Chai na vitumbua asubuhi katika Ikulu Ndogo Tanga, kabla ya kuanza kazi kuelekea Muheza na kisha Mkinga kuzungumza na wananchi na kuhusu kazi, na namna zaidi ya Shilingi Trilioni 3.1 toka serikalini kuja Mkoa wa Tanga zilivyobadili maisha yao kupitia miradi mbalimbali katika kipindi cha miaka minne.
Imekuwa Jumatatu nzuri ya kazi na wananchi Bumbuli, Lushoto Mjini, Mkomazi na kisha Korogwe Mjini, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yangu ya kikazi katika Mkoa wa Tanga.
Mbali na kuupa Mkoa wa Tanga Shilingi Trilioni 3.1 kwa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne ambayo sasa tunaona matokeo yake kwenye maisha ya wananchi, tumeanza ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji Mkomazi, moja ya miradi muhimu kwa watu wa Mkoa wa Tanga hasa kwenye kilimo. Katika Wilaya ya Korogwe pekee, mradi huu utanufaishi zaidi ya wananchi 20,000, na kuwapa nafasi ya kukua zaidi katika kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
@jokateM Hakika mama yupo kazini anawagusa wote haachi mtu watanzania tunajivunia Rais wetu kipenzi @SuluhuSamia Mungu ampe maisha marefu ilituendelee kufurahia matunda yake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Pangani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa kumba ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025.
@ikulumawasliano Tumeona wanachi wa nafuraha Sana shangwe na ndeleo wakimfurahia Rais wetu kipenzi @SuluhuSamia amefanya mambo mengi sana katika mkoa wa tanga kawagusa sana wanachi hakika kazi iendelee