Mzozo kuhusu muziki wenye sauti kubwa umeishia kwa kifo cha Msichana mwenye umri wa miaka 16, Keinerlein Rangel, baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mvulana wa miaka 10 katika Jiji la Albuquerque, Jimbo la New Mexico nchini Marekani, Oktoba 31, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi wa Albuquerque, tukio hilo lilianza baada ya Elaina Gomez-Villeda (40), Mama wa Mvulana huyo, kulalamikia muziki uliokuwa ukipigwa kwa sauti kubwa na Majirani zake ambapo mzozo huo uligeuka kuwa mapigano kati yake na Mama wa Marehemu, Susana Rangel.
Polisi wanadai kuwa Keinerlein alijaribu kuingilia kati kuzuia ugomvi huo, lakini naye akashambuliwa ambapo wakati wa vurugu hizo, Gomez-Villeda anadaiwa kumwagiza Mwanaye kwenda ndani kuchukua bastola kisha Mtoto huyo anadaiwa kurudi na kufyatua risasi moja iliyomuua Keinerlein.
Mama huyo amekamatwa na kushtakiwa kwa mauaji pamoja na makosa ya kuhatarisha usalama wa Mtoto na kumruhusu kupata silaha kwa uzembe, Mvulana huyo bado hajafunguliwa mashtaka, huku Mamlaka zikichunguza hatua zinazofaa kwa kuzingatia umri wake.
#MillardAyoUPDATES