RAIS MWINYI AZINDUA BARAZA LA 11 LA WAWAKILISHI, ATOA MWELEKEO WA SERIKALI KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA NANE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi Baraza la 11 la Wawakilishi Zanzibar na kutoa mwelekeo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Nane, akisisitiza dhamira ya Serikali kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa msingi wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza leo tarehe 10 Novemba 2025, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, Unguja, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya CCM 2025β2030, pamoja na ahadi za kampeni na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Nane.
Amesema Serikali itaendeleza mageuzi ya kiuchumi kwa kuimarisha sekta za uzalishaji, uwekezaji, sekta binafsi, na matumizi ya teknolojia za kisasa, ikiwa na lengo la kuongeza ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 7 hadi 10 kwa mwaka, kudhibiti mfumko wa bei chini ya asilimia 5, kuzalisha ajira mpya 350,000, na kuongeza kipato cha mwananchi hadi Dola 1,880 kufikia mwaka 2030.
Aidha, Serikali itatekeleza ujenzi wa bandari jumuishi ya Mangapwani, bandari za abiria Mpigaduri, Kizimkazi, Shumba na Wete, pamoja na boti mbili za kisasa za mwendo kasi zitakazohudumia safari kati ya Unguja, Pemba, Tanga na Dar es Salaam.
Katika sekta ya afya, Serikali itajenga hospitali nne za mikoa, kuendeleza ujenzi wa Hospitali ya Saratani Binguni, na kuboresha Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Katika elimu, Serikali itajenga madarasa mapya 2,000, shule tatu za sekondari za wasichana kwa kila mkoa, chuo cha kisasa cha ualimu, na kuajiri walimu 7,691.
Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha utumishi wa umma kwa kuongeza mafunzo, maslahi na nidhamu ya kazi, huku taasisi za ZAECA na CAG zikiimarisha mifumo ya udhibiti wa rushwa na matumizi sahihi ya fedha za umma.
Ameongeza kuwa Afisi ya Usalama wa Shughuli za Serikali (GSO) itaongoza usimamizi wa nidhamu serikalini.
Vilevile, Serikali itajenga vituo viwili vya utamaduni Unguja na Pemba, kuendeleza michezo, na kukamilisha maandalizi ya AFCON 27.
#mwinyiapp
#yajayonineemazaidi
Nukuu za Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza akifungua Baraza la Kumi na Moja la Wawakilishi Zanzibar leo tarehe 10 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Chukwani Zanzibar.

RAIS MWINYI AMUAPISHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa mara ya pili katika Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hafla ya uapisho imefanyika leo, tarehe 08 Novemba 2025, Ikulu Zanzibar, na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka SMZ na SMT, pamoja na wanafamilia.
#mwinyiapp
#yajayonineemazaidi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kumwapisha Mhe.Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar leo tarehe 8 Novemba, 2025 Ikulu Zanzibar.
#mwinyiapp#yajayonineemazaidi
MAISHA BORA ZANZIBAR: DK. MWINYI AMELETA NURU! KATIKA UMEME NA MAJI
Tazama jinsi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi anavyotekeleza Ilani ya CCM kwa kasi ya ajabu, akibadilisha maisha ya Wazanzibari!
Mafanikio Muhimu:
β’ Umeme: Zaidi ya nyumba 138,065 zimeunganishwa na umeme, na vijiji 231 vimeingizwa kwenye gridi ya taifa.
β’ Maji Safi: Mabomba yenye urefu wa kilomita 449.93km yamewekwa, kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama saa zote!
Huu ni uthibitisho wa kasi na uongozi thabiti wa Rais Dk. Mwinyi. Zanzibar Inang'ara!
Kutazama Makala hii zaidi Bonyeza Link hapa chini
https://t.co/si0LMkGjO1
#mwinyiapp
#yajayonineemazaidi
RAIS MWINYI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Hafla ya uapisho imefanyika leo tarehe 6 Novemba 2025, Ikulu, Zanzibar.
Dkt. Mwinyi Talib Haji ameteuliwa tena kushika nafasi hiyo baada ya kuitumikia katika kipindi kilichopita.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Mhandisi, Zena Ahmed Said, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Dini.
#mwinyiapp
#yajayonineemazaidi
RAIS MWINYI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SMZ.