🤔"Ni rahisi kuitamka subra, au kuihimiza subra kwa mwingine kuliko kuiishi subra yenyewe. Subra peke yake ni mtihani kuliko mtihani wenyewe unaokusubirisha."#Nasihi#NjeyaBox🕷
😲
"Kila mtu anapitia changamoto zake, kwa saizi yake na kwa namna yake. Amini tu kuwa; nyuma ya kila tabasamu la kuvutia kuna maumivu makali moyoni, kuna vita vikali na vikao vizito vinapiganwa kichwani kwa kila mtu. Usikate tamaa, pambana vita zako. Hauko peke yako."
#Valha
🤔
"Jambo hilo hilo ambalo ukisema wewe litakataliwa, linaweza kukubaliwa akilisema jambo hilo hilo mtu mwingine kwa mtu yuleyule. Ukitaka kufikisha jambo lako kwa mtu, peleleza kujua nani mtu huyo anamsikiliza kwa wepesi. Si kila kitu lazima useme wewe."
#VANDROSS🔞