Wapiga Kura 222,218 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Isimani lililopo Halamashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Mei 31, 2026 Mkoani Iringa wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Juni 01, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 628 vya Kupigia Kura vitatumika.
โwapiga kura 89,753 wapo kwenye Jimbo la Ismani na wapiga kura 132,465 wapo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo na vituo 277 vipo kwenye Jimbo la Ismani na vituo 351 vipo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo.,โamesema Jaji Mwambegele.
Aidha, amesema Katika Uchaguzi huo, jumla ya wagombea 108 kutoka katika vyama vya siasa 17 wanawania nafasi wazi ya ubunge na udiwani katika maeneo aliyoyataja.
โJimbo la Ismani lina wagombea 17 wa nafasi ya Ubunge ambapo kati ya wagombea hao wagombea nane (08) sawa na asilimia 47.06 ni wanaume na wagombea tisa (09) sawa na asilimia 52.94 ni wanawake. Kata 12 zinazofanya uchaguzi mdogo wa udiwani zina jumla ya wagombea 91 ambapo kati ya hao wagombea 61 sawa na asilimia 67.03 ni wanaume na wagombea 30 sawa na asilimia 32.97 ni wanawake.โ amesema Jaji Mwambegele.
Na kuongeza kwa kusema โNatumia fursa hii kuvikumbusha Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi kesho Juni 01, 2026 kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumlishia kura. Wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo na Kata husika, wamekamilisha taratibu zinazoweka mazingira yanayowawezesha mawakala wa vyama vya siasa kufuatilia mchakato mzima wa uchaguzi".
Amesema, mawakala hao, wanawajibika katika kulinda maslahi ya vyama na wagombea wao. Hivyo, wanapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu za Uchaguzi na maelekezo ya Tume katika utekelezaji wa majukumu yao vituoni.
Jaji Mwambegele amesema vituo vitafunguliwa saa 01:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 24, 2026 amezindua rasmi Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT) yaliyopo Kikombo jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Mhe. Lord Hugo Swire mara baada ya mazungumzo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kabla ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.
Saa 24 ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu Kailima, R. K (kulia) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Ndugu Adam Mkina wakishuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya
Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT - WAZALENDO), Mhe. Luhaga Joelson Mpina na Mgombea Mwenza, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej majira ya Saa 10:00 jioni ya leo (13/9/2025) ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria inayotaka fomu hizo kubandikwa kwa