Market opportunity
A buyer is looking for 200 tones of Rosecoco(beans) , if you can supply this quantity please call or WhatsApp us at +250786506040.
Could you please repost for the others?
Salamu za mwaka mpya wa 2024, toka kwa Mwl Christopher Mwakasege.
Na Malengo 5 ya kuwa nayo katika Mwaka 2024
Nilipokuwa ninaiombea tarehe 1 Januari 2024, hasa juu ya watu wa Mungu kuweka malengo ya mwaka. Kuna ujumbe ambao Mungu aliniwekea moyoni, ambao nataka nikushirikishe hapa kwa muhtasari tu.
Ujumbe huo ulihusu aina ya malengo, ambayo watu wake wengi, wanasahau kuyaweka kama malengo.
Wengi wao huwa wanaweka kama ajenda za maombi, lakini si kama malengo ya kuyaombea na kuyatekeleza, ili Mungu awasaidie katika kuyatekeleza.
Malengo yoyote yasiyo na mikakati ya kuyatekeleza, hata ukiyaombea, inakuwa vigumu kuyatekeleza, na kuyafuatilia kiutekelezaji.
Ndio maana Mungu akikupa “wazo” la kufanya, ujue anao mkakati anaotaka uutumie kulitekeleza wazo hilo. Neno linalotumika zaidi kibiblia kuhusu mkakati, ni neno “njia”.
Mungu anasema katika Isaya 55:8, 9; juu ya utofauti uliopo juu ya mawazo yake juu yetu, na utofauti wa njia zake au mikakati yake ya kutekelezea mawazo aliyonayo juu yetu.
Kila wazo lina mkakati wake wa kulitekeleza. Vivyo hivyo na malengo. Kila lengo lina mkakati wake wa kulitekeleza. Kwa hiyo, wazo la Mungu lina malengo na mikakati ndani yake.
Ukijiwekea malengo ambayo hayaendani na mawazo ya Mungu, na mikakati ya Mungu kwa ajili yako, inakuwa si vyepesi kupata msaada stahiki toka kwa Mungu, kwa ajili ya kuyafanikisha.
Ndani ya ujumbe niliowekewa moyoni mwangu, ni kukuwekea msisitizo ya kuwa, katika malengo yako ya mwaka 2024, usiyasahau malengo mkakati yafuatayo:
LENGO MKAKATI LA 1:
Upate kumjua Mungu zaidi, sawasawa na Ayubu 22:21.
Mstari huu wa Biblia unasema hivi: “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; ndivyo mema yatakavyokujia”. Ukitaka kuona mema aliyokupangia (Yeremia 29:11), kwa mwaka 2024 yanakujia, basi weka lengo hili na mikakati yake husika, kuhusu kumjua Mungu zaidi, ili uwe na amani.
LENGO MKAKATI LA 2:
Umzalie Mungu matunda, ambayo atayatumia kuwagusa wasiomjua, ili wapate kumjua, sawasawa na Ufunuo wa Yohana 22:2.
Mstari huu unazungumzia juu ya “Mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa”. Hii ina maana tuwe na lengo la kumzalia matunda kimkakati!
Yesu anapokuwa “mti” wa uzima, tuliookoka tunakuwa “tawi” lake la uzima! Tunatakiwa tumzalie matunda, kwa msaada wa uzima wake, aliouweka ndani yetu.
Leo, Yesu anatukumbusha ya kwamba hatukujichagua kuingia mwaka 2024, bali ni yeye aliyetuchagua sisi. Na lengo mojawapo la kutuingiza mwaka 2024, ni ili tumzalie matunda, na matunda hayo yapate kukaa (Yohana 15:16).
LENGO MKAKATI LA 3:
Uweze kuomba kwa mfululizo kwa lisaa limoja, angalau mara moja au zaidi kwa wiki, sawasawa na Mathayo 26:40, 41.
Yesu anauliza kwenye mstari huu swali hili: “Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? Kesheni, muombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”
Yesu anataka tujue, msaada tunaoupata tunapoomba kwa muda mrefu kwa mfululizo, wa kutusaidia kushinda upinzani dhidi ya mwombaji kutengenezewa mazingira ya kukishinda, kile kinachomzuia asiyafanye mapenzi ya Mungu.
Soma na kutafakari habari hii ya Mathayo 26:36 – 46, inayotujulisha jinsi maombi ya muda mrefu yalivyomsaidia Yesu, kuivunja nguvu ya mwili iliyokuwa inafanya roho yake iombe kikombe kimwepuke.
LENGO MKAKATI LA 4:
Jiwekee lengo kimkakati la kuweka akiba ya kutosha, uweze kupambana na upungufu wa pesa, katika eneo ambalo mwaka 2023, lilikusumbua kwa upungufu wa pesa za matumizi, sawasawa na Mithali 6:6 – 11.
Mistari hii ya Mithali 6:1 – 11, inaweka msisitizo wa mtu kushinda uzito moyoni, ambao watu wengi wanakuwa nao, wa kushindwa kuweka mikakati endelevu ya kuweka akiba.
Kumbuka ya kuwa, akiba ni jambo mojawapo muhimu linalokusaidia kuweka akiba ya kukidhi mahitaji yako ya wakati ujao.
LENGO MKAKATI LA 5:
Jiwekee lengo mkakati la kuilinda imani ndani yako, inayobeba amana uliyokabidhiwa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu, sawasawa na 2 Timotheo 1: 14.