Katibu Mtendaji wa BMT Bi. Neema Msitha akieleza jambo kuhusu tuzo za Baraza 2024 leo Mei 20, 2025 katika mkutano na Waandishi wa habari kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo Prof. Mkumbukwa M.Mtambo, tukio lililofanyika katika hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam.
#Uchaguzi wa Viongozi wa TAFF
Wagombea wa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye Ulemavu wakijinadi kwa wapiga kura katika uchaguzi wa TAFF unaofanyika leo Mei 18, 2025 katika ukumbi wa Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.
#Usaili wa wagombea nafasi za uongozi chama cha mchezo wa mpira wa miguu kwa Watu wenye Ulemavu (TAFF) umemalizika leo tarehe 17 Mei, 2025 katika wa uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika tarehe 18 Mei, 2025 uwanja wa Mkapa.
#Usaili wa wagombea wa nafasi za uongozi wa chama cha mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu (TAFF) unaendelea uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2025
Katibu mtendaji wa BMT Bi. Neema Msitha amepokea taarifa ya kukamilika kwa utafiti juu ya ushiriki wa michezo na mazoezi ya viungo nchini Tanzania kutoka kwa Tomoya Shiraishi Mtaalam mshauri wa Michezo kutoka nchini Japani ambaye anafanya kazi BMT, Mei 15, 2025.