wale Ulihisi Si Level Yako.Ukikielewa Kifo,Umeyaelewa Maisha.
Jifunze kusimama kwa miguu yako. Kujitegemea. Kuwa INDEPENDENT.
Kumbuka ulishangiliwa utotoni ulipoanza kusimama peke yako. Shangwe hizo zilikuwa na maana kubwa kwamba sasa hukuwa ukihitaji kushikwa na mtu kila mara ili uweze kusimama.
Natamani Mngelijua Ugumu Tunaopitia Katika Utafutaji Wetu.Natamani Mngelijua Japo Kwa Uchache Kuhusu Historia Za Maisha Yetu Naamini Mngeacha Kutuwekea Vikwazo Chuki,Husda Na Fitna Zisizo Na Msingi Ila Tambueni Mwenyez Mungu Ni Wetu Sote Na Muda Ni Mwamuzi Wa Kweli.
"Njia nyingine nzuri ya kuwekeza katika maisha ni kuwatendea wema watoto wadogo. Wao huridhika na vitu vidogo, hushukuru kwa dhati, na hubaki daima na kumbukumbu ya waliowatendea wema utotoni mwao. Dua zao kwa Mungu husikika zaidi." ~Togolani Mavura.
"Yanayokuzunguka katika maisha yako yanatokana na wanaokuzunguka. Ukibadilisha wanaokuzunguka na yanayokuzunguka yanabadilika.Kuwa makini na
unaowakaribisha katika mzunguko wa maisha yako maana watu huja na heri na shari zao." ~Togolani Mavura.
"Furaha hupatikana kwa kuthamini na kufurahia ulichonacho,huku ukiwekeza imani na matumaini ya kupata mbeleni kile unachokitamani. Ukitaka maisha ya furaha jizoeze kuishi maisha yanayolingana na kipato na uwezo wako." ~Togolani Mavura.
"Mwenyezi Mungu ameficha katika macho ya binadamu mambo 3, umri, rizki na kiama. Hatujui tutaishi miaka mingapi, hatujui rizki yetu ya kesho na hatujui mwisho wetu na maisha yetu akhera yatakuwaje. Hekima yake ni tuwe wanyenyekevu." ~Togolani Mavura.
"Life is too short to wake up in the morning with regrets. So love the people who treat you right and forget about the ones who don’t." - Harvey Mackay