@HildaNewton21 Na bado tunadai KATIBA MPYA wako kimya na tunasema MBOWE SIO GAIDI wako kimya huu ni mwanzo tu yatavunjwa sana wamekalia kula sadaka tu kama hawaoni nchi inakoenda
Kiongozi 1: Habari yako Furaha?
Mimi : Njema, za siku?
Kiongozi: Kiasi, mmeleta shida, Mnaodai #KatibaMpya
Mimi: Kila mwananchi ana haki ya kudai katiba bora. Nani analalamika?
Kiongozi: Tumepewa kazi juu ya hilo. Hatujui pakuanzia. Hongereni mnaipenda nchi
#WenyeNchiWananchi
Wananchi wanapopiga kura na kuchagua viongozi wao, haina maana ni lazima wasubiria miaka 5 ili kubadilisha viongozi wabovu, lazima kuwa na mfumo wenye kuruhusu wananchi kutoa mapendekezo hata kabla ya uchaguzi.
#KatibaMpya#WenyeNchiWananchi
Tume ya Uchaguzi ( NEC ) na ile ya Zanzibar ( ZEC) zote zina changamoto ya kuwa Tume Huru, kutokana na namna Tume hizo zinavyopatikana kwa kuteuliwa na Rais.
#KatibaMpya#WenyeNchiWananchi
Karibu nchi 30 zinatumia mfumo wa demokrasia ya moja kwa moja, Demokrasia ya moja kwa moja ni pale ambapo wananchi wanapokuwa na maoni, au wito (petition) sheria inatoa mwongozo wa namna bunge litakavyo shughulikia maoni husika.
#KatibaMpya#WenyeNchiWananchi
"Mtu akikata tamaa kwa sababu ya uchaguzi wa mwaka jana, huyo hajajua maana ya mageuzi. Chama hiki kimeundwa miaka 30 iliyopita." Mhe. @freemanmbowetz.
#NukuuMbowe#MboweSioGaidi