@SuluhuSamia Ahsante our president, mimi nitagombea natia Nia 2025 ukiiwakilisha nchi kwenye uraisi basi vivo hivo Jimbo flani ntakuwakilishia pamoja na wananchi wa Jimbo flani
Nafikiri mimi ni mtu mwenye bahati sana Duniani..!
Kila inapofika siku ya tarehe 12 May Dunia huadhimisha siku maalum ya "MAMA"
Nafikiri Duniani mimi ndiye mtu pekee mwenye mama wawili (Two mothers).
Nilipataje mama wawili? Ni hadithi ya mapenzi ya kusisimua.
Mtu na mdogo wake walionyeshana upendo wa ajabu (upendo wa agape)
Mama aliyenizaa (biological mother) aliguswa na upweke pamoja na huzuni ya mdogo wake baada ya kupata ujauzito na kuharibika kisha madaktari kumwambia hatoweza kupata tena mtoto.
Mama alikuwa mwenye huzuni na kukata tamaa ya kuishi, ndipo Dada yake akamuhaidi kutafuta mtoto na kumpatia moja kwa moja kama faraja kwake.
Mama alitimiza ahadi yake, alipojifungua aliishi na mimi siku 40, kisha akanigawa kwa mdogo wake wa tumbo moja ambaye hakuwahi kubahatika kuwa na mtoto maishani mwake.
Kwa hiyo sikuwahi kuishi naye zaidi ya siku 40, baada ya kunizaa Kisha kunikabidhi kwa mdogo wake kwa bahati nzuri kwake alikuwa tayari ana watoto watano tayari (tajiri wa watoto)
Alikuja Dar es saalam kwa mdogo wake na ujauzito, baada ya kujifungua akanikabidhi kwa mdogo wake akaondoka bila mtoto.
Hakuwahi kugeuka nyuma kurudi kudai mtoto au kuja kumuona mpaka anafariki Dunia 1997, hata aliponiona aliniona kama mtu mgeni kwake (stranger) na siyo mtoto wake.
Na mimi mara zote nilipomuona nilikimbia kwa Mama (mdogo wake) kumwambia Mama kuna mgeni kaja.
Maisha haya yaliwekezana kirahisi kwa sababu sikuwahi kulelewa na Baba na nimemuona mara 2 tu maishani mwangu kabla hajafariki
Maisha yetu sisi wawili siku zote yalikuwa yenye furaha hayakupungukiwa na kitu, sikuwahi kuhisi kukosa upendo wa mama hata kujua hadithi hii nimekuja kuijua baada ya kuadithiwa na mama mwenyewe baada ya mimi kumaliza elimu ya chuo kikuu.
Mama akanilea, akanikuza, akanisomesha na sasa najitegemea kwa malezi yake.
Nikisema nina bahati ya kuwa na mama wawili ni sababu ya hadithi hii,imagine nilipoteza Mama na nimebakia na Mama..!
Najihisi kuwa mtu mwenye bahati Duniani, heri ya siku ya Mama Duniani.
@ahmed__ally Semaji kama semaji basi wanasimba tumekua na muda flani hivi wenyee questions ila sawa ni hatua hii nayenyewe kwahiyo ipo siku furaha itarejea as awali ,,,ahsante kiongozi