#UGANDA: UGANDA GHETTO KIDS MAKE HISTORY IN WORLD CUP 2026 SPOTLIGHT
The Ghetto Kids, a Ugandan dance troupe made up of street children, speak of their excitement at being invited by music superstar Shakira to perform at the World Cup.
MORE: https://t.co/Oi6CHIQHpq
Former Raja midfielder Moses Orkuma has joined Union Military SC in Libya on a six-month loan deal, with an option to extend.
#Transfers#AfricanFootball
Jina lake la kuzaliwa ni Selemani Msindi, Jina lake kwenye Ulimwengu wa Rap ni Afande Sele, miaka yake ya kuzaliwa ni 49 na tukio lake kubwa la leo ni ndoa aliyofunga na Mpenzi wake aitwae Wema Raphael Makongoro.
Wawili hawa leo Disemba 6, 2025 Mkoani Morogoro wamefunga ndoa hii ya Kiserikali chini ya Katibu Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro Hillary Sagara na kuhudhuriwa na Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wasanii mbalimbali.
Hii inakuwa ni ndoa ya pili kwa Afande Sele katika maisha yake baada ya Mkewe Mama Tunda kufariki dunia Agosti 14, 2014, AyoTV tunawatakia kila la kheri Afande na Wema katika unganiko hili lililozaliwa rasmi hii leo. #MillardAyoUPDATES
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhutubia Taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kesho December 02,2025 Jijini Dar es salaam .
Akiongea leo December 01,2025, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema β"Kutokana na Mkoa wetu kuendelea kurejea katika hali yake ya amani, Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atazungumza na Wazee wa Dar es Salaam kesho December 02, 2025 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC kuanzia saa tano asubuhi na kuendeleaβ
βMh. Rais katika kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam atatumia nafasi hiyo pia kuhutubia Taifa, nitoe rai kwa Wana Dar es salaam na Watanzania kumsikiliza Mhe.
Rais atakapokuwa anazungumza na Wazee wa Dar es salaamβ
βHii ni moja ya hatua kubwa anayochukua kuhakikisha nchi yetu inarejea katika amani, katika kuhutubia huko ataambataana na Wageni wengi wakiwemo Viongozi wa Serikali na Viongozi wasio Watumishi wa Umma, ni mkutano muafaka unaorejesha matumaini na kuendelea kuponya pale ambapo Watanzania waliumiaβ
#MillardAyoUPDATES
Nakiri nilikosea, siwezi kujifanya kiziwi, kipofu ikiwa naona na nasikia. Siwezi kusonga mbele wakati safari ni ngumu kutembea siwezi moyo na mwili havifanyi kazi sababu ya maumivu.
Nilikosea, siwezi kurekebisha makosa ila naweza kuanza upya. Naomba radhi wote niliowaangusha.
Mkongwe wa Mziki nchini Uganda Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone amevunja ukimya kuhusu mwenendo wa talaka yake na Mke wake Daniella Atim waliofunga ndoa miaka 17 iliyopita na kusisitiza kuwa ingawa amekubali mali zake kugawanywa lakini hakubaliani na kitendo cha kulazimishwa kusaini wosia.
Kwa mujibu wa ripoti ya Vyombo vya Habari Nchini Uganda vya BigEye na Pulse Uganda, Chameleone amesema hayo wakati akiwa LIVE kupitia kurasa zake Mtandaoni na kuweka wazi kuwa mali wanazogombea na Mkewe ni mali za Watoto na sio zao binafsi.
βMambo tunayopigania ni ya Watoto sio yetu na hata Watoto watawaachia Watoto wao, acha kutengeneza hali ambayo hakuna" amesema Chameleone.
Mchakato wa kugawanywa kwa mali zake umeanza kuonekana mapema baada ya Mke wake kufungua mashtaka Mahakamani kudai talaka mnamo mwezi Machi mwaka huu ambapo August 21 alikubali kutoa talaka kwa kile Mkewe alichokiita kutelekezwa.
Chameleone mwenyewe amesema kuwa hana pingamizi la kusaini hati za kisheria ikiwa sheria itamtaka na amesisitiza kuwa utajiri wake wote ni kwa manufaa ya Watoto wake watano na sio yeye wala Mkewe na ameongeza kwamba hajalemewa na mchakato wa talaka amewahakikishia Mashabiki zake kuwa bado yuko katika amani wakati vita ya kisheria ikiendelea.
#MillardAyoUPDATES