Zamani sana, yule dogo alikuwa akija kwetu kucheza, muda wa chakula lazima umkute pale.
Tunakula wote mwanzo mwisho, kwa akili za kitoto kabisa, niliwahi kumuuliza Mama..
Kwanini yule dogo anakula kwetu, wakati Mama yeye katukataza tusile kwa watu, hasa kwao yule dogo?..
Habari @YasTanzania_ Naomba kujua mmechukua hatua Gani Mpaka Sasa kuhusu watu wanaokatwa Hela na Tech Vault LTD.
Tukipiga simu maelezo ni Mengi na hayana Msingi.
Ukipitia comment kwenye post hii ya Facebook https://t.co/dNFEiIBjVN
Unagundua Namna Gani wimbi ni kubwa, Mnazingua.
. @wizara_afyatz na @changiadamutz
Mama mjamzito amejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala – Amana Regional Referral Hospital. Anapatikana katika wodi No. 09, ambapo katika kipindi hicho cha kujifungua aliongezewa damu chupa 12.
Familia ya mama mjamzito, imelipa gharama stahiki za huduma ya kujifungua, baadae wakaletewa gharama ya mzazi huyo kuwekewa damu ambayo wamepewa risiti ya malipo ya damu. Pia, wamelipa malipo yote.
Mama aliyejifungua amekuwa discharged (ameruhusiwa kutoka hospitalini), lakini amenyimwa ruhusa ya kuondoka hospitalini hadi alete watu 12 wa kuchangia damu (replacement donation) iliyotumika.
Maagizo hayo ya kumzuia mama aliyejifungua yametolewa na Muuguzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala (Amana Regional Referral Hospital), ambaye anapatikana chumba Na. 15 katika hospitali hiyo
Je, utaratibu huo ni sahihi kisheria? Kwanini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala inautumia kama sharti la kumzuia (dention) mgonjwa? Je, kumzuia mgonjwa kuondoka baada ya kuruhusiwa siyo false imprisonment?
Kisheria, chini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja na Wizara ya Afya, hospitali hairuhusiwi kumshikilia mgonjwa aliyesharuhusiwa kuondoka (discharged) kwa sababu tu hajapata wachangiaji wa damu wa hiari.
Sera hii ililetwa kwa sababu ya tatizo la kihistoria katika hospitali nyingi ambapo wagonjwa au familia zao waliambiwa wapeleke “wachangiaji damu” kabla mgonjwa hajaruhusiwa kuondoka hospitalini.
Sera inaweka msimamo: Damu inayochangiwa ni ya hiari na bure. Wagonjwa hawapaswi kulazimishwa kulipa au kuleta wachangiaji kama sharti la kupata huduma ya damu. Hairuhusiwi kuuza au kununua damu.
Gharama inayolipwa hospitalini ni vifaa vya maabara, vipimo vya usalama wa damu, uhifadhi wa damu, na huduma ya kuongezewa damu, lakini siyo malipo ya damu yenyewe. Wagonjwa wasibebeshwe mzigo.
Kwamba wagonjwa wanatakiwa kuleta wachangiaji wa damu (replacement donors) ndiyo waruhusiwe kuondoka wodini? Je, wakikosekana hao replacement donors? Mgonjwa atashikiliwa kwa muda gani hospitali?
HAKI ZA MTUHUMIWA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 [RE 2022], pamoja na Sheria nyingine za jinai, mtuhumiwa ana haki zifuatazo mara baada ya kukamatwa.
Form Four👇
2015
2016
2017
2018
2019
2020
Mkapata One, Two Au Three!!
Nyie Wanaume Mnoo,
Mnastahili Heshima👏
Zile Pepa Na Zile Grade Magufuli Alikaza Sana!!
Na Alikua Serious Mnoo😂😂
Hapo Bado Wizara Inatangaza Hamna Pepa Kuvuja Wala Kurudiwaa😂😂🙌
Wazee kutibiwa kwa cash kuna umiza nilimpeleka ndugu yangu hospital moja ya private wakamlaza kama siku tatu hivi ile naenda kufuatilia bili mkeka unasoma milioni tatu.
Nikarudi kumpangilia mgonjwa hali halisi akasema kaka hapa nina kama laki tano tu kawapunguze nikarudi kubonga nao nikawapa ile mia tano nikawaambia nyingine inatumwa sio muda nikarudi wodini mdau akanambia kaka hapa hatutoboi waza kiyakuza nikamwambia haina neno mkali.
Usiku wa kama saa nane hivi manesi wakiwa wamelala na mwana bado ana ma canula, nikacheki getini naona mlinzi nae kapiga usingizi chap sana nikambeba mwana shuka kwenye mangazi kwa kunyata sisi hao tukatorokea kwenye migomba.
Wale wakuu wa hospitali watusamehe tu tulifanya yote hayo sababu ya umaskini tu.
Hilo tukio huwa silisahau maana tulipiga kama zile movie za mayakuza wa kijapani📌
Kwa ujumla, furaha ni neno lenye maana pana; mtu mmoja anaweza kuwa na furaha kwa kuwa yuko vacation Dubai, wakati mwingine anafurahi kwa sababu kuku wake ametotoa vifaranga.
Kuna ile Clip ya yule jamaa yupo na familia yake wanakula ugali.
Then baada ya kumaliza akamshukuru Mungu kwakuwa familia imefanikiwa kupata Mlo.
Ile pia ni Furaha.
Mwenye ile Clip anisaidie hapa🙏🏾
RASMI! @barakamaviatu Sasa ni Mwana Karakana!
@barakamaviatu tumejiunga na familia na kutuandalia kozi "Biashara ya viatu vya mtumba" na inaanza rasmi LEO kupitia #Karakana App
Pakua Karakana App leo na uwe miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kujifunza.
#Ujasiriamali