#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 171
Mhe. Lissu anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.
Amemaliza kusoma maelezo anamuonesha maeneo aliyodanganya au kuleta mkanganyiko.
1. Dini
2. Umri
3. Shughuli za Chama alizoambiwa atakuwa anataka kuzifanya
4. Tar. 04/04/2025 ulikuwa na simu infinix smart 8.
5. Hiyo simu yako lilikuwa na bando la Internet
6. Uliingia kwenye mtandao wa youtube wa Jambo Tv
7. Mimi mtuhumiwa nilisema yoyote atakayekuwa nasi tutaenda nae ambae hatataka tutamuacha.
8. Nilisema anayetaka kugombea udiwani au ubunge asahau na mimi niliyetaka kugombea urais nisahau
9. No Reforms: No Election.
10. Wanasema tutafanya uasi ni kweli tutafanya.
11. Niliitoa hotuba yangu ndani ya ukumbi na kulikuwa na bendera ya taifa na ya Chadema
12. Nilivaa kombati za kaki nayo nataka unioneshe.
13. Kwamba tutazuia uchaguzi kwa kufanya vurugu
14. Nataka niyaone maneno ya Mwamba wa Kigoma.
15. Kwamba Mwamba wa Kigoma alikusifia kwa uamuzi wa kishujaa na wewe ni mojawapo ya vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.
16. Tar. 06/04/2025 ulipata taarifa kuwa Mh. Tundu Lissu atatembelea Mkoa wa Ruvuma.
17. Ulipewa taarifa ya kumpokea Mwenyekiti wa Chama Taifa.
Mhe. Lissu anamsomea maeneo ambayo shahidi amedanganya au ameyasema leo lakini kwenye maelezo yake ya Polisi hajasema.
Anaweza msomea maeneo hata 50.
Kwa kifupi anachokifanya kuyataja hayo maeneo ni kama anamuandaa au kumlainisha shahidi kabla ya kuanza kumsokota, kuonyesha uongo wa shahidi.
Ameonyesha maeneo 20.
Mhe. Lissu Lissu: Anamuuliza je ungependa maelezo yako yapokelewe kama sehemu ya ushahidi na mimi nikuhoji sawasawa?
Shahidi wa kificho P6: Amenyamaza hasemi chochote, hapo haya ndo maelezo yangu na kama kuna kitu hakipo mimi ni binadamu siwezi kukumbuka kila kitu na kama kuna kitu nimekizungumza mahakamani siwezi kukumbuka kila kitu.
Mhe. Lissu: Shahidi Kaka yangu ungependa hayo maelezo yako yapokelewe kama kielelezo?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu niloyoyaandika Polisi au niliyozungumza hapa Mahakamani ndio nimetakiwa nizungumze mbele ya Mahakama.
Mhe. Lissu: wambie ungependa yawe sehemu ya ushahidi mahakamani.
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu yawe ushahidi Mahakamani.
Hatimaye amekubali.
Majaji wanaandika sasa.
Huyu Shahidi amesumbua sana kuyakubali maelezo yake ili yapokelewe hapa Mahakamani.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?
Renatus Mkude anasema No Objection.
Jaji Nduguru: Basi maelezo haya yatakuwa ni D4.
Mhe. Lissu: Anasema ahsante sana, sasa anaendelea.
Kabla hujaapishwa hapa Mahakamani uliulizwa dini yako ukasema wewe ni Mkristo?
Shahidi wa kificho P6: Kweli
Mhe.Lissu: waeleze majaji kwenye hayo maelezo yako eneo la dini yako umeweka nini?
Shahidi wa kificho P6: Sijaona hapo.
Anasimama Katuga anaweka pingamizi watu wanamzomea.
Jaji anasema tuendelee
Shahidi wa kificho P6: Hapa Dini imeandikwa sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Dini imeandikwa Muislamu?
Shahidi wa kificho P6: hapa sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Umri wako je?
Shahidi wa kificho P6: Miaka 23 imeandikwa hapa.
Mhe. Lissu: Ulisema shughuli za Chama ulizopewa ni kuongoza misafara ya Chama ukiwa na bendera na pikipiki?
Shahidi wa kificho P6: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yanaonesha nitashiriki kwenye mikutano ni vitu ambavyo sikuviandika.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hayo yameandikwa au hayajaandikwa?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yameandikwa kushiriki mikutano.
Mhe. Lissu: We Chadema wa Mapolisi usitupotezee muda, tuambie yapo kama yapo.
Shahidi wa kificho P6: sijui
Mhe. Lissu: Tarehe 04/04 umesema ulikuwa na simu yako infinix smart 8 tuambie kama hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Mhe. Lissu: Sijakuuliza unayafahamu au huyafahamu, nimekuuliza yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Part 172, itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 170
Shahidi wa kificho P6: Akasema tutawanyike na atapanga tarehe nyingine ya mkutano huo.
Wakili: Huyo Makamu Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Heche.
Wakili: Tar. 18/04/2025 nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Nilipokea taarifa kuwa tarehe 20/04/2025 siku ya pasaka kutakuwa na matembezi ya hiyari ambapo katika matembezi hayo yataambatana na kuvalia tshirt zilizoandikwa agenda ya No Reforms: No Election ili kuendeleza agenda ya Chama.
Wakili: Kingine kilichoendelea?
Shahidi wa kificho P6: Ukafanyika utaratibu wa kuzipata tshrit na tunachangia elfu 10 ndipo zitasafirishwa hadi kutufikia.
Tukaambiwa hadi kufikia tarehe 20 basi tutakutana kwa ajili ya matembezi hayo ya hiari.
Wakili: Tar. 20/04/2025 kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulijikusanya kwa ajili ya matembezi ya hiari kila mmoja alipata tisheti yake na tukakubaliana jioni majira ya saa 10 ndio matembezi ya hiari yatafanyika.
Wakili: Ulipata wapi hizo taarifa:
P6: Group la Siasa Yetu.
Wakili: Matembezi mlikubaliana mkutane wapi?
Shahidi wa kificho P6: Songea Mjini kwa Disi Kitimoto na ilipofika majira ya saa 10 huku tukiwa na bodaboda huku tukisubiri wengine. Mimi nilikuwa kwenye muonekano wa kuvaa tshirt iliyoandikwa agenda ya No Reforms: No Election.
Wakili: Nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Wakaja Polisi wakajitambulisha kwa ghafla kuwa wanatokea kituo cha Polisi Songea na wakatuambia tunahitajika kituo cha Polisi Songea kwa ajili ya mahojiano.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P6: Walitukamata na kutupeleka kituo cha Polisi Songea na wakatuhoji kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Wakili: nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakasema tutatoka kwa dhamana lakini tulihitajika kwenda kuripoti ofisi ya RCO.
Wakili: Tarehe 25/04 nini kiliendleea?
Shahidi wa kificho P6: Tuliripoti Ofisi ya RCO tumuelezee kilichotokea hadi kufika sehemu hiyo.
Wakili: Mhe. Jaji ndio hayo kwa shahidi huyo.
Watu wanashangaa sasa huyu shahidi sijui alikuwa anazungumza nini na kinasaidia nini kwenye Uhaini ni Maajabu, ngoja Tunasubiri aanze kuulizwa maswali hapa.
Jaji Ndunguru: Vipi mshitakiwa tukupe nafasi ujikusanye vizuri?
Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu shahidi nilishajiandaa nae toka juzi.
Sasa shahidi sijui wewe ni Kaka au Dada lakini naomba ujibu maswali yangu sawa?
Shahidi wa kificho P6: sawa.
Mhe. Lissu: Uliandika maelezo Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Sijaelewa swali.
Mhe. Lissu: Kitaeleweka tu. Jibu swali langu Bwana.
Shahidi wa kificho P6: niliandika
Mhe. Lissu: Ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P6: ndio.
Mhe. Lissu: Ulisaini?
Shahidi wa kificho P6: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji naomba aonyeshwe maelezo yake.
Shahidi wa kificho P6: Nimeyapata na ndio maelezo yangu niliyoandika Polisi Songea.
Mhe. Lissu: Je yana sahihi yako?
Shahidi wa kificho P6: sahihi yangu ipo ndio.
Mhe. Lissu: Ni maelezo ya Tar. 25/04/2025.
Shahidi wa kificho P6: Sioni hiyo Tarehe.
Mhe. Lissu: Angalia juu mwanzoni, anamsomea hilo eneo.
Shahidi wa kificho P6: Sijayaona hayo maelezo.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka ku impeach huyu shahidi, nitamsomea maelezo yake, anamsomea hapa.
Mimi ni mkazi wa Bombambili, kazi yangu Bodaboda na kituo changu ni miembeni.
Ilipofika mwaka 2025 nilimfuata Katibu wa Vijana Essau Chiza alinikaribisha kwenye Chama na kunifanyia mpango wa kadi ya Chama.
Nakumbuka tarehe 04/04/2025 niliona mtandao wa youtube hotuba ya Lissu iliyokua inahusu uchaguzi 2025 iliyokuwa ikihamaisha uasi. Ilinipa moyo wa kijasiri wa kutaka kuvuruga uchaguzi.
Nikamtafuta Essau Chiza ambae ni Katibu kunipa mipango mingine ikiwemo ziara ya Mwenyekiti Taifa.
Anaendelea kumsomea maelezo yake yote hapa.
Part 171 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 13, 2026
Jana tuliishia Part 167 so leo tunaendelea na-;
Part 168
Mahakama imeanza muda huu saa tatu na nusu.
Mhe. Lissu anaingia akiwa amevaa kombati nyeusi.
Sauti ya High Courttt inapigwa kila mtu anasimama na kelele za kumsalimia Mwenyekiti zinasimama kidogo.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Ignas, Cathbert na Winiwa na wote tunawakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Sisi tuko tayari kuendelea na leo tumekuja na P6 yuko tayari, endapo Mshitakiwa atakuwa tayari.
Mhe. Lissu anaulizwa na yeye anasema yuko tayari.
Jaji Ndunguru: Naomba shahidi aje sasa.
Shahidi analetwa kama Bangi kule mbele kwenye kibox hatumuoni chochote tunaona milango tu inafunguliwa sijui amevalishwa baibui.��
Mlango wa kizimba umefunguliwa muda huu.
Shahidi anaulizwa umri wake anasema miaka 24 na ni Mkristo so anaapishwa muda huu.
Jaji anauliza nani atamuongoza? Anajibiwa ni Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ndio atamuongoza.
Anamuuliza unanisikia.
Haya mkazi wa wapi?
Mimi natokea Ruvuma Songea na kazi yangu ni Afisa Usafirishaji Bodaboda, nafanyia huko huko Songea shughuli zangu.
Mwezi October 2024 ni mwaka ambao nilianza kushirikisha siasa za Chama cha Chadema.
Wakili: Ulishiriki kivipi?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kushiriki kwenye mikutano ya hadhara na kuwafuatilia viongozi mbalimbali wa Chadema na nikafanikiwa kuwafahamu Mhe. Lissu na baadhi ya Viongozi waliokuwepo Songea.
Wakili: wakiwepo akina nani?
Shahidi wa kificho P6: nilimfahamu Katibu wa Vijana Songea.
Wakili: Alikuwa anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P6: alikuwa anaitwa Chiza au Mwamba wa Kigoma maarufu kwa jina hilo.
Wakili: January 2025 unakumbuka nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kuwa nimeshiriki siasa za Chadema na kuvutiwa kuwa mwanachama wa Chama hicho.
Nikaanza jitihada za kutafuta viongozi waliopo Songea, nikamfuata kiongozi wa Vijana Chiza na kumueleza nia yangu ya kutaka kuwa mwanaChama.
Wakili: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Shahidi wa kificho P6: Alinipokea na kunisifia kwa uamuzi mzuri. Akasema napaswa kuwa na kadi ya Chama, nilifuatilia hiyo kadi na nikaambiwa nisubiri mashine bado ni mbovu na ataendelea kunishirikisha kwenye shughuli za Chama.
Wakili: Zipi hizo shughuli za Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sisi bodaboda huwa tunakuwa kwenye misafara ya Chama na bendera.
Wakili: Tar. 04/04/2025 kilitokea nini?
Shahidi wa kificho P6: Hiyo tarehe nikiwa sehemu yangu ya kazi pia nikiwa na simu yangu ya mkononi aina ya infinix smart 8 nikiwa naangalia mtandao wa Youtube.
Wakili: Youtube ni nini?
Shahidi wa kificho P6: ni mtandao wa kijamii ambao unamuwezesha mtu kutuma video, audio na maudhui mengine.
Huyu Bodaboda wa miaka 24 anavyoelezea mambo unashangaaa ni kama anajibu essay huyu atapata tabu kwenye maswali. 😂
Anaendelea kuwa simu yake ilikuwa na internet na aliingia google kumuwezesha kuingia youtube.
Shahidi wa kificho P6: Niliingia kwenye account ya Jambo TV nilifanikiwa kuona na kusikiliza hotuba aliyokuwa anatoa Mwenyekiti wa Chama cha Chadema ambapo alionekana akihutubia watu akisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo tunaenda kukinukisha.
Tunakwenda kuvuruga Uchaguzi pia nilisikia na kuona akisema tunakwenda kukinukisha na yeyote atakayekuwa pamoja nasi tutakwenda nae na ambae hatataka tutamuacha pia alisema kama kuna mtu yeyote anatarajia kugombea asahau jambo hilo.
Wakili: Pia akasemaje?
Shahidi wa kificho P6: Pia hata mimi kugombea uenyekiti msahau pia akasema bila mabadiliko hakuna Uchaguzi.
Wakili: Kingine kipi?
Shahidi wa kificho P6: Pia akasema watasema tunafanya uasi ni kweli utakuwa ni uasi kwasababu bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Part 169 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 164
Anaendelea Mhe. Lissu na cross examination.
Mhe. Lissu: Uliporudi nyumbani kwako umesema kwamba ulimpigia ndugu yako askari?
Shahidi wa kificho: kweli.
Mhe. Lissu: ulisema anafanya kazi tabata relini?
Shahidi wa kificho: kweli.
Mhe. Lissu: Tuoneshe yako wapi kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Mhe. Lissu: huyo ndugu yako askari Polisi ana jina?
Shahidi wa kificho: ndio jina analo.
Mhe.Lissu: Polisi umemtaja jina? Waeleze majaji kama kuna mahali umemtaja jina?
Shahidi wa kificho: Sijamtaja.
Mhe. Lissu: Ana cheo chochote?
Shahidi wa kificho: sijui kama ana cheo chochote.
Mhe. Lissu: ana force no?
Shahidi wa kificho; sijui hata maana yake mimi.
Mhe. Lissu: ulipoangalia ile video ukaona maneno ukapata hofu?
Shahidi wa kificho: kweli.
Mhe. Lissu: kwenye maelezo yako wapi?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo hayo.
Mhe. Lissu: Tarehe 09 siku unaandika maelezo yako Polisi ulipofika Central ulimpigia simu aliyekupigia mwanzoni?
Shahidi wa kificho: ndio.
Mhe. Lissu: uliandika wapi kwenye maelezo yako polisi?
Shahidi wa kificho: Yapo yameandikwa lakini hapa hayapo.
Mhe. Lissu: maana yake nini sikuelewi?
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo.
Mhe. Lissu: Yale maneno kwamba tutakinukisha ndio yaliyotokea siku ya Uchaguzi ulisema hivyo?
Shahidi wa kificho: Ndio nimesema.
Mhe. Lissu: je uliandika maelezo ya ziada polisi ili kujumuisha kilichotokea tar. 29/10 au wamekupanga tu uje uongeze na hayo.
Shahidi wa kificho: Tar. 09/04 ndio maelezo yangu.
Mhe. Lissu: kwahiyo huna maelezo ya ziada?
Shahidi wa kificho: kwa hapa hamna na hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: Najua akina Mafwele, Kingai na George wamekwambia tu kaseme sasa nakuuliza yapo maneno hayo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Shahidi wa kificho: Unanichanganya mimi.sijui.
Mhe. Lissu: Ulikaa ndani siku sita ukiwa na njaa. Hebu tuonyeshe kama yapo kwenye maelezo yako polisi?
Shahidi wa kificho: Kwa hapa hayapo ili niliyatolea maelezo.
Mhe. Lissu: Kwahiyi Mapolisi wamekuuza na kukupuuza, uliwaambia vitu hawakuandika?.
Shahidi wa kificho: Kimya
Mhe. Lissu: Sasa nimemaliza kukuonesha kuwa wewe ni mtu wa kupuuzwa huaminiki. Ngoja nianze kukuuliza maswali yangu sasa.
Watu wanacheka.😂😂😂
Mhe. Lissu: Huo mtandao wa Facebook ni account ya nani?
Shahihi wa kificho: ilikuwa kwenye account yangu ya faceebook.
Mhe. Lissu: unaelewa kweli unachojibu? Niambie account inaitwaje?
Shahidi wa kificho: Sikujua account inaitwaje.
Watu wanacheka.😂😂😂
Mhe. Lissu: uliona video ya Tundu Lissu. Sasa Majaji hawajaona hiyo video. Wewe umewaonyesha.
Shahidi wa kificho: Simu yangu ilipotea mwaka jana.
Mhe. Lissu: umewaonyesha.
Shahidi wa kificho: Sikuwaonyesha.
Mhe. Lissu: Umeiwasilisha hiyo video Mahakamani?
Shahidi wa kificho: sikuiwasilisha.
Mhe. Lissu: ulipompigia yule askari simu na kumuuliza kama wameyasikia ya Tundu Lissu. Hayo unakumbuka ulisema?
Shahidi wa kificho: ndio nakumbuka.
Mhe. Lissu: Je ulienda kutoa polisi taarifa?
Shahidi wa kificho: Sikwenda.
Mhe. Lissu: Huyo ndugu yako Polisi alikwambia uende kufungua RB polisi?
Shahidi wa kificho: Hakuniambia hayo.
Mhe. Lissu: Ulichosikia kwenye video kwamba kukinukisha sasa tusaidie maana ya kukinukisha ni nini?
Shahidi wa kificho: muashirio ya kuchocheo fujo au vurugu.
Mhe. Lissu: Umeyatoa wapi hayo? Mimi nina kamusi ya kiswahili. Unataka nikusomeee?
Shahidi wa kificho: sio mbaya.
Mhe. Lissu: anamsomea tokwa na harufu mbaya au vunda. Na nukia na toa harufu nzuri yakunukia kama vile marashi. Haya yakwako umetoa wapi?
Shahidi wa kificho: Mimi nimesikia mitandaoni na kupitia watu pia.
Mhe.Lissu: Kwahiyo kamusi yako ni mitandao na watu?
Shahidi wa kificho: ndio.
Mhe.Lissu: Je kuna mahali kokote Polisi uliposema maana ya kukinukisha ni kufanya fujo kwenye hayo maelezo yako?
Part 164 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 163
Anaendelea Mhe. Lissu na cross examination
Watu wanacheka jamaa kuulizwa kama yeye ni mwanaume.😂😂😂
Shahidi wa kificho: Hapa hayapo ili nilihojiwa.
Mhe. Lissu: safi ukisema hayapo unaokoa muda, sasa uliulizwa kuhusu ulikuwa unafanya nini Posta ya zamani Garden na ukasema ulikuwa unaperuzi facebook whatsapp na youtube.
Sasa waeleze majaji kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako uliyonayo mkononi?
Shahidi wa kificho; Whstapp na Youtube hakuna hayajaandikwa hapa na Faceebok na Youtube hapa hayajaandikwa ila nilisema.
Mhe. Lissu: uliulizwa kuhsuu simu yako na ukasema ni smartphone sony experior galax unakumbuka ulisema hivyo?
Shahidi wa kificho: Nakumbuka.
Mhe. Lissu: je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi wa kificho: Yapo.
Mhe. Lissu: Yako wapi? Mstari wa ngapi yapo?
Shahidi wa kificho: mstari wa tano.
Mhe. Lissu: Haya soma tuone na mimi nakufuatilia.
Mhe. Lissu: Hata kama upo kwenye kiboksi utasema tu. Hayapo tukubaliane?
Shahidi wa kificho: Ila Kweli hayapo.
Mhe. Lissu: Naomba unijibu kama nakosea. Katika maelezo yako yote. Hakuna mahali kokote uliposema ulikuwa na simu kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho: nilikuwa na simu.
Mhe. Lissu: Nakuuliza kwenye maelezo yako sasa imeelezwa wapi?
Shahidi wa kificho: Hakuna humu.
Mhe. Lissu: Niko Gerezani miezi 10 kwa ushahidi wa aina hii. Umesema simu yako ulikuwa na account ya faceebook.
Shahidi wa kificho; Ni kweli.
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako: yako wapi hayo maelezo? Kwamba wewe ulikuwa na account ya Facebook?
Anasimama Ajuaye anasema Mheshimiwa naomba mshitakiwa asitoe matusi kwa shahidi.
Lissu: Sijamtukana nimemuuliza ana akili timamu au hana.
Majaji tuendelee hakuna shida.
Lissu: Ulisema ulikuwa na bando la kutosha. Onyesha kwenye maelezo.
Shahidi: yapo hayo maneno.
Lissu: nauliza kwenye maelezo yako Polisi yapo?
Shahidi: yapo nafikiri.
Jaji: Shahidi unatuchanganya. Unaulizwa kuhusu hayo maelezo uliyonayo hapo. Useme kama yapo au hayapo.
Lissu: Ulipoulizwa juu yangu ulisema kwamba unamfahamu Tundu Lissu kupitia vyombo vya habari na mitandaoni na mwanasiasa.
Shahidi: Kweli.
Lissu: onyesha kwenye maelezo yako hayo yako wapi maneno hayi.
Shahidi: Hapa hayapo.
Lissu: Ulisema Tundu Lissu alikuwa amesimama Jukwaani.
Shahidi: Kweli.
Lissu: yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi: Hapa Hayapo.
Lissu: Umesema ulimuona akiwa amevaa magwanda ya kaki, tsheti nyeusi na bendera ya taifa?
Shahidi: ni kweli.
Lissu: hayo nayo yako wapi kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi: Hawa mapolisi hawakuandika na hayo sijui kwanini.
Lissu: Ulisema ulipanda daladala kwenda ubungo na kwenda kijiwe cha kahawa cha maskani?
Shahidi: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je kwenye maelezo yako polisi na kwenda kijiwe cha Kahawa maskani? Hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho; ameunguruma hasikiki.
Mhe. Lissu: unasema?
Shahidi wa kificho: Kwa hapa sijaona.
Mhe. Lissu: Ulipofika kwenye kijiwe cha kahawa ulikuta mzozo juu ya video ya Tundu Lissu:
Shahidi wa kificho: Kweli
Mhe. Lissu: Yako wapi hayo nayo kwenye maelezo Polisi?
Shahidi wa kificho; Hapa haipo.
Part 164 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
BADO MASAA 24 TUKOMBOE NCHI YETU.
Muda kama huu Kesho nchi nzima itakuwa na MAANDAMANO ya amani tukiwa na MABANGO yetu.
NB: Tutaandamana kwa AMANI NCHI NZIMA.
REPOST 200
#D9#Disemba9Tunatoka#SiriNiNamba#TUTAKUWEPO🫵😎
@realDonaldTrump
Dear Mr. President,
My name is Mange Kimambi, and I am a Tanzanian pro-democracy activist who has been living in the United States since 2012. I am writing to bring to your attention what I believe to be a grave injustice committed against the people of Tanzania and myself by Meta, and to respectfully request your support in defending democratic activism and freedom of expression online.
Recently, my Meta accounts — including Instagram (@mangekimambi80), Instagram News media page owned by me (@wananchiforum), and my WhatsApp number (+1 424-537-3057) — were deactivated after I raised awareness about a series of severe abuses and horrific events occurring in Tanzania. These include, the kidnappings of regular citizens and kidnappings, killings and imprisonment of opposition leaders on fabricated treason charges, the barring of opposition parties from participating in the general election, widespread corruption, misuse of public funds, and the large-scale looting and exploitation of Tanzania’s natural resources by foreign governments such as the UAE, China, Oman, and most recently Russia, which is currently seeking access to Tanzania’s significant uranium deposits. Despite the country’s natural wealth, millions of Tanzanians continue to live in extreme poverty and lack even basic necessities — including clean drinking water — due to systemic corruption.
For months, I used my platforms to highlight these issues and consistently encouraged PEACEFUL protests, as many Tanzanians feel there is no safe alternative for expressing dissent. The government has been widely accused of kidnapping, torturing, or killing individuals who speak out against injustice, which makes digital communication one of the only remaining tools for civic engagement. Every post I made emphasized peaceful, non violent protests.
On October 29 2025— the day of the general election — protests led largely by Gen Z erupted across the country. These demonstrations were met with extreme state violence. Thousands of young Tanzanians were killed and many more injured as security forces responded with lethal force. The African Union, SADC, and the EU Parliament have all publicly condemned the compromised electoral process and the deadly violence that followed. Most Tanzanians view the President, Samia Suluhu Hassan — who claimed 97% of the vote — as an illegitimate president who chose to kill thousands of Tanzanian youth instead of stepping down from power. Numerous photos and videos documenting these horrific events and deaths remain visible on my X account (@mangekimambi).
My social-media platforms were essential tools for communicating with supporters, organizing peaceful civic action, and documenting human-rights abuses in real time. Their removal has severely hindered the ability of Tanzanians to access truthful information and to organize safely. Traditional media inside Tanzania has been effectively silenced; journalists who speak out risk being kidnapped, disappeared, or killed. This leaves social-media platforms run by diaspora activists like myself as one of the last remaining channels for Tanzanians to document and expose abuses.
I respectfully ask that you publicly urge Meta to reinstate my accounts without delay. I also request that you encourage Congress to consider legislation that grants activists and individuals with significant public platforms meaningful legal recourse when their accounts are removed without transparency, due process, or a clear path to appeal. Millions of people around the world — especially those advocating for democracy and human rights — depend on platforms such as Instagram, Facebook, X and TikTok to have their voices heard. In today’s world, where civic freedoms and personal safety often depend on digital communication, these companies must be held accountable.
On the same day my accounts were removed, another prominent Tanzanian activist, Maria Sarungi @MariaSTsehai saw her Instagram page